Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni akalishwa chini licha ya kulipa nauli kamili

Sawa mkuu nmekuelewa.

Sishangai ndo mana msanii akipata madhara akiwa na wenzake, huyo msanii pekee ndie atakayekuwa anazungumziwa na kujaliwa na sio wale wenzake wa kawaida.
 
Hizo luxury zimekaa kikuda ukienda chooni kila mtu anakukodolea macho luxury zipo Kilimanjaro express ila nauli yake 70k pia hata hao wakina Bm wana ma-ngarangara mara ya mwisho kupanda bm nilipanda la saa mbili asubuhi kutoka dsm nikafika Arusha saa 5 usiku.
 
Vijana wa siku hizi mmpoje?Mwaka 1940 enzi zangu sijui ingekuwaje!Ningekaa hata siti ya dereva halafu yeye asimame huku anaendesha hilo basi.
Kwenda huko,ukapandie Ndiuka upate siti!😁😁😁

Enzi zako mlikuwa mnajazwa kwenye Kwacha au Comfort ile ya carrier juu hadi mkawa mnaruhusiwa kuingia na mabegi ndani ili mkalie
 

Your browser is not able to display this video.

​

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, kupitia Kikosi cha Usalama barabarani imeendesha operesheni na ukaguzi wa vyombo vya moto na kuchukua hatua za kisheria kwa maafisa usafirishaji wanao kiuka Sheria za usalama barabarani ikiwemo kuzidisha abiria kinyume na taratibu katika vyombo vya moto.

Akiongoza Operesheni hiyo Oktoba 18, 2026 iliyoenda sambamba na utoaji wa elimu Kwa watumiaji wote wa barabara Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma (SSP) Yusufu Kamota, amesema zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kubaini makosa ya usalama barabarani ya kuzidisha abiria pamoja na ubovu wa vyombo vya moto.

Mbali na utoaji elimu baadhi ya mabasi yaliozidisha abiria na kukutwa na changamoto mbalimbali yamechukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuandikiwa faini Kwa mujibu wa Sheria pamoja na kurejesha nauli za abiria waliozidi katika vyombo hivyo.

Akizungumza Mmoja wa abiria aliezidishwa katika chombo cha usafiri mwanafunzi anaetarajia kujiunga na Chuo kikuu mwaka wa kwanza Jijini Dar es salaam akitokea Bukoba, ambaye ametozwa nauli ya shilingi laki Moja na elfu kumi 110,000/= bila kupewa siti amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kumsaidia kurejeshewa nauli yake na kupatiwa usafiri mwengine na kuendelea na safari.
 
Ila kuna kampuni za mabasi ni wahuni sana. Yaani mtu akose siti toka Bukoba hadi Dodoma. Siyo fair kabisa
 
Well done RTO Kamotta πŸ’ͺ
 
Sasa Dogo atakubali vipi kukaa chini, sema Malezi na mazingira Yake yamechangia. Mtu anayekwenda chuo sio mtoto so anatakiwa kuwa na reasoning kidogo Tu, bongo Hapa kama Adui unammudu usimuachie mungu coz utateseka na Sheria au mamlaka haiwezi kukusaidia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…