JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mwanafunzi wa Upadri (Frateri) wa Kanisa Katoliki Shirika la Roho Mtakatifu Jimbo la Tanga Rogassion Hugho anadaiwa kujinyonga hadi kufa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amezungumza na JamiiForums na kusema “Ni kweli huyo Mwanafunzi wa Upadri amekutwa amejinyonga kwenye mazingira ya eneo wanalosoma (Magamba alipokuwa akiishi).
“Uchunguzi wa awali unaonesha chanzo ni kwamba alifeli masomo yake, akiwa ndiye Mwanafunzi pekee kati ya wote waliofanya mitihani.
“Alikuwa na umri wa Miaka 25 na kinachofanyika kwa sasa ni uchunguzi wa Jeshi la Polisi kuendelea ili kubaini kama kulikuwa kitu kingine kilichosababisha afanye maamuzi hayo.”
Amesema chanzo cha kujinyonga kwake kinadaiwa ni kufeli mtihani wake uliokuwa unampeleka kwenye Daraja la Upadri ambapo wenzake wote wamefaulu kasoro yeye.
Hivyo, kutokana na msongo wa mawazo ndiyo akafikia uamuzi huo wa kujinyonga,” amedai Kamanda Mchunguzi.
Amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho na ukikamilika, taarifa kwa umma itatolewa.