Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Huo ulimbukeni upo ata kwa watoto wa ulaya. Shida inaanzia kwenye familia.
Wewe kama mzazi uliishawai kaa na watoto wako ukawapa elimu juu ya gadgets za mawasiliano (simu, computer, internet nk) ? Uliishawai wapa nafasi ya kutumia vifaa vya mawasiliano huku ukifatilia kwa ukaribu? Na jua utajibu "NO" bas ata ww na utu uzima wako ukiletewa kitu kipya ambacho ulikuwa unazuiliwa kukitumia mda kwa mda mrefu lazma utakuwa limbukeni.
Bro hivi ushawai kukaa chini na kuongea na mabinti hasa hawa walio sekondari na wakakuambia ukweli kabisa wa maisha yao wanayoishi wao kwa wao hasa wakike wanaotumia simu wanaoishi bweni au hata nyumbani?

Kuna wengine wameanza kutumia simu toka kitambo tu na wengine iyo elimu wamepata ya matumizi mazuri ya vifaa vya teknolojia lakini Mkuu bado wanachofanya ni madudu yaani hao watoto wanaishi kimakundi yani kama kaoza mmja basi wote nao ni hivyo hivyo asee ni changamoto sana.
 
Zimebadilika lini hizo zama!?
Yani unataka kuleta umagharibi huku, nyie ndo mnaharibu watoto wenu kwa kutowachapa kosawasawa eti zama zimebadilika.

Viboko 20 wala sio vingi kiasi hicho mpaka mtoto aumie au azimie labda kama walikua wanamchapa bila utaratibu yaani wanachapa popote tu ila kama mboko 20 kwa kalio mbona zinakaa fresh kabisa.
Wewe mwalimu usifuate ushauri huu. Kesho mchape mwanafunzi afe halafu uone kama mamlaka zitasema usilete utamaduni wa kimagharibi. Sijui kwanini walimu kila siku hamjifunzi?
 
Yaani huu uzi umenifungua sana macho. Nimegundua mambo matatu.
Mosi,wana JF wengi ni "makatili" (sadists) sana.
Pili, wana JF wengi ni walimu.
Tatu, moja ya sababu za msingi sana za kuwa na elimu ya hovyo na wahitimu wa hovyo ni walimu wa hovyo.
Kama taifa,hatuwezi kuwa wastaarabu kama tutaendeleza matendo yale yale ya kikoloni na kitumwa.
Hatuwezi tukawa taifa la kuhukumu kwanza bila ya kupata uhakika wa kile kilichotokea,kama ambavyo asilimia kubwa ya wachangiaji walivyomuhukumu huyo binti mchapwa viboko.

Napenda kutoa ushauri kwa serikali kuhakikisha hizi kada mbili za ualimu na upolisi, zinapatiwa mafunzo stahiki ya kisaikolojia kulingana na wakati uliopo, pamoja na kuangaliwa kwa stahili zao.

Wazazi nao watimize majukumu yao kwa kuwalea watoto katika njia iwafaayo.
 
Usiseme sasa hv maana ata wakubwa wa sasa bado effects za viboko vilivyopitiliza wanazo ila hawajijui tu. Na Matokeo yake anashindwa ata kudai haki yake ye mwenyewe maana toka mwanzo hakujengewa kujiamin
Napokea taarifa mkuu naelewa sana hilo tatizo na linakua siku hadi siku
 
Nakuelewa sana Mkuu,,, Hoja zako pia zijikite kwenye Uhalisia wa Mazingira,,, adhabu za kufanya kazi zinahusisha PUMZI,,,na hili kwa wenye matatizo ya Afya ni baya zaidi,,, Impact ya Bakora ni yale Maumivu mtu hupata....na ile ndio hufanya asirudie kufanya kosa tena.....

Vijijini huko hizo adhabu ulizosema sio adhabu,,,kwa sababu ni kazi watoto huzifanya majumbani kwao kila siku,,(kulima, kufagia, kufyeka,kufyatua tofali n.k),,,,so ukiwafanyisha kwao inakuwa sio adhabu....

Vijana wengi kusoma huwa ni kama adhabu kwao,,,,na ndio maana Mwalimu asipoingia kwenye kipindi wanafunzi wanafurahi,,,,,,sasa kitendo cha Mwanafunzi kufyeka masaa mawili ni anapoteza sana wakati ilihali angekula Bakora 5 tu akarudi darasani bado lengo litakuwa ni lile lile....

