Mwanafunzi Esther wa Panda Hill aliyepotea kwa siku 35 amepatikana, yadaiwa alitoroshwa na mchoma mkaa

Mwanafunzi Esther wa Panda Hill aliyepotea kwa siku 35 amepatikana, yadaiwa alitoroshwa na mchoma mkaa

Hatimaye Ester Noah Mwanyiru mwanafunzi wa sekondari ya Pandahill aliyetoweka 18 May 2023 amepatikana.

Taarifa iliyotolewa na mama yake mzazi inaeleza amepatikana wilayani Mbalizi kwa mama fundi cherehani. Alibadili jina kuwa Erica na amekua akivaa Hijab inayofunika uso, na kuacha macho tu na hivyo kuwa ngumu kutambulika.

Chanzo cha kupatikana ni baada ya binti mmoja wa Mbalizi kusimuliwa kisa cha Ester na kudai amemuona kwa mama mmoja fundi cherehani. Leo asubuhi polisi wamevamia nyumba ya mama huyo na kumkuta Ester. Wote wawili wapo kituo cha Polisi Mbalizi kutoa maelezo.

#MyTake:
Simulizi ya kupotea kwa Ester na kupatikana kwake inaacha maswali mengi kuliko majibu.

1. Ester alitoroka shuleni baada ya kukutwa akifanya udanganyifu kwenye mtihani. Akachapwa viboko vitatu, kisha akapewa mtihani mwingine afanye. Lakini polisi walipoenda shuleni hakukua na mtihani wowote Ester aliofanya. Je mitihani yake ilienda wapi?

2. Shule ya Pandahill ina ukuta (fence) ya urefu wamita 3 na juu kuna nyaya za umeme. Inawezekanaje mtoto wa kike kuruka ukuta wa mita 3 wenye umeme?

3. Matron wa shule anasema Ester alitoroka na mwenzie mmoja na walikimbizwa hawakupatikana. Hata hivyo "rall call" ilipofanyika wanafunzi wote walikuwepo isipokua Ester tu. Je huyo aliyekimbia na Ester akiwa kwenye sare za shule ni nani?

4. Barua aliyoacha Ester alidai kuonewa na Mwalimu Jimmy, japo hakutaja uonevu huo. Kwanini hakwenda nyumbani kuwaeleza wazazi badala ya kukimbilia Mbalizi?

5. Kwanini Headmaster alienda kwa wazazi wa Ester kutoa pole?

6. Huyo mama wa Mbalizi aliwezaje kumpokea binti asiyemfahamu na kukaa nae comfortably?

7. Aliishi kwa huyo mama kama nani? Housegirl au?

8. Inaelezwa alienda kwa huyo mama na Hijab. Aliipata wapi? Sare za shule alizototoka nazo aliziacha wapi?

9. Alibadili jina kuwa Erica lakini akavaa Hijab. Huyo mama hakujiuliza iweje mtoto wa Kikristo kuvaa Hijab?

10. Binti aliyetoa taarifa kuwa amemuona Ester Mbalizi alimtambuaje ikiwa alivaa Hijab ya kufunika uso na kubakiza macho tu?

NB: Tunamshukuru Mungu Ester amepatikana akiwa mzima, lakini kwa kuwa suala hili limepaziwa sauti na umma, basi ni vema umma ukapewa majibu ya kuridhisha.!
The search finally has ended with fruitful results.. Mengine atayaongea mlengwa maana bado yuko hai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom