Mwanafunzi UDOM ajirusha toka ghorofani akidai kufelishwa mitihani

Mwanafunzi UDOM ajirusha toka ghorofani akidai kufelishwa mitihani

Nadhani muda huu amesha tambua kuwa afya ni Bora kuliko hayo matokeo ya kwenye makaratasi. Amevunja spinal cord nani atakuwa anamzolea kinyesi.

Vijana tujifunze kuwa na roho ngumu na tujue kukabiliana na changamoto zozote tunazokutana nazo bila kujiingiza kwenye vitu vitakavyo tuletea matatizo
 
Inasikitisha sana.

---
Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wa Shule ya Uuguzi na Afya ya umma (SoNPH) Ezekiel Sostenes amelazwa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya kati Benjamin Mkapa baada ya kujirusha ghorofani.

Awali kabla ya tukio hilo jana, kulikuwa na ujumbe wa WhatsApp ambao Mwananchi imeuona, uliosambaa mitandaoni ukionyesha majibizano kati ya mwanafunzi huyo akimlalamikia mkufunzi wake kuwa alimfelisha kwa makusudi.

Akizungumza na Mwananchi leo Desemba 15, 2022 Dk Winnie Msangi kutoka hospitalini hapo amesema walimpokea mwanafunzi huyo jana akiwa kwenye hali mbaya.

Winnie amesema Ezekiel anaendelea na matibabu baada ya kupata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.

"Tulimpokea jana na kufanyiwa huduma ya kwanza kwa sababu alikuwa kwenye hali mbaya ya maumivu, mpaka sasa majeraha makubwa tuliyoyabaini ni kwenye uti wa mgongo lakini anaendelea ja matibabu zaidi," amesema Daktari huyo.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo Ofisa habari wa Chuo cha UDOM, Beatrice Mtenga amedai kuwa hana taarifa za tukio hilo na kuomba kupewa muda wa kulifuatilia.


Chanzo: Mwananchi
Hasira hasara,
 
Sijafanikiwa kufika chuo, bado najikongoja kwa kujiendeleza huku nikisaka ela ya tonge.

Kwa msoto huu siku nikifanikiwa kufika huko hao mnaowaita wakufunzi kama ndio tabia zao hizi watajuta kunijua.

Huku kwetu Mtu kuchezea elimu unayoisotea kwa nguvu na jasho anastahili kabisa kucharangwa mapanga ili iwe fundisho kwa wengine
 
Ila walimu wa vyuo nao wanaushamba mwingi sana aisee
Jinga wewe kwahiyo umemuamini huyo dogo? Hivi nyie mkoje? Wanafunzi wakifaulu sana mnawapigia kelele walimu ati wanagawa maksi za bure. Wakisimamia principles madogo wazembe wakafeli, mnakuja mbio kuwalaumu. Kifupi hamjui mtakalo. Aliyekwambia kuwa ukishasajiliwa chuoni hakuna Kufeli ni nani?
 
Siyo pimbi sometimes limeuzwa shamba la familia ili aokoe ukoo na ukute alikuwa anagombania mwanamke na lecture akaambiwa live wewe hapa hutoboi na kafail kweli.

Inatafakarisha.
Vijana someni. Achaneni na vi excuses msivyoweza kuvithibitisha.
 
Sijafanikiwa kufika chuo, bado najikongoja kwa kujiendeleza huku nikisaka ela ya tonge.

Kwa msoto huu siku nikifanikiwa kufika huko hao mnaowaita wakufunzi kama ndio tabia zao hizi watajuta kunijua.

Huku kwetu Mtu kuchezea elimu unayoisotea kwa nguvu na jasho anastahili kabisa kucharangwa mapanga ili iwe fundisho kwa wengine
Aliyekuambia kwamba kufaulu ni lazima ni nani? Wewe uende chuoni, halafu ukalie kubet na kubishania Simba na Yanga halafu ufaulu katika vyuo serious? Sahau.
 
India lecturer mmoja unakuta kwa mwaka ana vichwa viwili vimeaga dunia kwa kujitupa relini na kugongwa na treni baada ya kufeli kwenye mtiani wa mwisho.

Huyo lecturer ahamie India.
 
Back
Top Bottom