Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Mkuu ishu siyo picha ishu ni kwamba ni wwapo panazuia msafara wa rais kupigwa picha?

Mbona kina Putin huku tunawapiga picha hawajawahi kumkamata mtu?

Mambo mengine ni ujinga na ushamba
 
White house tu marekan watu wanajiself nje sembuse uku bara la giza uzwazwa tu na ushamba
 
Nakumbuka kuna mama mmoja alishuka kwenye kona ya kwenda ferry sababu alikuwa anaogopa purukushani za kituon asingeweza kushuka, akakutana na wale jamaa alitembezwa kibatabata. Hadi nilidhani wale wanajeshi ni robots yaani wamekuwa coded kwa brutal tu hawasikilizi mtu
 
Ikulu yetu nayo ipo karibu mno na shughuli za raia wa kawaida; pale hata ukiwa unapita upande wa ukuta wakati unakwenda ferry jamaa wanakudaka aisee utaruka kichura hadi utapike msosi wa jana yake usiku.
 
Watu wa aina yako ndio tatizo la nchi hii, yaani unaona uvunjifu wa haki za Mtanzania unaona ni sawa kabisa. Hata kama kafanya kosa apewe adhabu stahili, sio kurushwa kichura.
 
We hukuchukua hata kavideo ukaweke humu
 
2020 twende na Membe.
Mambo yote haya yatakwisha...

Itakuwa ni mwendo wa Kazi na Bata.
Full kupiga piga mapicha green house kuanzia getini pale mbele mpaka kule nyuma usawa wa beach kule....

Hivi wale wauza karanga kutokea feri wa enzi za JK badogo wanaendaga kuwaonjesha karanga wale walinzi wa green house kama zamani??

2020 Twende na Membe.
Tutarudi kuuza karanga zetu
Ni mwendo wa kazi na bata tu.
 
Siyo lazima awe mwanao. Binadamu yoyote kupigwa kwa jambo la kijinga kama hilo mtu yoyote mwenye ubinadamu lazima unaumia. Haipaswi binadamu tuishi kama wanyama. Kama wameona ana kosa kona hatua za kuchukua na siyo kumpiga. Kama walinzi wanaotakiwa kuwa na displine kama wa Ikulu wanafanya ushenzi wa aina hiyo mgambo wa vijijini watafanyaje?
 
Maeneo mengi ya Serikali Picha haziruhusiwi labda kwa kibali maalum sembuse Ikulu, kajitakia tu
 
Vyou vikuu vya wapi viandamane? Hapahapa bongo daslam? Thubutu
 
ndo tatizo ya watu wa mapicha picha unapiga unanyakuliwa unaumizwa inakuwa mfano na elimu kwa wengine sasa mimi hapo nishajifunza kuwa pale picha ni NO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…