TANZIA Mwanahabari Raphael Waryana na Rafikiye John Dotto wafariki Dunia Muhimbili

TANZIA Mwanahabari Raphael Waryana na Rafikiye John Dotto wafariki Dunia Muhimbili

Pole kwa wafiwa, ila mtoa taarifa ameandika kihuni sana, eti "wawili hawa hakuna anaejua kama mwenzake amefariki."
 
Salaam Wakuu,
View attachment 1677753
John Dotto na Mwanahabari Raphael Waryana mwenye fulana ya blue. Wamepoteza Uhai. Waryana aliyekuwa mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na kiongozi mwandamizi wa timu ya KMC. Alikuwa mwanahabari wa Radio one akiripoti zaidi vipindi vya Nipashe na Mambo Mseto.

Wawili hawa na Marafiki, Wote wawili wamefariki Muhimbili jijini Dar Es Salaam na wawili hawa hakuna anaejua kama mwenzake amefariki.

Dotto alikuwa Mwandishi, Mjasiriamali na Mwanasiasa

Wapumzike mahali pema. Amen!

====

KIONGOZI MWANDAMIZI WA KMC FC AFARIKI DUNIA

Kiongozi Mwandamizi wa Timu ya KMC FC ndugu, Raphael Waryana amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi

Ndugu Waryana atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa ambao alikuwa akiutoa katika Timu ya KMC FC ikiwa ni pamoja na ushirikiano wake katika kipindi ambacho Timu ilipokuwa ikitimiza majukumu yake.

Aidha uongozi umeshtushwa na taarifa hiyo na kuahidi kuendelea kuuenzi mchango wake mkubwa aliokuwa anautoa kwa Timu wakati wa uhai wake.

Uongozi unatoa pole kwa familia yake, mashabiki wa Timu ya KMC FC na Umma wa wanamichezo na kuwaomba wawe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wetu.

Imetolewa na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya KMC FC
Uandishi mwingine bwana, unasema kuwa wote wamefariki halafu unasema hakuna anayejua kama mwenzake kafariki. Toka lini maiti akawa na ufahamu?

Mhubiri 9:5​

Maana, walio hai hujua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui chochote. Hawana tuzo tena; hata kumbukumbu lao limesahauliwa kabisa.
 
Kuna mmoja hapo namdai,,ila namtakia Rip,,japo alinikwazaga sana back then,,,,,
 
Back
Top Bottom