Mimi nilichogundua, haka katoto kameamua rasmi kuichafua shule ya Pandahill, lakini pia kujaribu kumharibia kazi yake huyo mwalimu Jimmy!
Ingawa naamini vyote viwili havitafanikiwa. Maana siku zote kwenye ukweli, uongo hujitenga. Huyo mtoto kabla ya kulalamikia kubakwa na huyo mwalimu, angetujibu haya maswali yetu kwanza;
1. Kwanini baada ya kubakwa hakutoa taarifa kwa kiongozi wake wa bweni, Matron, Mkuu wa shule, nk?
2. Kwanini baada ya kutoroka shule, hakutoa taarifa kwa wazazi wake juu ya hilo tukio la ubakaji? Au hata kuwapigia tu simu ili kuomba msaada?
3. Kwanini alipotoroka alikimbilia kwa muuza mkaa (baba Jose), aliyeishi naye kinyumba kwa zaidi ya mwezi mmoja mpaka huyo Baba Jose alipoenda kumuombea hifadhi kwa mama muuza genge? (Na inawezekana ni baada ya Rc wa Mbeya kutangaza lile dau la mil. 5 bila shaka, akaona mambo yatakuwa magumu kwake)
4. Kwa nini alipokuwa kwa mama muuza genge alidanganya taarifa zake muhimu kama majina yake, mahali anapotokea, shughuli anayofanya, nk?
Ajibu kwanza haya maswali yetu, ili tuone ukweli ulipo.