Mwanafunzi SAUT auawa kizembe

Mwanafunzi SAUT auawa kizembe

1456528769170.jpg
Ukweli ni kwamba huyo jamaa na huyo demu ni wapenzi wa mda mrefu.,,na pia jamaa sio mwanafunzi ni raia wa kawaida anayehusika na mambo hasa ya modeling na amekuwa akiandaa event mbalimbali kama mtakuwa na kumbukumbu vizuri kuna kipindi kulitokeaga shindano la MISS ALBINISM lililofanyika Mwanza huyu jamaa alikuwa miongoni mwa wahusika wa hilo shindano,na siku tatu zilizopita huyu jamaa alitoka kumzika baba yake mzazi.

Kilichotokea hapo ni baada ya jamaa kwenda hostel za wanawake ambazo zipo ndani ya chuo ambapo ndipo alipokuwa akiishi huyo demu wake, katika kukagua simu ndipo akakuta sms za utata,ukatokea ugomvi katika mabishano demu akasema atamwita mwizi kama utani kweli demu akaita mwizi.

Jamaa kwa kuogopa na sababu hakuwa na kitambulisho ndipo akatoka mbio,hapo ndipo alipoharibu wananzengo na wanachuo bila kujali wakaanza kupiga na mpaka wanafika polisi alikuwa kapigwa sana,alipelekwa kituoni kutoa maelezo.Baada ya hapo ndipo tukapata taarifa kafariki na hiyo ni sababu ya kipigo.

Kinachofanywa na uongozi wa chuo ni kutaka kuonesha huyo binti hana makosa ili kuondoa uhasama na wananzengo ila ukweli utabaki kuwa huyo jamaa na mwanamke walikuwa wapenzi.
 
Japokua ni unyama uyo binti alichofanya lakini ni funzo kwa wengine.!
Unaanzaje kubeba simu ya mwenzako et kisa umekuta sms???
Ukishachukua simu itakusaidia nini haswaaaaa.....hapo ukute hakuna hata senti yako iliyotumika kwenye ununuzi wa simu
 
IMG-20160227-WA0002%255B1%255D.jpg

Habari yenu,
kwa masikitiko makubwa tukio tajwa hapo chini limetokea Chuo cha SAUT mwanza ambapo mwanafunzi wa jinsia ya kiume ,alienda kumtembelea mpenzi wake chuoni SAUT bweni la RUGAMBWA,baada ya kufika katika kuangalia simu ya mpenzi wake alikuta sms ya mwanaume mwingine ambapo,alichukia na kuamua kuondoka na simu ya mpenzi wake.
Alichokifanya binti huyo aliita MWIZI ,watu walikuja na kupiga bila kuuliza,TAZAMA VIDEO HAPO CHINI.



Read More >>>>>kuona video
wewe unapewa mkopo na serikali ukasome halafu wewe husomi kazi yako ni kutembelea tu mabweni ya wasichana.na utakufa sana tu ukiendelea na tabia hiyo
 
Mmmmh hii ni hatari. Hapa ndipo unapoonekana ubaya wa kujichukulia sheria mikononi. Huyo mdada analaana siyo bure.
 
huyu marehemu aliwah kunusurika kifo huko huko rugambwa hostel mwaka 2011,alijifanya mwanafunzi na kuzoeana sana na wasichana.aliiba laptop na kukimbilia kwao pale nyamalango,nzengo ilimtetea sana.huwez kuamini kwa maramoja tu katika mia mmoja aseme huyu ni mwizi,ila polisi wana taarifa zake nying za wizi.
wakati ameitiwa mwizi na kuanza kukimbia,alikuwa na kisu na kuwatishia mabinti waliokuwa wanamkimbiza.
 
Huyu Jamaa ni Fala na amekufa kizembe...


Alikuwa anataka kuondoka na simu ya huyo demu ili iweje???... Demu mwenyewe labda wamekuta kichuo chuo anataka kumdhibiti kama mke wa ndoa!.


Huu ni upumbavu!.....


.
!
 
Huyu Jamaa ni Fala na amekufa kizembe...


Alikuwa anataka kuondoka na simu ya huyo demu ili iweje???... Demu mwenyewe labda wamekuta kichuo chuo anataka kumdhibiti kama mke wa ndoa!.


Huu ni upumbavu!.....


.
!
tah teh! mapenzi ya run dunia mapenzi yana nguvu ya kunyanyua Mlima Kilimanjaro !! Mapenzi yanaumaa
 
Nzi kufa kwenye kidonda sio ufala ila kupenda... Kumbukumbu yake imebaki kaburini... Naijua vizuri sana SAUT hizi mambo zipo sana.. Tatizo la hawa dada zetu hawana mmoja! Wana tamaa sana... Lakini na sisi jamani hata kama ni kupenda sio kama huyu jamaa.. Dunia imebadilika.. Ukimchunguza bata humli..
 
Wizi ni kitendo cha kuchukua,ku nakili,kuhamisha kitu cha mtu bila ya idhini yake. Kupiga na hatimae kuua mtu aliekuwa kwny jaribio la wizi ni makosa KISHERIA.
 
Japokua ni unyama uyo binti alichofanya lakini ni funzo kwa wengine.!
Unaanzaje kubeba simu ya mwenzako et kisa umekuta sms???
Ukishachukua simu itakusaidia nini haswaaaaa.....hapo ukute hakuna hata senti yako iliyotumika kwenye ununuzi wa simu

nasikitika kusema kwamba hata wewe pia una genes za uuaji
 
Wanawake wengine ni wauaji kweli nimeshuhudia matukio km hayo ya wasichana kuwaitia wapenzi wao wezi na wakauwawa kisa wamefumaniwa na vidume vingine
 
Back
Top Bottom