Mwanajeshi ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mtalaka wake na Mwanajeshi

Mwanajeshi ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mtalaka wake na Mwanajeshi

Hivi adhabu ya kunyongwa ipo
Haipo hadi rais asaini unyongwe

Kwa Tanzania ni kiini macho tu haitekelezwi hakuna rais anaekubari kutia saini ili mtu auwawe kwa kunyongwa, maana tangu itungwe hio sheria mwaka 1989 hadi leo hakuna kiumbe msumbufu alimaarufu km mhalifu alienyongwa

Kwa hio mtu akipewa adhabu ya kunyongwa magereza yana-assume km kapewa adhabu ya kifungo cha maisha

Ukija upande wa haki za binadamu na baadhi ya watu wa masuala ya kisheria husema ni kheri mtu km huyo afanye kazi akiwa kwenye usimamizi uko magereza kuliko kumuua ndio maana hua hawauwawi kwa kunyongwa ila wanafungwa maisha

Nchi zinazotekeleza hizo sheria kwa Africa nchi inayoongoza ni Misri ambapo mpaka watu 150 hunyongwa kwa mwaka kwa makosa tofauti

Nchini nyingine yenye kutekeleza kwa ukali ni kutoka bara la Asia ambayo ni China inasemekana kwa mwaka watu 1000 hunyongwa au hupigwa risasi China km adhabu ya kifo kwa makosa tofauti na kati ya hayo ni kosa la kubeba na kusafirisha Madawa ya Kulevya

Napita..
 
Hiyo ni silaha ya kivita, ndio Osama bin Laden muda wote ilikuwa pembeni yake.
Hio silaha sio mchezo njugu zake hua zinatembea km hazitembei yaan ukibonyeza tu hizi hapa na speed yake range per distance inapenya hadi upande wa pili
 
Hivi adhabu ya kunyongwa ipo
Kuuwa kwa kukusudia hakuna adhabu mbadala ni kunyongwa tu.

Waarabu wao hawakuishia kwenye kutowa tu adhabu ya kifo Bali na utekelezaji wake ufanyike ndani ya muda Fulani.

Sisi tumewaachia Marais jukumu la kuidhinisha mtu kunyongwa wote wanakimbia mafile matokeo yake imegeuka kuwa kifungo cha maisha.
 
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha 08/691 KJ Chandarua mkoani Ruvuma, Sajenti Batsin Sanga amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuwaua kwa risasi mtalaka wake na mwanajeshi mwenzake.

Desemba 27 mwaka 2018 katika lango kuu la kambi hiyo, askari huyo mwenye namba za kijeshi MT81337 akiwa na bunduki aina ya AK47, aliwashambulia kwa risasi Veronica Kayombo na Aaskari mwingine na kusababisha wafe papo hapo.

Ingawa jina la askari aliyeuawa pamoja na Veronica halitajwi kwenye hukumu, ushahidi unaonyesha askari huyo alifyatua risasi 10 kati ya 30 alizokabidhiwa huku miili ya marehemu ikikutwa na majeraha ya risasi kichwani.

Hukumu hiyo ilitolewa Septemba 28 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea, Yose Mlyambina aliyesema adhabu kwa anayepatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia ni moja tu, nayo ni kunyongwa hadi kufa.

Awali, kesi iliendeshwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Shaban Mwegelo akisaidiana na Amina Mawoko ila baadaye ikaendeshwa na Wakili Hebel Kihaka akisaidiwa na Lugano Mwasubiria na Tumpare Lawrence.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mlyambina alisema kulingana na ushahidi uliotolewa, mshitakiwa alimpiga risasi ya kichwa Veronica na akamlenga risasi ya kichwa na mkono askari mwenzake.

“Pia silaha iliyotumiwa na mshitakiwa ilikuwa ni ya hatari. Hiyo inadhihirisha mshitakiwa alidhamiria kuwaua marehemu. Mshitakiwa angeweza kuwapiga risasi maeneo mengine ya mwili kama miguuni lakini hakufanya hivyo.

Upande wa mashitaka umethibitisha pasipo kuacha mashaka kwamba mshitakiwa aliwaua watu hao akiwa na dhamira ovu,” alisema Jaji Mlambina katika hukumu yake.

Ukiacha ushahidi huo, jaji alisema mshitakiwa alikanusha kuwaua marehemu ila alikiri kutokea mauaji katika eneo lake la kazi ambako watu wawili walipigwa risasi.

“Mapenzi ni hisia kali sana za ndani ambazo hazielezeki. Kwa lugha rahisi mapenzi ni kitu kizuri sana na chenye harufu nzuri ya kuvutia na ambacho kinadumu milele bila kujali mazingira. Ingawa siku hizi jamii imethibitisha kinyume chake. Mapenzi yamekuwa bidhaa inayoharibika, inaoza na kuzama. Utamu umekuwa uchungu kiasi cha kusababisha wapendanao kuuana wao kwa wao,” alisema jaji akihukumu.

Siku mauaji hayo yanatokea, ilikuwa ni karibu miaka mitatu tangu mshitakiwa atalikiane na Veronica na jana yake Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea ilitoa haki ya mke kutunza mtoto.

Veronica akiwa na rafiki yake aitwaye Jamila Said walienda kwenye kambi hiyo alikokuwa akifanya kazi mshitakiwa ili kupeleka amri hiyo.

