Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Bro hivi ushawai kukaa chini na kuongea na mabinti hasa hawa walio sekondari na wakakuambia ukweli kabisa wa maisha yao wanayoishi wao kwa wao hasa wakike wanaotumia simu wanaoishi bweni au hata nyumbani?

Kuna wengine wameanza kutumia simu toka kitambo tu na wengine iyo elimu wamepata ya matumizi mazuri ya vifaa vya teknolojia lakini Mkuu bado wanachofanya ni madudu yaani hao watoto wanaishi kimakundi yani kama kaoza mmja basi wote nao ni hivyo hivyo asee ni changamoto sana.
 
Wewe mwalimu usifuate ushauri huu. Kesho mchape mwanafunzi afe halafu uone kama mamlaka zitasema usilete utamaduni wa kimagharibi. Sijui kwanini walimu kila siku hamjifunzi?
 
Yaani huu uzi umenifungua sana macho. Nimegundua mambo matatu.
Mosi,wana JF wengi ni "makatili" (sadists) sana.
Pili, wana JF wengi ni walimu.
Tatu, moja ya sababu za msingi sana za kuwa na elimu ya hovyo na wahitimu wa hovyo ni walimu wa hovyo.
Kama taifa,hatuwezi kuwa wastaarabu kama tutaendeleza matendo yale yale ya kikoloni na kitumwa.
Hatuwezi tukawa taifa la kuhukumu kwanza bila ya kupata uhakika wa kile kilichotokea,kama ambavyo asilimia kubwa ya wachangiaji walivyomuhukumu huyo binti mchapwa viboko.

Napenda kutoa ushauri kwa serikali kuhakikisha hizi kada mbili za ualimu na upolisi, zinapatiwa mafunzo stahiki ya kisaikolojia kulingana na wakati uliopo, pamoja na kuangaliwa kwa stahili zao.

Wazazi nao watimize majukumu yao kwa kuwalea watoto katika njia iwafaayo.
 
Usiseme sasa hv maana ata wakubwa wa sasa bado effects za viboko vilivyopitiliza wanazo ila hawajijui tu. Na Matokeo yake anashindwa ata kudai haki yake ye mwenyewe maana toka mwanzo hakujengewa kujiamin
Napokea taarifa mkuu naelewa sana hilo tatizo na linakua siku hadi siku
 
Kwahiyo mkuu unashauri viboko vitumike mtu achapwe viboko 50 maana adhabu ya viboko pia kuwa watu wanakua sugu huwezi mchapa mwanafunzi viboko vitano ili akome utaenda mpaka 50 sasa mkui viboko 50 au hata viboko 20 huoni unaelekea pabaya, nikuilize tu mara pah umemchapa ukampoteza mtoto wa watu utawajibu nini wazazi wake muangalia na side effect ya adhabu,

Mkuu ukiniambia kulima unazoea ni kama shuguli za nyumbani unakosea mashamba ya shule ni makubwa acha adhabu ya kulima zipo nyingi ambazo mtoto sio rahisi akawa mkaidi kwa kuzoea adhabu na mtoto akishakua kwenye hiyo stage ya ukomavu wa adhabu hata ukitumia fimbo hatasikia zaidi atakuongezea hasira utampiga vibaya
 
Hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa hao waalimu kwa kutoa adhabu ndogo kama hiyo. Ilitakiwa kila siku saa 8 mchana huyo mwanafunzi apate viboko kumi kwa wiki nzima. Yaani kabla ya chakula cha mchana apite ofisini kupata viboko 10 kila siku kwa wiki moja
 
ushaid sasa video pleas!!,, maana wazaz wa siki hiz mnalea wtt kama mayai ndo maana tuna mapolomoko makubwa ya madili kwa wtt wetu,, hamtak wtt waguswe na walimu, tupe usahid wa hizo fimbo 20 ndo tutowe go ahead,,,.
 
Wewe mwalimu usifuate ushauri huu. Kesho mchape mwanafunzi afe halafu uone kama mamlaka zitasema usilete utamaduni wa kimagharibi. Sijui kwanini walimu kila siku hamjifunzi?
Mimi sio mwalimu, ila shule iliyo karibu yangu mboko zinachapwa kama hawachapi tena vile na madogo wananyooka.
 
Walimu huwa ni wapumbavu sana. Huwa wana mob psychology
Ukitafakari vema utaona pia athari za mob psychology kwa wazazi na walezi dhidi ya walimu.

Mtoto wa wazazi wasiojitambua in mzigo kwa walimu, halikadharika mwanafunzi wa mwalimu asiyejitambua yuko hatarini na ni janga kwa Taifa.

