TANZIA Mwanafunzi wa UDSM (COET) agongwa na gari

TANZIA Mwanafunzi wa UDSM (COET) agongwa na gari

Hivi kuweka CCTV camera nako kunahitaji msaada wa watu wa "weupe"????? nchiza "wenzetu" huu dereva asingetembea hata km 1 zaidi bila kukamatwa, lakini "shamba" la bibi hili!so sad! BURIANI MWANAUDSM!
 
r.i.p kijana wetu

mtoa mada umefanya jambo jema kutoa funzo ya kwamba tuwe tunatembea na vitambulisho popote,nami naongezea funzo lingine,wakati wa kuvuka barabara kunapokuwa na magari machache ni hatari zaidi maana magari huenda kasi zaidi na inapokuwa ni usiku hali huwa mbaya zaidi,tuongeze tahadhari zaidi ktk mazingira hayo tajwa

lakini mwisho wa maelezo yako binafsi sijayapenda

kwanini umetengeneza "roho" ya kisasi???kusoma kwako hadi chuo kikuu kunakufanya uamini dereva anaweza kufanya makusudi kumgonga mtu???na hata wa gari la pili na la tatu unaona nao wamefanya makusudi kumgonga?
Je na wewe kusoma kwako mpaka sijui wapi,bado unaamini kumgonga na gari binadamu mwenzako na kukimbia sio makusudi?,na kunahitaji msamaha kwa namna yeyote ile?
 
Poleni kwa msiba mzito wana UDSM
Ila pia tukumbushane ajali nyingine zinatokea kwa sisi watembea kwa miguu kutokua makini,mtu yupo highway afu kaweka earphone mziki vol ya mwisho unapigiwa hon wala husikii,we unatembetea kwa kunata na biti mara gar hiloo vuuu ajali tayari!! Earphone siyo nzuri pindi utembeapo barabarani
 
Yani kila mwisho ya semister ya mwisho wa mwaka UDSM kifo hutokea kwa mwanafunzi kwa ajali sijui nini? Wote tunapita duniani si wakaaji R.I.P mwanafunzi
 
So sad, poleni sana na M/Mungu amlaze pema... Amin
 
Niliwahi kukuta ajali kama hii. Niliposimama kutoa msaada nilijuta maana nilitukanwa kwa niaba ya madereva wote. Na kibaya zaidi nilipofika hospitali polisi walinianzishia maelezo kama mimi ndio nimegonga. Kwa kifupi nilipata usumbufu sana. Ilikuwa nifike nyumbani saa 12 jioni nilifika saa 6 usiku na gari limetapakaa damu. Ni vizuri kutumia tuu magari ya polisi.

Kaisari usiogope changamoto
Siku nyingine watu watashindwa kukuokoa wewe au mkeo kwa kuogopa matusi au police interogation ama kuchafua nguo na magari ama damu(HIV)
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana,na pia nawapongeza kwa ubinadamu mliouonyesha hata
kabla ya kujua kuwa ni mwanachuo mwenzenu.
Pia naomba eneo hilo liangaliwe kwa kuwekewa alama
za barabarani kwani ni njia kuu ya waenda kwa miguu.
 
Niliwahi kukuta ajali kama hii. Niliposimama kutoa msaada nilijuta maana nilitukanwa kwa niaba ya madereva wote. Na kibaya zaidi nilipofika hospitali polisi walinianzishia maelezo kama mimi ndio nimegonga. Kwa kifupi nilipata usumbufu sana. Ilikuwa nifike nyumbani saa 12 jioni nilifika saa 6 usiku na gari limetapakaa damu. Ni vizuri kutumia tuu magari ya polisi.

jamii tunayoishi ndipo ilipofika ubinadamu hakuna kabisa....binafsi nimewahi kugonga watu wawili na kuua ....wa kwanza ni mtoto huyu alikuwa amewekwa na wenzake kwenye box kubwa halafu wenzake wanavuta barabarani gafla nami nikafika nikapiga honi wale watoto waliokuwa wanavuta box wakaliacha box barabarani kwa speed niliyokuwa kuwa nayo nkashindwa kulikwepa...nikakanyaga masikini yle mtoto akafa alikwa wa mwaka na miezi kadhaa...sikukimbia bali nilisimama na kubeba maiti na box lake na kwenda polis then hosp..kilichoniokoa ni kamera niliyofunga ndani ya gari ambayo hurekodi kila kitu barabarani ule ndo ulikuwa ushahidi wangu mbele ya polis na mahakama.....mwingine niligonga ni binti wa miaka 14 huyu alikuw anakimbizwa na baba yake...binti akaingi barabrani akitokea uchochoroni ..nikakutana nae..pale pale akafariki na ilikuwa niue na mzee bahati nzuri alisalimika...nayo hii sikukimbia...safari hii pia camera ilinisaidia kushinda kesi na majirani waliofika wakimlaum mzee yule kwa kumpiga binti na kumkimbiza nao wakati tuko eneo la tukio camera iliendelea kurekodi kila kitu...anayway kukimbia eneo la tukio inategemeana na mtu mwenyewe ila wengi hukimbia kwa hofu na mara nyingi unakuta makosa ni ya dreva lakini pia anaweza kukimba kwa kuogopa kupigwa na raia
 
Kaisari usiogope changamoto
Siku nyingine watu watashindwa kukuokoa wewe au mkeo kwa kuogopa matusi au police interogation ama kuchafua nguo na magari ama damu(HIV)

Ndugu kwangu damu sio shida. Maana niliwahi beba mjamzito akajifungulia kwenye gari hii imenitokea mara mbili. Nina amani maana nimetoa msaada. Kero ni pale unamfikisha majeruhi hospital halafu unageuzwa mtuhumiwa. Watu wanaanza kuuliza maswali ya ajabuajabu. Umemtoa wapi? Ilikuwajekuwaje. Nani. Mtu haongei wanakuuliza jina lake details zake.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom