Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni akalishwa chini licha ya kulipa nauli kamili

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni akalishwa chini licha ya kulipa nauli kamili

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414


Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, kupitia operesheni za ukaguzi wa vyombo vya
moto, limeendelea kuchukua hatua kuhakikisha usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara unazingatiwa.

Katika operesheni hiyo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Yusuph Kamotta, alifanikiwa kulisimamisha basi la kampuni ya Katarama Luxury lililokuwa limezidisha idadi ya abiria wanaoruhusiwa kusafiri. Miongoni mwa abiria waliokuwamo ndani va basi hilo ni mwanafunzİ anayetarajiwa kuanza mwaka wa kwanza chuoni, aliyekuwa akisafiri kutoka Bukoba kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza safari yake ya elimu ya juu.

Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alilipa nauli ya shilingi 110,000 kwa safari yake, lakini licha ya kulipa kiasi hicho, alilazimika kukaa chini katika sehemu ya basi hilo kuanzia Bukoba hadi alipofika Dodoma kutokana na kuzidi kwa idadi ya abiria. Hata hivyo, hali hiyo ilibainika wakati wa ukaguzi uliofanywa na Kamanda Kamotta, ambaye baada ya kubaini changamoto iliyomkabili mwanafunzi huyo, alimuagiza kondakta wa basi hilo kumrejeshea fedha zake ili aweze kutafuta usafiri mwingine na kuendelea na safari yake katika mazingira salama.

Hatua hiyo inalenga kusisitiza umuhimu wa wamiliki wa mabasi, madereva na makondakta kuzingatia sheria za usafirishaji, ikiwemo kubeba idadi ya abiria inayoruhusiwa na kuhakikisha kila abiria anapata nafasi inayostahili
kwa usalama wake
 
Kiongozi zingatia hapa Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza bado fresh from school hajachamka bado so nikawaida ukizingatia ninakotoka kule kwetu mabondeni.
Kama ni huko mabondeni ,sawa.Ila wengine ni watata tangu tukiwa darasa la kwanza.
 
Huyo mtoto alikua desperate sana kusafiri Hadi akakubali kukaa chini?
Labda mabus yalikuwa machache kakosa yote
 
Huyo dogo hajapita JKT atumie kidogo utayari na ukakamavu wake wahedi au mwaka wa kwanza DIRPOMAA😬
 
Back
Top Bottom