Mwanafunzi Esther wa Panda Hill aliyepotea kwa siku 35 amepatikana, yadaiwa alitoroshwa na mchoma mkaa

Mwanafunzi Esther wa Panda Hill aliyepotea kwa siku 35 amepatikana, yadaiwa alitoroshwa na mchoma mkaa

Hawa madogo wameanza kuijua mboro mapema sana aisee.
Watoto wa kike ni hatari kinoma, kuna dogo alikua vizuri sana primary. Alipofika form three wakaanza kumzagamua basi akabadirika kila kitu.

MImi nalia na mavazi, hawa madogo wanavaa hovyo sana aisee.
Wazazi sijui umagharibi umewajaa, madogo wanaruhusiwa kuvaa wanavyotaka aisee.
Wanatongozwa na vijana si kwakua vijana wana tamaa sana ila wanashawishiwa na mavazi wanayovaa hawa watoto.
 
Huu umeme wa Makamba hizo electric fence ni mapambo tu.

Sijaona umri wa binti ukitajwa,au ni wale wamama waliorudi shule kwa hisani ya watu wa Marekani.
 
Hatimaye Ester Noah Mwanyiru mwanafunzi wa sekondari ya Pandahill aliyetoweka 18 May 2023 amepatikana.

Taarifa iliyotolewa na mama yake mzazi inaeleza amepatikana wilayani Mbalizi kwa mama fundi cherehani. Alibadili jina kuwa Erica na amekua akivaa Hijab inayofunika uso, na kuacha macho tu na hivyo kuwa ngumu kutambulika.

Chanzo cha kupatikana ni baada ya binti mmoja wa Mbalizi kusimuliwa kisa cha Ester na kudai amemuona kwa mama mmoja fundi cherehani. Leo asubuhi polisi wamevamia nyumba ya mama huyo na kumkuta Ester. Wote wawili wapo kituo cha Polisi Mbalizi kutoa maelezo.

-----


ALIJITAMBULISHA KAMA ERICA KUTOKA MKOANI MOROGORO

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema Mwanafunzi Esther Noah, aliyepotea tarehe 17 Mei 2023 (Siku 37) katika Sekondari ya Panda Hill, Mbeya amekutwa katika maeneo ya Ifisi, Mbeya alikuwa kwa mtu aliyefahamika kwa jina Moja la Baba Jose.

Mtu huyo baada ya kukaa na Mwanafunzi huyo kwa muda alikwenda kumuweka kwa mama mmoja na kuahidi kwenda kumchukua siku atakayopata chumba ili wakaendelee kuishi pamoja. Mama huyo alipobanwa na Jeshi la Polisi alisema kuwa Mwanafunzi huyo aliletwa na Baba Jose ambaye huwa anamletea magunia ya mkaa kuuzwa pale gengeni kwake takriban wiki mbili zilizopita, na alimwambia yule ni mke wake na ametoka naye Morogoro, hivyo anaomba amuhifadhi hapo mpaka atakapopata chumba cha kupanga ili aje amchukue mkewe. Mwanamke huyo alichukua jukumu la kumhoji mwanafunzi huyo, na aliambiwa kuwa anaitwa Erica na ametoka mkoani Morogoro.

BABA JOSE ANASAKWA NA JESHI LA POLISI
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema jeshi la Polisi liko makini na litahakikisha linamkamata baba Jose anayedaiwa kumtorosha Mwanafunzi Esther Noah, Sekondari ya Panda Hill, Mbeya aliyepotea tarehe 17 Mei 2023 (Siku 37) na kumfikisha kwenye mikono ya sheria.

APIMWA MIMBA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema wamempima Esther Noah kipimo cha mimba Ili kujua hali yake na majibu yameonesha hana mimba.

Na kwa siku zijazo ikionyesha ana mimba watampa nafasi ya kwenda kujifungua na kurudi shule.