Nimechoka kuandika LAKINI Adhabu ya Bakora bado ni Sahihi sana kuliko hizo zingine kwa Wanafunzi,,,,,,Swala la kufa hata hizo adhabu zingine mtoto anaweza kufa pia kwasababu zinahusisha Nguvu,,Pumzi na zinataka mtoto awe na Afya njema kuzifanya,,,,,Yaleyale tu,,,,BUT BAKORA binafsi naona is the Best.
Kwahiyo mkuu unashauri viboko vitumike mtu achapwe viboko 50 maana adhabu ya viboko pia kuwa watu wanakua sugu huwezi mchapa mwanafunzi viboko vitano ili akome utaenda mpaka 50 sasa mkui viboko 50 au hata viboko 20 huoni unaelekea pabaya, nikuilize tu mara pah umemchapa ukampoteza mtoto wa watu utawajibu nini wazazi wake muangalia na side effect ya adhabu,

Mkuu ukiniambia kulima unazoea ni kama shuguli za nyumbani unakosea mashamba ya shule ni makubwa acha adhabu ya kulima zipo nyingi ambazo mtoto sio rahisi akawa mkaidi kwa kuzoea adhabu na mtoto akishakua kwenye hiyo stage ya ukomavu wa adhabu hata ukitumia fimbo hatasikia zaidi atakuongezea hasira utampiga vibaya
 
Hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa hao waalimu kwa kutoa adhabu ndogo kama hiyo. Ilitakiwa kila siku saa 8 mchana huyo mwanafunzi apate viboko kumi kwa wiki nzima. Yaani kabla ya chakula cha mchana apite ofisini kupata viboko 10 kila siku kwa wiki moja
 
Walimu 6 wa Jangwani Sekondari jijini Dar es salaam wamemhukumu kwa kumchapa makalioni fimbo 20 mwanafunzi wa kike wa kidato cha tatu na kumjeruhi vibaya kwa tuhuma za kuwa alionekana ameshika simu.

Mwalimu aliyesema hivyo alimvua nguo na kumpekua kila mahala na hakukuta simu. Alimchukua hadi ofisi ya walimu na kumlazimisha akiri lakini alikataa ndipo walimu 6 wakamshushia kipigo cha fimbo 20.

Mmoja alimchapa 5 wawili 4 kila mmoja, mmoja 3 na wawili 2 kila mmoja. Wapo walimu wa kiume na wa kike waliofanya kipigo hiki. Alipoona kipigo kina zidi aliropoka kuwa yeye hana simu bali aliye na simu ni mwenzake.

Huyo aliyetajwa kachukuliwa hatua japo mzazi alikuja kukiri binti yake kuwahi kuwa na simu.

Huyu binti aliyechapwa alihamishiwa shuleni hapo na kuishi bweni akitokea mkoani kutokana na tatizo la kiafya. Hali hiyo bado ilikuwa inamsumbua na zipo kumbukumbu katika hospitali za Dar na huko alikotoka lakini baadhi ya walimu wanasema anajifanyisha hivyo kushindikiza atolewe bweni azma ambayo wameipitisha pamoja na hicho kipigo.

Tatizo jingine ni imani kwa kuwa jitihadi za kumbadili kupitia ugonjwa zilipo shindikana wanasema haumwi.

Wapo wanafunzi walibadilishwa na kwenda upande wa hao walimu.

Tunaomba TAMISEMI, Polisi na Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto wafuatilie suala hili. Huyu binti ni mgonjwa sasa akiwa mwanafunzi wa kutwa akipata tatizo njiani nani wa kuwajibika.

Mtoto wa kike anadhalilishwa fimbo 20 shule tena kwenye makalio.

Tupaze sauti.
ushaid sasa video pleas!!,, maana wazaz wa siki hiz mnalea wtt kama mayai ndo maana tuna mapolomoko makubwa ya madili kwa wtt wetu,, hamtak wtt waguswe na walimu, tupe usahid wa hizo fimbo 20 ndo tutowe go ahead,,,.
 
Wewe mwalimu usifuate ushauri huu. Kesho mchape mwanafunzi afe halafu uone kama mamlaka zitasema usilete utamaduni wa kimagharibi. Sijui kwanini walimu kila siku hamjifunzi?
Mimi sio mwalimu, ila shule iliyo karibu yangu mboko zinachapwa kama hawachapi tena vile na madogo wananyooka.
 
Walimu huwa ni wapumbavu sana. Huwa wana mob psychology
Ukitafakari vema utaona pia athari za mob psychology kwa wazazi na walezi dhidi ya walimu.

Mtoto wa wazazi wasiojitambua in mzigo kwa walimu, halikadharika mwanafunzi wa mwalimu asiyejitambua yuko hatarini na ni janga kwa Taifa.

Kila MTU acheze nafasi yake vema, tutimize wajibu wetu bila kujali wengine.
 
Etii umagharibi. Kuna kitu gani unachotumia wewe hakijatokea magharibi? Utamaduni wa Mtanzania unasukumwa na utamaduni wa kimagharibi. Kila kitu unachotumia wewe kimetokea magharibi au kimegunduliwa magharibi halafu hapa unajifanya kupinga umagharibi. Pia mkuu kama unataka kufanikiwa unajifunza kutoka kwa mtu aliyefanikiwa siyo unajifunza kwa mtu aliyeshindwa. Utamaduni wa magharibi umeonekana kuwa na tija na kufanikiwa ingawa siyo utamaduni wote ni wa kuiga. Sasa kujifunza namna wa magharibi walivyo weza kustaaribika ni vibaya?
Sio kila kitu ni cha kuiga kwa aliefanikiwa wewe?? Kwahiyo ukiwa raisi wewe unaweza kuhalalisha ushoga kisa ni kutoka nchi iliyoendelea??

