Rashidi Jololo
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 1,704
- 2,858
Unajuaje kama huyu sio Malisa mwenyewe mumbwa wewe? Unamfahamu kila mtu hapa JF? Acha ujuajiMleta uzi unajua ku copy hadi nukta.
Cc credit to Malisa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unajuaje kama huyu sio Malisa mwenyewe mumbwa wewe? Unamfahamu kila mtu hapa JF? Acha ujuajiMleta uzi unajua ku copy hadi nukta.
Cc credit to Malisa
Sio kama yenu ostadhi ya kuonyesha macho tuHapo namba 9 mbona masista wanavaa hijabu?
Apimwe na UkimwiHatimaye Ester Noah Mwanyiru mwanafunzi wa sekondari ya Pandahill aliyetoweka 18 May 2023 amepatikana.
Taarifa iliyotolewa na mama yake mzazi inaeleza amepatikana wilayani Mbalizi kwa mama fundi cherehani. Alibadili jina kuwa Erica na amekua akivaa Hijab inayofunika uso, na kuacha macho tu na hivyo kuwa ngumu kutambulika.
Chanzo cha kupatikana ni baada ya binti mmoja wa Mbalizi kusimuliwa kisa cha Ester na kudai amemuona kwa mama mmoja fundi cherehani. Leo asubuhi polisi wamevamia nyumba ya mama huyo na kumkuta Ester. Wote wawili wapo kituo cha Polisi Mbalizi kutoa maelezo.
-----
ALIJITAMBULISHA KAMA ERICA KUTOKA MKOANI MOROGORO
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema Mwanafunzi Esther Noah, aliyepotea tarehe 17 Mei 2023 (Siku 37) katika Sekondari ya Panda Hill, Mbeya amekutwa katika maeneo ya Ifisi, Mbeya alikuwa kwa mtu aliyefahamika kwa jina Moja la Baba Jose.
Mtu huyo baada ya kukaa na Mwanafunzi huyo kwa muda alikwenda kumuweka kwa mama mmoja na kuahidi kwenda kumchukua siku atakayopata chumba ili wakaendelee kuishi pamoja. Mama huyo alipobanwa na Jeshi la Polisi alisema kuwa Mwanafunzi huyo aliletwa na Baba Jose ambaye huwa anamletea magunia ya mkaa kuuzwa pale gengeni kwake takriban wiki mbili zilizopita, na alimwambia yule ni mke wake na ametoka naye Morogoro, hivyo anaomba amuhifadhi hapo mpaka atakapopata chumba cha kupanga ili aje amchukue mkewe. Mwanamke huyo alichukua jukumu la kumhoji mwanafunzi huyo, na aliambiwa kuwa anaitwa Erica na ametoka mkoani Morogoro.
BABA JOSE ANASAKWA NA JESHI LA POLISI
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema jeshi la Polisi liko makini na litahakikisha linamkamata baba Jose anayedaiwa kumtorosha Mwanafunzi Esther Noah, Sekondari ya Panda Hill, Mbeya aliyepotea tarehe 17 Mei 2023 (Siku 37) na kumfikisha kwenye mikono ya sheria.
APIMWA MIMBA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema wamempima Esther Noah kipimo cha mimba Ili kujua hali yake na majibu yameonesha hana mimba.
Na kwa siku zijazo ikionyesha ana mimba watampa nafasi ya kwenda kujifungua na kurudi shule.
View attachment 2666551
Mwanafunzi Esther akiwa na Mama yake Mzazi
------
#MyTake:
Simulizi ya kupotea kwa Ester na kupatikana kwake inaacha maswali mengi kuliko majibu.
1. Ester alitoroka shuleni baada ya kukutwa akifanya udanganyifu kwenye mtihani. Akachapwa viboko vitatu, kisha akapewa mtihani mwingine afanye. Lakini polisi walipoenda shuleni hakukua na mtihani wowote Ester aliofanya. Je mitihani yake ilienda wapi?
