Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Sasa hivi una muona hana akili, ila subiri mamlaka zichukue hatua ndiyo utajua kuwa jamaa ana akili au hana akili. Au subiri huyo mwanafunzi apatwe na madhila mabaya zaidi ndiyo utajua reaction ya watu. Atakaye teseka ni mwalimu/walimu waliohusika na hilo tukio. Walimu sijui hawajifunzi kutokana na matukio ya siku za nyuma. Pia nyakati zimebadilika sana. Kila kimebadilika sana, na mabadiliko huwezi kuyazuia wewe. Suala la fimbo sikatai ila fimbo 20 hapo Hapana. Times have changed. Hatuwezi kuendelea kuishi kwa kutumia akili na nadharia za karne ya 20. Sasa hivi ni karne ya 21 kaka. Dunia imebadilika kwenye kila eneo pamoja na kwenye namna ya kutoa adhabu. Sasa wamemchapa huyo mwanafunzi, nini wamenufaika? Na hii habari aliyoanzisha huyo jamaa itaelea kama upepo. Huna uwezo wa kuzuia siku hizi kutoa habari kwa sababu kila mmoja amepewa platform ya kutoa habari. Wasalam
Unatetea uovu wa mwanafunzi.
mleta hoja aliegemea kulalamikia walimu bila kueleza uhalisia watukio lenyewe.

Shule sio kanisani kwamba mwanafunzi afanye vile anataka..kuchapa atachapwa tu no way out mkuu.
 
Huna akili wewe.
Nyie ndio mnalea ujinga kwa watoto
Tupoteze muda kwa swala la malezi mabovu kwa mtoto wako. Kwanza hao walimu wangeongeza idadi zifike fimbo 100 kwa tako moja.
Ameenda kusoma au kuchati na kupiga picha walimu..
Ficha ujinga wako mkuu

Soma maelezo tena mkuu,,
Alipoona kipigo kina zidi aliropoka kuwa yeye hana simu bali aliye na simu ni mwenzake.

Huyo aliyetajwa kachukuliwa hatua japo mzazi alikuja kukiri binti yake kuwahi kuwa na simu.

Afrika ukatili umepitiliza,,huwa najaribu sana kuwatetea walimu especially kwenye ishu ya salary,,, however, kwa kitendo hichi cha kumpiga mwanafunzi wa kike, isitoshe matakoni!!!, hapana aise. mwanamke hapigwi matakoni, ni kumdhalilisha, wajifunze shule za kiislamu, zina maadili hawana upumbavu kama shule za upande wa pili.
 
Unatetea uovu wa mwanafunzi.
mleta hoja aliegemea kulalamikia walimu bila kueleza uhalisia watukio lenyewe.

Shule sio kanisani kwamba mwanafunzi afanye vile anataka..kuchapa atachapwa tu no way out mkuu.

Kama nikweli alikutwa na simu, japo hakuna evidence yoyote, ni tuhuma tu. So,,Hawakupaswa kupigwa, ungefanyika uchunguzi kwanza.
 
Walimu 6 wa Jangwani Sekondari jijini Dar es salaam wamemhukumu kwa kumchapa makalioni fimbo 20 mwanafunzi wa kike wa kidato cha tatu na kumjeruhi vibaya kwa tuhuma za kuwa alionekana ameshika simu.

Mwalimu aliyesema hivyo alimvua nguo na kumpekua kila mahala na hakukuta simu. Alimchukua hadi ofisi ya walimu na kumlazimisha akiri lakini alikataa ndipo walimu 6 wakamshushia kipigo cha fimbo 20.

Mmoja alimchapa 5 wawili 4 kila mmoja, mmoja 3 na wawili 2 kila mmoja. Wapo walimu wa kiume na wa kike waliofanya kipigo hiki. Alipoona kipigo kina zidi aliropoka kuwa yeye hana simu bali aliye na simu ni mwenzake.

Huyo aliyetajwa kachukuliwa hatua japo mzazi alikuja kukiri binti yake kuwahi kuwa na simu.

Huyu binti aliyechapwa alihamishiwa shuleni hapo na kuishi bweni akitokea mkoani kutokana na tatizo la kiafya. Hali hiyo bado ilikuwa inamsumbua na zipo kumbukumbu katika hospitali za Dar na huko alikotoka lakini baadhi ya walimu wanasema anajifanyisha hivyo kushindikiza atolewe bweni azma ambayo wameipitisha pamoja na hicho kipigo.