Hatukatai ni viziri kuiga kutoka kwa waliofanikiwa lakini sio kila kitu na pia hadi kufikia hapo kuna stages walizipitia hawakuibuka from no where wakawa hapo.
Hao marekani wamepata uhuru almost miaka 300+ iliyopita, utajifananisha na ww uliepata uhuru miaka 58 sijui.

Walianza transformation many years back, na hayo mabadiliko ni muda mrefu, kuimpose culture kwa watu si jambo dogo ndgu yangu.

Kibongo bongo mtoto usimpoletea ukauzu kiasi ipo siku atakuabisha sana kama sio yeye kuharibika vibaya sana.
 
Wewe mwalimu usifuate ushauri huu. Kesho mchape mwanafunzi afe halafu uone kama mamlaka zitasema usilete utamaduni wa kimagharibi. Sijui kwanini walimu kila siku hamjifunzi?
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Safi mkuu
 
Mimi sio mwalimu, ila shule iliyo karibu yangu mboko zinachapwa kama hawachapi tena vile na madogo wananyooka.
Ni kuanzia viboko vingapi mtoto akichapwa atakua anaogopa adhabu ya viboko, nijuavyo mimi viboko lazima uchapwe mpaka uombe msamaha au uchapwe mpaka mwalimu afurahi roho na nafsi yake, sasa mnataka muue watoto kisa?!??
 
Ni kuanzia viboko vingapi mtoto akichapwa atalua anaogopa adhabu ya viboko, nijuavyo mimi viboko lazima uchapwe mpaka uombe msamaha au uchapwe mpaka mwalimu afurahi na nafsi yake, sasa mnata muue watoto kisa?!??
Sio kuua ni kuadabisha.
 
Sio kuua ni kuadabisha.
Kwani unavyoanza kuchapa unajua kama utaua, unajua ukichapa huwa kuna hasira nyuma ya lile tendo unalolifanya sasa ukianza kuchapa unakua huna dhamira ya kuua ila unaposhika bakora na kuanza kuchapa kila neno lake moja mwanafunzi wewe mwalimu unakazia mtoto anasema nimekosa sitarudia tena wewe ndiyo unazidisha kumla fimbo moyo wako unasema ngoja huyu leo mpaka akome unajua madhara ya hiyo dhana
 
Waalimu ni watu wenye Misongo sana ya Mawazo hasa wa hizi Shule za Serikali,
Sipati Picha angekua Mwanangu wangeifunga hiyo Shule kwa muda.

Upo sahihi Mtoa Mada Adhabu za Viboko ni Ukatili, Utumwa na Ujinga.
 
Sio kila kitu ni cha kuiga kwa aliefanikiwa wewe?? Kwahiyo ukiwa raisi wewe unaweza kuhalalisha ushoga kisa ni kutoka nchi iliyoendelea??

Hatukatai ni viziri kuiga kutoka kwa waliofanikiwa lakini sio kila kitu na pia hadi kufikia hapo kuna stages walizipitia hawakuibuka from no where wakawa hapo.
Hao marekani wamepata uhuru almost miaka 300+ iliyopita, utajifananisha na ww uliepata uhuru miaka 58 sijui.

Walianza transformation many years back, na hayo mabadiliko ni muda mrefu, kuimpose culture kwa watu si jambo dogo ndgu yangu.

Kibongo bongo mtoto usimpoletea ukauzu kiasi ipo siku atakuabisha sana kama sio yeye kuharibika vibaya sana.
Mimi nimesema kila utamaduni wa kuiga kutoka magharibi?
 
Walimu wengine mnawapiga sana watoto wakike kumbe nyuma ya pazia mna ajenda huenda mtoto alikukataa kimapenzi sasa unalazimisha awe mchumba wako, mtoto amekutosa wewe umekaza tafuta malaya huko sasa ole wako wewe mwalimu unae wanayanyasa watoto kwa viboko vikali kwa stayle zake ujue tu karma itakurudia tu, huna maisha marefu utaingia mtegoni
 
Waalimu ni watu wenye Misongo sana ya Mawazo hasa wa hizi Shule za Serikali,
Sipati Picha angekua Mwanangu wangeifunga hiyo Shule kwa muda.

Upo sahihi Mtoa Mada Adhabu za Viboko ni Ukatili, Utumwa na Ujinga.

Wewe ndiyo mzazi mwenye uchungu na manyanyaso ya watoto sio wengine , walimu wengi ni vijana hawajapata watoto so wanapiga tu watoto, halafu hao hao wanatongoza watoto wetu wanawalazimisha watembee nao
 
Nadhani hili ndio la kuzungumziwa....na sio Mayai tu,,,, hata Nidhamu hawana kabisa......

Na kupitia hii dhana ya Umayai imefanya Walimu waachane nao,,,,na kutengeneza kizazi cha ajabu kweli....
Ni hivi uzazi umekuwa wa shida sana watoto wengi wanazaliwa na shida wabovu wabovu ,sio kama zamani watoto wa sasa ni wapyaa unaweza mnasa kibao akafa
 
Back
Top Bottom