2. Shule ya Pandahill ina ukuta (fence) ya urefu wamita 3 na juu kuna nyaya za umeme. Inawezekanaje mtoto wa kike kuruka ukuta wa mita 3 wenye umeme?
3. Matron wa shule anasema Ester alitoroka na mwenzie mmoja na walikimbizwa hawakupatikana. Hata hivyo "rall call" ilipofanyika wanafunzi wote walikuwepo isipokua Ester tu. Je huyo aliyekimbia na Ester akiwa kwenye sare za shule ni nani?
4. Barua aliyoacha Ester alidai kuonewa na Mwalimu Jimmy, japo hakutaja uonevu huo. Kwanini hakwenda nyumbani kuwaeleza wazazi badala ya kukimbilia Mbalizi?
5. Kwanini Headmaster alienda kwa wazazi wa Ester kutoa pole?
6. Huyo mama wa Mbalizi aliwezaje kumpokea binti asiyemfahamu na kukaa nae comfortably?
7. Aliishi kwa huyo mama kama nani? Housegirl au?
8. Inaelezwa alienda kwa huyo mama na Hijab. Aliipata wapi? Sare za shule alizototoka nazo aliziacha wapi?
9. Alibadili jina kuwa Erica lakini akavaa Hijab. Huyo mama hakujiuliza iweje mtoto wa Kikristo kuvaa Hijab?
10. Binti aliyetoa taarifa kuwa amemuona Ester Mbalizi alimtambuaje ikiwa alivaa Hijab ya kufunika uso na kubakiza macho tu?
NB: Tunamshukuru Mungu Ester amepatikana akiwa mzima, lakini kwa kuwa suala hili limepaziwa sauti na umma, basi ni vema umma ukapewa majibu ya kuridhisha.!
Pia soma: DOKEZO - Ester Noah Mwanyilu, Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Pandahill Mbeya amepotea
Duuuh usikute kakosa mimba Ila ukimwi tayariApimwe na Ukimwi
Naunga mkono na Apewe ajira Usalama Wa taifa..... Bado suala la Bandari nakumbukaHuyo Binti aliyemgundua apewe milion 5 zake.
Malisa hatumiagi id fake popoteUnajuaje kama huyu sio Malisa mwenyewe mumbwa wewe? Unamfahamu kila mtu hapa JF? Acha ujuaji
Hata mimi nafikiria hivyo..Eeh alikua anaandaliwa kwenda kujitoa mhanga huko mashariki ya kati nini maana harakati zimepamba moto... soon na bongo wataanza kujilipua ili kuunga mkono DP World!
Ndio njia yao ya kupata kiki...Hii nchi viongozi na watu wake wanapenda kuhangaika na vitu vidogo vidogo sana! Eti mpaka waziri???
Hujasahau tu bandari mkuu?!Naunga mkono na Apewe ajira Usalama Wa taifa..... Bado suala la Bandari nakumbuka
Yani kalambwaa mpaka taifa zima linajuaaa..Amepatikana kimasihara
Bado sarakasi za kunisahaulisha azijapatikana.... Madktal wa Sudan Nimetoka kapa.... Na hili pia waruke zingine nizioneHujasahau tu bandari mkuu?!
Sheria gani?Binti kafuata dudu huyo anamsingizia mwalimuMungu mkubwa bint amepatikana!, uchunguzi wa kina ufanyike, siku hizi kuna walimu na vijana wapuuzi sana...sheria ifuate mkondo.
Tulia hapo hapo, kuna kitu kiko jikoni kinakaribia kuiva..Bado sarakasi za kunisahaulisha azijapatikana.... Madktal wa Sudan Nimetoka kapa.... Na hili pia waruke zingine nizione
Niko nasubiri mzee Hila sidhan kama nitasahauTulia hapo hapo, kuna kitu kiko jikoni kinakaribia kuiva..
Lazima utasahau tu utake usitake
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Nchi buana, viongozi sometimes wanatuonaga kama mazuzu fulani hivi
Mtoto wa kike unapataje ujasiri wa kutoroka kwenu kwenda kwa mwanaume???Kwanini unasema malezi mkuu?