Wakiwa lango kuu, mshitakiwa alimuona mtalaka wake na kwenda alipokuwa akiwa ameshika bunduki na kumuuliza amefuata nini na akamjibu wameshahudumiwa.

Ghafla mshitakiwa alichukua bunduki aliyokuwa nayo na kumfyatulia risasi Veronica kisha akaanza kumkimbiza askari mwenzake aliyekuwepo eneo hilo na kumfyatulia risasi pia na wote wawili kufariki.

Jamila alifanikiwa kutoroka kupitia kibanda kilichokuwapo jirani na alipokuwa anakimbia alisikia milio mingine ya risasi kule alikokuwa ametoka baadaye alijulishwa rafiki yake ameuawa na mtalaka wake.

Mshitakiwa akiwa na bunduki alielekea ofisi kuu ya kambi akiendelea kufyatua risasi kabla askari wawili hawajamdhibiti.
doooh masanja mwema kuna kitu unatakiw kujifunza hapa
 
Mapenzi ni hisia kali sana za ndani ambazo hazielezeki. Kwa lugha rahisi mapenzi ni kitu kizuri sana na chenye harufu nzuri ya kuvutia na ambacho kinadumu milele bila kujali mazingira. Ingawa siku hizi jamii imethibitisha kinyume chake. Mapenzi yamekuwa bidhaa inayoharibika, inaoza na kuzama.

Utamu umekuwa uchungu kiasi cha kusababisha wapendanao kuuana wao kwa wao,” alisema jaji akihukumu
HUYU JAJI KWA MISTARI HII ANAYOSHUKA AMETISHA AISEEE KAMA MTUNZI WA NYIMBO.ZA MAPENZI
 
Haipo hadi rais asaini unyongwe

Kwa Tanzania ni kiini macho tu haitekelezwi hakuna rais anaekubari kutia saini ili mtu auwawe kwa kunyongwa, maana tangu itungwe hio sheria mwaka 1989 hadi leo hakuna kiumbe msumbufu alimaarufu km mhalifu alienyongwa

Kwa hio mtu akipewa adhabu ya kunyongwa magereza yana-assume km kapewa adhabu ya kifungo cha maisha

Ukija upande wa haki za binadamu na baadhi ya watu wa masuala ya kisheria husema ni kheri mtu km huyo afanye kazi akiwa kwenye usimamizi uko magereza kuliko kumuua ndio maana hua hawauwawi kwa kunyongwa ila wanafungwa maisha

Nchi zinazotekeleza hizo sheria kwa Africa nchi inayoongoza ni Misri ambapo mpaka watu 150 hunyongwa kwa mwaka kwa makosa tofauti

Nchini nyingine yenye kutekeleza kwa ukali ni kutoka bara la Asia ambayo ni China inasemekana kwa mwaka watu 1000 hunyongwa au hupigwa risasi China km adhabu ya kifo kwa makosa tofauti na kati ya hayo ni kosa la kubeba na kusafirisha Madawa ya Kulevya

Napita..
China hunyonga watu hadi 10000 kwa mwaka

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hii adhabu ingerudishwa tu kuna watu wanamagukio ya ajabu sana
 
Hii adhabu ingerudishwa tu kuna watu wanamagukio ya ajabu sana
Tatizo haki za binadamu na mienendo ya kidini

Mfano kuna Amri kwenye zile Amri 10 nahisi ni ya 7 km sio ya 8 inasema Usiue, sasa unafikiri rais anaejitambua anaweza akasaini hukumu ya kunyongwa mtu hadi kufa huku kuna Amri inayombana asiue? Maana akifanya hivyo atakua anatenda dhambi na anafanya kinyume na Amri aliyopewa
 
China hunyonga watu hadi 10000 kwa mwaka

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Ndio mkuu kwa mujibu wa takwimu za haraka haraka zinazofanyika kila mwaka na hayo ni makadirio tu yaliyopo na hutolewa kwa wale wanaofuatilia kila mwaka ni kiasi gan cha watu wenye hukumu ya kifo adhabu zao zimetekelezwa..
 
Toka 2018 hukumu ndio inatoka leo daah kweli tuna shida kwenye taifa hili
 
Hapo ndio nashangaa miaka 4 yote
Kesi hizi huendeshwa kwa umakini zaidi ndio maana wengine hua wanaachiwa ikithibitika hawakutenda kosa kwa kukusudiwa au wengine hua wanabambikiwa kesi

Kuna kesi moja Jamaa alishtakiwa km huyo kifungo cha maisha na kunyongwa hadi kufa akakaa jela na kutumikia kifungo miaka 17 mwaka wa 18 akaachiwa huru sasa hivi yupo uraiani, unajua ilikuaje kuaje hadi akaachiwa huru?

Nakuja..
 
Hio silaha sio mchezo njugu zake hua zinatembea km hazitembei yaan ukibonyeza tu hizi hapa na speed yake range per distance inapenya hadi upande wa pili
Ulaya na Marekani mbona hawazitumii AK 47, na SMG kwenye vita?
 
Ulaya na Marekani mbona hawazitumii AK 47, na SMG kwenye vita?
Huko ni wanatumia advanced technology zaidi yaan vitani marobot ndio yanayofanya kazi zaidi mkuu

Mfano mzuri unaambiwa hii Network unayotumia hapo ulipo kasi yake ni tofauti kabisa na kasi ya Network iliyopo Ulaya na Marekani kwa hio jiongeze kifkira mkuu
 
Back
Top Bottom