Mwanafunzi Esther wa Panda Hill aliyepotea kwa siku 35 amepatikana, yadaiwa alitoroshwa na mchoma mkaa

Mwanafunzi Esther wa Panda Hill aliyepotea kwa siku 35 amepatikana, yadaiwa alitoroshwa na mchoma mkaa

kabisaa ndo ninachokionaa hapaa

Kwa binti WA umri huyo anaakili kabisa. Ni MTU mzima.
Kuna Binti akipotea zaidi ya miezi mitatu, alikuwa kidato cha tatu, Baba yake kuhangaika weeh! Polisi wakamuambia wanafuatilia. Ikaja kubainika kawekwa kinyumba na Mjeda mmoja mtaa wa Saba Huko.
Binti kadinda ATI mjeda(Mchumba wake) asichukuliwe hatua yoyote ya kisheria na kinidhamu. Vinginevyo atajidhuru. Kwa Akili za Yule Binti(kwani pia ninamjua) kila MTU alikuwa anaelewa nini angekifanya. Wakaachwa.
Binti alirudi baadaye akaenda kufanya paper (alikuwa akisoma hizi shule za kayumba). Akamaliza shule.
 
Number 9. Kwa mtanzania Hijab ni vazi la heshima.Kama kwa Marehem Mrema aliva baraghashia na muda mwengine alivaa kanzu,hii si ajabu...
Huyu bint kalamba utamu na ulimkolea,majuto ya anayo yafanya atalia baadae.
 
Hatimaye Ester Noah Mwanyiru mwanafunzi wa sekondari ya Pandahill aliyetoweka 18 May 2023 amepatikana.

Taarifa iliyotolewa na mama yake mzazi inaeleza amepatikana wilayani Mbalizi kwa mama fundi cherehani. Alibadili jina kuwa Erica na amekua akivaa Hijab inayofunika uso, na kuacha macho tu na hivyo kuwa ngumu kutambulika.

Chanzo cha kupatikana ni baada ya binti mmoja wa Mbalizi kusimuliwa kisa cha Ester na kudai amemuona kwa mama mmoja fundi cherehani. Leo asubuhi polisi wamevamia nyumba ya mama huyo na kumkuta Ester. Wote wawili wapo kituo cha Polisi Mbalizi kutoa maelezo.

#MyTake:
Simulizi ya kupotea kwa Ester na kupatikana kwake inaacha maswali mengi kuliko majibu.

1. Ester alitoroka shuleni baada ya kukutwa akifanya udanganyifu kwenye mtihani. Akachapwa viboko vitatu, kisha akapewa mtihani mwingine afanye. Lakini polisi walipoenda shuleni hakukua na mtihani wowote Ester aliofanya. Je mitihani yake ilienda wapi?

2. Shule ya Pandahill ina ukuta (fence) ya urefu wamita 3 na juu kuna nyaya za umeme. Inawezekanaje mtoto wa kike kuruka ukuta wa mita 3 wenye umeme?

3. Matron wa shule anasema Ester alitoroka na mwenzie mmoja na walikimbizwa hawakupatikana. Hata hivyo "rall call" ilipofanyika wanafunzi wote walikuwepo isipokua Ester tu. Je huyo aliyekimbia na Ester akiwa kwenye sare za shule ni nani?

4. Barua aliyoacha Ester alidai kuonewa na Mwalimu Jimmy, japo hakutaja uonevu huo. Kwanini hakwenda nyumbani kuwaeleza wazazi badala ya kukimbilia Mbalizi?

5. Kwanini Headmaster alienda kwa wazazi wa Ester kutoa pole?

6. Huyo mama wa Mbalizi aliwezaje kumpokea binti asiyemfahamu na kukaa nae comfortably?

7. Aliishi kwa huyo mama kama nani? Housegirl au?

8. Inaelezwa alienda kwa huyo mama na Hijab. Aliipata wapi? Sare za shule alizototoka nazo aliziacha wapi?

9. Alibadili jina kuwa Erica lakini akavaa Hijab. Huyo mama hakujiuliza iweje mtoto wa Kikristo kuvaa Hijab?

10. Binti aliyetoa taarifa kuwa amemuona Ester Mbalizi alimtambuaje ikiwa alivaa Hijab ya kufunika uso na kubakiza macho tu?

NB: Tunamshukuru Mungu Ester amepatikana akiwa mzima, lakini kwa kuwa suala hili limepaziwa sauti na umma, basi ni vema umma ukapewa majibu ya kuridhisha.!

Jambo la msingi, amepatikana. Hayo mengine ni ya Polisi, Shule na familia. Wengine kuyajadili ni umbea tu unaosumbua
 
Na usije shangaa kibwana chake kimo humu kilikuwa kinasubiri akiondoka kianzishe uzi kuwa kimekula mbususu week nzima bure tu. Kilikuwa kinasoma threads za humu kinacheka kina mpinda dogo kumchapa nao.... Huku wakitucheka.... Mafalah sana hawa.
 
mazuzu utayajua tu, eti umewaza mbali, jambo serious la kitaifa mtu antoa ushuzi wa kipumbavu bado anatokea zuzu anamsifu rti umewaza mbali. Nasikitika nchi hii ina watu wamedumaa akili. Watu km nyie mtaweza kuelewa kitu gani achilia mbali habari za DP World
Mind your own businesses,,, utuache na uzuzu wetu 🙃🙃🙃
 
Kulea mtoto wa kike kazi sana 🤣🤣🤣. Panda Hill wanajitahidi sana kudhibiti nidhamu ya watoto, hata watoto watukutu ambao wakiwa shule za serikali wanapata zero pale wanafaulu.

Lakini Esther ameweza kuwapiga chenga shule nzima kwa kutumia mbinu za medani na ujanja wa porini.
 
#UPDATES Mwanafunzi Ester Noah Mwanyilu, amepatikana katika chumba cha kupanga cha Mama Abdul kilichopo maeneo ya Ifisi Mbalizi, na kwamba alipelekwa hapo na muuza mkaa aitwaye Baba Jose na kusema ni mke wake hivyo anaomba hifadhi baada ya siku mbili angemchukua ili wakaishi wote.

Aidha vipimo vyote vya kiafya vimefanyika na Ester hana ujauzito na hivyo ataendelea kukaa na maafisa ustawi wa jamii ili kumsaidia kumpa ushauri wa kisaikolojia arudi shule, na mwanaume huyo atasakwa mpaka akamatwe.

RC Homera ametoa rai kwa walimu wa Pandahill kupunguza kasi ya kuchapa viboko.

#MwanafunziApatikana
#EastAfricaTV
 

Attachments

  • 1687531935535.png
    1687531935535.png
    144.3 KB · Views: 7
Back
Top Bottom