Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
poleni sana wanaUDSM Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi...Tunaiombea familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumupoleni sana wana UDSM
Je na wewe kusoma kwako mpaka sijui wapi,bado unaamini kumgonga na gari binadamu mwenzako na kukimbia sio makusudi?,na kunahitaji msamaha kwa namna yeyote ile?r.i.p kijana wetu
mtoa mada umefanya jambo jema kutoa funzo ya kwamba tuwe tunatembea na vitambulisho popote,nami naongezea funzo lingine,wakati wa kuvuka barabara kunapokuwa na magari machache ni hatari zaidi maana magari huenda kasi zaidi na inapokuwa ni usiku hali huwa mbaya zaidi,tuongeze tahadhari zaidi ktk mazingira hayo tajwa
lakini mwisho wa maelezo yako binafsi sijayapenda
kwanini umetengeneza "roho" ya kisasi???kusoma kwako hadi chuo kikuu kunakufanya uamini dereva anaweza kufanya makusudi kumgonga mtu???na hata wa gari la pili na la tatu unaona nao wamefanya makusudi kumgonga?
Dereva angesimama kungekuwa na misiba miwili. R.I.P mwanachuo.
sometimes ukimya pia ni hekima,watu kama wewe unaweza kula pilau msibani ukasema mbona kachumbali hakuna.ukasahau kama pale msibani.
Niliwahi kukuta ajali kama hii. Niliposimama kutoa msaada nilijuta maana nilitukanwa kwa niaba ya madereva wote. Na kibaya zaidi nilipofika hospitali polisi walinianzishia maelezo kama mimi ndio nimegonga. Kwa kifupi nilipata usumbufu sana. Ilikuwa nifike nyumbani saa 12 jioni nilifika saa 6 usiku na gari limetapakaa damu. Ni vizuri kutumia tuu magari ya polisi.

Kaisari usiogope changamoto
Siku nyingine watu watashindwa kukuokoa wewe au mkeo kwa kuogopa matusi au police interogation ama kuchafua nguo na magari ama damu(HIV)
si ndo yule kijana wa Lyamungo kweli ??