View attachment 2666551
Mwanafunzi Esther akiwa na Mama yake Mzazi


------


#MyTake:
Simulizi ya kupotea kwa Ester na kupatikana kwake inaacha maswali mengi kuliko majibu.

1. Ester alitoroka shuleni baada ya kukutwa akifanya udanganyifu kwenye mtihani. Akachapwa viboko vitatu, kisha akapewa mtihani mwingine afanye. Lakini polisi walipoenda shuleni hakukua na mtihani wowote Ester aliofanya. Je mitihani yake ilienda wapi?

2. Shule ya Pandahill ina ukuta (fence) ya urefu wamita 3 na juu kuna nyaya za umeme. Inawezekanaje mtoto wa kike kuruka ukuta wa mita 3 wenye umeme?

3. Matron wa shule anasema Ester alitoroka na mwenzie mmoja na walikimbizwa hawakupatikana. Hata hivyo "rall call" ilipofanyika wanafunzi wote walikuwepo isipokua Ester tu. Je huyo aliyekimbia na Ester akiwa kwenye sare za shule ni nani?

4. Barua aliyoacha Ester alidai kuonewa na Mwalimu Jimmy, japo hakutaja uonevu huo. Kwanini hakwenda nyumbani kuwaeleza wazazi badala ya kukimbilia Mbalizi?

5. Kwanini Headmaster alienda kwa wazazi wa Ester kutoa pole?

6. Huyo mama wa Mbalizi aliwezaje kumpokea binti asiyemfahamu na kukaa nae comfortably?

7. Aliishi kwa huyo mama kama nani? Housegirl au?

8. Inaelezwa alienda kwa huyo mama na Hijab. Aliipata wapi? Sare za shule alizototoka nazo aliziacha wapi?

9. Alibadili jina kuwa Erica lakini akavaa Hijab. Huyo mama hakujiuliza iweje mtoto wa Kikristo kuvaa Hijab?

10. Binti aliyetoa taarifa kuwa amemuona Ester Mbalizi alimtambuaje ikiwa alivaa Hijab ya kufunika uso na kubakiza macho tu?

NB: Tunamshukuru Mungu Ester amepatikana akiwa mzima, lakini kwa kuwa suala hili limepaziwa sauti na umma, basi ni vema umma ukapewa majibu ya kuridhisha.!

Pia soma: DOKEZO - Ester Noah Mwanyilu, Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Pandahill Mbeya amepotea
Apimwe na Ukimwi
 
Eeh alikua anaandaliwa kwenda kujitoa mhanga huko mashariki ya kati nini maana harakati zimepamba moto... soon na bongo wataanza kujilipua ili kuunga mkono DP World!
Hata mimi nafikiria hivyo..
Ngoja tuwasubiri wajitoaji mhanga wengine!
Maana nchi yetu kwa "kiki" haijambo..
Anyway, let's give it time.
 
Bado sarakasi za kunisahaulisha azijapatikana.... Madktal wa Sudan Nimetoka kapa.... Na hili pia waruke zingine nizione
Tulia hapo hapo, kuna kitu kiko jikoni kinakaribia kuiva..
Lazima utasahau tu utake usitake
😁😁😁😁😁😁
Nchi hii buana, viongozi sometimes wanatuonaga kama mazuzu fulani hivi
 
Tulia hapo hapo, kuna kitu kiko jikoni kinakaribia kuiva..
Lazima utasahau tu utake usitake
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Nchi buana, viongozi sometimes wanatuonaga kama mazuzu fulani hivi
Niko nasubiri mzee Hila sidhan kama nitasahau
 
Way back 2003/4
Kuna familia ulizuka utata mzito sana kama wa Esther lakini kumbe Esther yule alikuwa pahala akihesabu vinywele vya mjuba flani hivi kifuani siku 3 mara 4 mara week.
Afande mmoja kijana mwerevu ni baharia kama mabaharia akakalisha zile familia na kuwapa jambo kuwa yaaishe.

Esther yule alipopatikana akasema anataka kuolewa asilazimishwe.
 
Back
Top Bottom