Japo tulikuwa chama kimoja na wapalestina wakati tunapigania Afrika kusini iwe huru. Lakini Afrika yote ilipokuwa huru, tukawatosa Wapalestina. Nyerere alipokufa ndio kabisa. Hivyo ndivyo waafrika walivyo!
Ni wepesi sana kusahau matatizo waliyoyapata. Pengine hii ndio dhambi yetu kubwa, inayotufanya tusitoboe.
Tusitafute mchawi, na ndio maana hata tukienda Afrika kusini wanatukataa maana hawatuelewi. Wakati wao wapo mstari wa mbele kusimama na wapalestina, serikali yetu inashindwa hata kutoa tamko au hata kumuunga Raisi wa Afrika kusini kwa kutaka Nitanyau ashitakiwe.
Na tumesahau kabisa kuwa tuliwasaidia akina Mandela kijeshi na kutumia mbinu hizo hizo ambazo HAMAS wanatumia leo kujikomboa. Du, hivi ndivyo miafrika ilivyo!
R.I.P Clemens Mtenga.
Zawadi Ngota:
Mkuu umezungumza ukweli nusu (Half truth), Sio Ukweli wote. Ni ukweli kabisa enzi za kupigania uhuru kulikuwa na support kubwa dhidi ya Palestine kutoka nchi za Kiafrika, kwanza karibu wote tulikuwa na agenda moja kubwa kupata uhuru kutoka kwa waliotutawala (Wakoloni) Na enzi hizo karibu nchi nyingi zilipata support kutoka nchi za Mashariki, USSR na satellite zake, na Chama cha PLO 1969 kiliweka wazi msimamo wako katika Charter yake kuwa kinafuata siasa za Marxist/Leninism, hii ilitosha kuwa na ukaribu na nchi nyingi mno za Kiafrika na kina Nyerere. In short wakati huo adui yetu alikuwa mmoja....Mkoloni au Beberu.
Lakini baada ya kupata uhuru toka kwa mabeberu agenda za nchi za Kiafrika ilibadilika mno, ikawa ni kuleta maendeleo kwa na Mababeru wakawa ni wadau wa Maendeleo, na nchi nyingi za Kiafrika zikawa zinategemea mno katika kujikwamua kiuchumi kutoka Magharibi, na Nchi za Mashariki hasa USSR na kuanguka kwake akawa sio msaada mkubwa tena, hivyo ukaribu na Harakati juu ya Wapelestine ikapungua mno.
Lakini pia harakati za Wapalestine zimebadilika na agenda yao imekuwa ikibadilika, kunya nyakati wanatambua kuweko kwa taifa la Israel, kama lilivyotambuliwa na UN kwenye resolution 181 ya 1947, na kuna baadhi ya Wapalestine hawatambua kabisa kuwepo kwa taifa hilo hapo! Waarabu wenyewe wamegawanyika mno! Na kuweka wanatoa support kuwa njia panda!
Na ujio wa Hamas umebadilisha kabisa mambo! Itikadi ya Hamas ni ya kidini, Kuutumia Uislamu ! iko wazi kwenye Charter yao ya 1987, akina Ahmed Yassin walichukua itikadi ya Moslem Brotherhood, ambayo hata baadhi ya hata nchi za Waislamu kama EGYPTY, hawaikubali na kuifanya nguzo kuu katika mapambano yao na Israel, hivyo nchi nyingi kuikubali Hamas ni kama umekubali itikadi ya Siasa kali....Hii imeifanya support ya Palestine kutokuwa na nguvu, mfano nchi kama Nigeria, kuikubali Hamas ni kama kuihalalisha Boko Haram. Msimamo wa Hamas umeingiza agenda mpya katika mapambano hao.
Na sababu nyingine kubwa ni kukua kwa uchumi wa Israel na misaada yake kwa nchi za Kiafrika! Ile Israel ya 1948 sio hii ya leo, licha ya kutokuwa na mafuta, uchumi wao na msaada wao kwa nchi za Kiafrika umeongezeka sana! Nani alijua nchi kama Tanzania tuna vijana kama 260 wanachukua kozi mbali mbali Israel, na nafahamu vijana wengi wa TISS wamesomea Israel.....Ndio maana support ya Palestine sio kubwa, Nchi kama South Africa na chama kama ANC, hawajali mno misaada ya kiuchumi, ndio maana wana ujasiri wa kuvunja uhusioano na Israel! Baadhi ya nchi haziwezi kufanya hivyo.
Hivyo mkuu nchi nyingi zinaangalia maslahi yake kwanza....Unagopa uikiunga mkono waziwazi nini utapoteza.