Kila MTU acheze nafasi yake vema, tutimize wajibu wetu bila kujali wengine.
 
Sio kila kitu ni cha kuiga kwa aliefanikiwa wewe?? Kwahiyo ukiwa raisi wewe unaweza kuhalalisha ushoga kisa ni kutoka nchi iliyoendelea??

Hatukatai ni viziri kuiga kutoka kwa waliofanikiwa lakini sio kila kitu na pia hadi kufikia hapo kuna stages walizipitia hawakuibuka from no where wakawa hapo.
Hao marekani wamepata uhuru almost miaka 300+ iliyopita, utajifananisha na ww uliepata uhuru miaka 58 sijui.

Walianza transformation many years back, na hayo mabadiliko ni muda mrefu, kuimpose culture kwa watu si jambo dogo ndgu yangu.

Kibongo bongo mtoto usimpoletea ukauzu kiasi ipo siku atakuabisha sana kama sio yeye kuharibika vibaya sana.
 
Wewe mwalimu usifuate ushauri huu. Kesho mchape mwanafunzi afe halafu uone kama mamlaka zitasema usilete utamaduni wa kimagharibi. Sijui kwanini walimu kila siku hamjifunzi?
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Safi mkuu
 
Mimi sio mwalimu, ila shule iliyo karibu yangu mboko zinachapwa kama hawachapi tena vile na madogo wananyooka.
Ni kuanzia viboko vingapi mtoto akichapwa atakua anaogopa adhabu ya viboko, nijuavyo mimi viboko lazima uchapwe mpaka uombe msamaha au uchapwe mpaka mwalimu afurahi roho na nafsi yake, sasa mnataka muue watoto kisa?!??
 
Ni kuanzia viboko vingapi mtoto akichapwa atalua anaogopa adhabu ya viboko, nijuavyo mimi viboko lazima uchapwe mpaka uombe msamaha au uchapwe mpaka mwalimu afurahi na nafsi yake, sasa mnata muue watoto kisa?!??
Sio kuua ni kuadabisha.
 
Sio kuua ni kuadabisha.
Kwani unavyoanza kuchapa unajua kama utaua, unajua ukichapa huwa kuna hasira nyuma ya lile tendo unalolifanya sasa ukianza kuchapa unakua huna dhamira ya kuua ila unaposhika bakora na kuanza kuchapa kila neno lake moja mwanafunzi wewe mwalimu unakazia mtoto anasema nimekosa sitarudia tena wewe ndiyo unazidisha kumla fimbo moyo wako unasema ngoja huyu leo mpaka akome unajua madhara ya hiyo dhana
 
Waalimu ni watu wenye Misongo sana ya Mawazo hasa wa hizi Shule za Serikali,
Sipati Picha angekua Mwanangu wangeifunga hiyo Shule kwa muda.

Upo sahihi Mtoa Mada Adhabu za Viboko ni Ukatili, Utumwa na Ujinga.
 
Mimi nimesema kila utamaduni wa kuiga kutoka magharibi?
 
Walimu wengine mnawapiga sana watoto wakike kumbe nyuma ya pazia mna ajenda huenda mtoto alikukataa kimapenzi sasa unalazimisha awe mchumba wako, mtoto amekutosa wewe umekaza tafuta malaya huko sasa ole wako wewe mwalimu unae wanayanyasa watoto kwa viboko vikali kwa stayle zake ujue tu karma itakurudia tu, huna maisha marefu utaingia mtegoni
 
Waalimu ni watu wenye Misongo sana ya Mawazo hasa wa hizi Shule za Serikali,
Sipati Picha angekua Mwanangu wangeifunga hiyo Shule kwa muda.

Upo sahihi Mtoa Mada Adhabu za Viboko ni Ukatili, Utumwa na Ujinga.

Wewe ndiyo mzazi mwenye uchungu na manyanyaso ya watoto sio wengine , walimu wengi ni vijana hawajapata watoto so wanapiga tu watoto, halafu hao hao wanatongoza watoto wetu wanawalazimisha watembee nao
 
Nadhani hili ndio la kuzungumziwa....na sio Mayai tu,,,, hata Nidhamu hawana kabisa......

Na kupitia hii dhana ya Umayai imefanya Walimu waachane nao,,,,na kutengeneza kizazi cha ajabu kweli....
Ni hivi uzazi umekuwa wa shida sana watoto wengi wanazaliwa na shida wabovu wabovu ,sio kama zamani watoto wa sasa ni wapyaa unaweza mnasa kibao akafa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…