Tatizo jingine ni imani kwa kuwa jitihadi za kumbadili kupitia ugonjwa zilipo shindikana wanasema haumwi.

Wapo wanafunzi walibadilishwa na kwenda upande wa hao walimu.

Tunaomba TAMISEMI, Polisi na Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto wafuatilie suala hili. Huyu binti ni mgonjwa sasa akiwa mwanafunzi wa kutwa akipata tatizo njiani nani wa kuwajibika.

Mtoto wa kike anadhalilishwa fimbo 20 shule tena kwenye makalio.

Tupaze sauti.
Duh, we jamaa 20 strokes unalalama hivi!! Mimi nilishawahi kuchapwa 60 na nikala ubuyu tu fresh. Muache mtoto arekebishwe.
 
Yaan viboko 20 unaongea? Cc tulikuwa tunachapwa 50 na tunatoka fresh. Acheni ujinga bana
 
Kuna adhabu za kuwapa watoto na sio mabakora. Ndio maana tunaonekana manyani meusi yasiyo na akili.
Mpe jembe akalime/afyeke/asafishe vyoo vya shule/apige magoti aite mvua mpaka wenzake wakitoka darasani/apewe suspension/alazimishwe asome vitabu kadhaa na aviandikie muhtasar la sivyo anafukuzwa shule n.k nk. mpe adhabu za kumjenga na sio kudhalilisha utu wa
Akalime, afyeke, 'apige magoti aite mvua hadi wenzake watoke'..

Kwamba hizo adhabu hazidhalilishi utu wake au unataka kusema nn?
 
Watu tumepigwa fimbo 100 na bado hata huelew kesho unarudia kosa.

Yan hawa wanafunzi wa dar aisee

NB; mkuu huyo mwanafunzi ni demu wako
 
Afrika ukatili umepitiliza,,huwa najaribu sana kuwatetea walimu especially kwenye ishu ya salary,,, however, kwa kitendo hichi cha kumpiga mwanafunzi wa kike, isitoshe matakoni!!!, hapana aise. mwanamke hapigwi matakoni, ni kumdhalilisha, wajifunze shule za kiislamu, zina maadili hawana upumbavu kama shule za upande wa pili.
Upande wa pili wanachapa sana watoto wait tangu vikiwa vichanga.

Wanakuwa wamezoea bakora.. hata malalamikaji kwenye kesi hiyo inaonekana so wa upande huo wa pili kwani asingethubutu kufungua mdomo wake.

Tatizo ni kuonekana na simu shuleni kinyume na taratibu za shule. Kahojiwa kakataa makusudi. Huenda na madharau juu.

Walimu ni binadanu.

Wazazi tufundisheni watoto wetu utii wa sheria bila shuruti. Wafuate sheria, kanuni na taratibu za kila pahala wanapokuwa.
 
Ungewataja hao waalimu, hasira za ugumu wa maisha wanamalizia watoto.
 
Tangu uhuru hili taifa limekuwa na watu wengi kama nyie mnaopiga watoto kama mifugo na halijfika popote.
Wengi wanaounga mkono huu ujinga ni ama ni waalimu au wahanga wa kuchapwa bakora utotoni mwao. Wengi maskini hawajui kama waliathiriwa kisaikolojia.
Twende nao tu hawa watu wazima wahanga wa ukatili utotoni/ujanani mwao.
 
Wakati huohuo mtoto akikosa kipindi nongwa!

Acheni kukariri
Nani kasema nongwa?
Kukosa kipindi ni sehemu pia ya adhabu ambayo kimsingi naiunga mkono.
Bakora ni utumwa na inatweza utu wa mtu. Historia ya bakora inaenda sanjari na asili ya utumwa. Kuna namna nyingi za kumuadhibu mtoto/mwanafunzi.
 
Hao waalimu wachukuliwe hatuna kwa kutoa adhabu ndogo

Ilitakiwa adhabu iwe kubwa kuliko hiyo

Walimu wapewe nguvu labda itasaidia kupunguza mmomonyoko wa maadili
Maadili hayajengwi hvyo. Kama unategemea huyo mwalimu anae shinda na mwanafunzi masaa 8 per day kwa siku 5 ndani ya wiki atengeneze mwanafunzi mwenye maadili. Maadili msingi wake ni familia ndio zinakuja hizo taasisi nyingne.
 
Back
Top Bottom