Mwanafunzi UDOM ajirusha toka ghorofani akidai kufelishwa mitihani

Nadhani muda huu amesha tambua kuwa afya ni Bora kuliko hayo matokeo ya kwenye makaratasi. Amevunja spinal cord nani atakuwa anamzolea kinyesi.

Vijana tujifunze kuwa na roho ngumu na tujue kukabiliana na changamoto zozote tunazokutana nazo bila kujiingiza kwenye vitu vitakavyo tuletea matatizo
 
Hasira hasara,
 
Sijafanikiwa kufika chuo, bado najikongoja kwa kujiendeleza huku nikisaka ela ya tonge.

Kwa msoto huu siku nikifanikiwa kufika huko hao mnaowaita wakufunzi kama ndio tabia zao hizi watajuta kunijua.

Huku kwetu Mtu kuchezea elimu unayoisotea kwa nguvu na jasho anastahili kabisa kucharangwa mapanga ili iwe fundisho kwa wengine
 
Ila walimu wa vyuo nao wanaushamba mwingi sana aisee
Jinga wewe kwahiyo umemuamini huyo dogo? Hivi nyie mkoje? Wanafunzi wakifaulu sana mnawapigia kelele walimu ati wanagawa maksi za bure. Wakisimamia principles madogo wazembe wakafeli, mnakuja mbio kuwalaumu. Kifupi hamjui mtakalo. Aliyekwambia kuwa ukishasajiliwa chuoni hakuna Kufeli ni nani?
 
Siyo pimbi sometimes limeuzwa shamba la familia ili aokoe ukoo na ukute alikuwa anagombania mwanamke na lecture akaambiwa live wewe hapa hutoboi na kafail kweli.

Inatafakarisha.
Vijana someni. Achaneni na vi excuses msivyoweza kuvithibitisha.
 
Aliyekuambia kwamba kufaulu ni lazima ni nani? Wewe uende chuoni, halafu ukalie kubet na kubishania Simba na Yanga halafu ufaulu katika vyuo serious? Sahau.
 
India lecturer mmoja unakuta kwa mwaka ana vichwa viwili vimeaga dunia kwa kujitupa relini na kugongwa na treni baada ya kufeli kwenye mtiani wa mwisho.

Huyo lecturer ahamie India.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…