Mwanajeshi ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mtalaka wake na Mwanajeshi

Mwanajeshi ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mtalaka wake na Mwanajeshi

Hakuna rais aliewahi kusaini hukumu ya kifo tangu sheria ilipotungwa hadi leo hajanyongwa hata mtu mmoja kwa saini ya rais, km yupo taja hio kesi
Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI
. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.
 
...Miaka Mitatu baada ya kutalakiana! Ina maana Marehemu Vero allisha Move on lakini Mtalaka Wake alikuwa najamove on...sa Vero alipopata Mshikaji Mwingine, Matokeo ndio yakawa hayo...!!
 
Pumzika Vero. Sijui ulimfanya nn x wako. RIP soja mwingine.

Utakua uliingilia mapenzi ya Vero na Batsin wakaachana. Sisi tumejifunza kwamba tusioe.
Kwa tunayoyaona sasa huku katika Kambi zao na Jinsi hawa Majamaa ( Wajeda ) wanavyotombeana Kutwa Wake zao tegemeeni Taarifa nyingi za Mauwaji ya Kutisha yatokanayo na Visasi na Machungu.
 
Huyo Veronika walitalikiana na muuaji halafu Veronika akawa anachukuliwa na bosi wa muuaji. Siku ya tukio muuaji alikua lindo getini Mara akamuona Vero akaingia getini. Jamaa akahisi Vero anamringishia ndio akampiga risasi Kisha kwenda ofisini kwa mpenzi mpya wa Vero, bahati nzuri secretary wa huyo bosi alimuambia muuaji kwamba bosi hayupo otherwise naye angekua mwendazake. Kisha muuaji akaenda kujisalimisha.
duhh, ss huyo askari mwenzie aliemuua ilikuaje??

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
So sad !! This trend is here to stay !!!
 
Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI
. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.
Hii quote kwenye thread mojawapo humu jamii forum
 
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha 08/691 KJ Chandarua mkoani Ruvuma, Sajenti Batsin Sanga amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuwaua kwa risasi mtalaka wake na mwanajeshi mwenzake.

Desemba 27 mwaka 2018 katika lango kuu la kambi hiyo, askari huyo mwenye namba za kijeshi MT81337 akiwa na bunduki aina ya AK47, aliwashambulia kwa risasi Veronica Kayombo na Aaskari mwingine na kusababisha wafe papo hapo.

Ingawa jina la askari aliyeuawa pamoja na Veronica halitajwi kwenye hukumu, ushahidi unaonyesha askari huyo alifyatua risasi 10 kati ya 30 alizokabidhiwa huku miili ya marehemu ikikutwa na majeraha ya risasi kichwani.

Hukumu hiyo ilitolewa Septemba 28 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea, Yose Mlyambina aliyesema adhabu kwa anayepatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia ni moja tu, nayo ni kunyongwa hadi kufa.

Awali, kesi iliendeshwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Shaban Mwegelo akisaidiana na Amina Mawoko ila baadaye ikaendeshwa na Wakili Hebel Kihaka akisaidiwa na Lugano Mwasubiria na Tumpare Lawrence.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mlyambina alisema kulingana na ushahidi uliotolewa, mshitakiwa alimpiga risasi ya kichwa Veronica na akamlenga risasi ya kichwa na mkono askari mwenzake.

“Pia silaha iliyotumiwa na mshitakiwa ilikuwa ni ya hatari. Hiyo inadhihirisha mshitakiwa alidhamiria kuwaua marehemu. Mshitakiwa angeweza kuwapiga risasi maeneo mengine ya mwili kama miguuni lakini hakufanya hivyo.

Upande wa mashitaka umethibitisha pasipo kuacha mashaka kwamba mshitakiwa aliwaua watu hao akiwa na dhamira ovu,” alisema Jaji Mlambina katika hukumu yake.

Ukiacha ushahidi huo, jaji alisema mshitakiwa alikanusha kuwaua marehemu ila alikiri kutokea mauaji katika eneo lake la kazi ambako watu wawili walipigwa risasi.

“Mapenzi ni hisia kali sana za ndani ambazo hazielezeki. Kwa lugha rahisi mapenzi ni kitu kizuri sana na chenye harufu nzuri ya kuvutia na ambacho kinadumu milele bila kujali mazingira. Ingawa siku hizi jamii imethibitisha kinyume chake. Mapenzi yamekuwa bidhaa inayoharibika, inaoza na kuzama. Utamu umekuwa uchungu kiasi cha kusababisha wapendanao kuuana wao kwa wao,” alisema jaji akihukumu.

Siku mauaji hayo yanatokea, ilikuwa ni karibu miaka mitatu tangu mshitakiwa atalikiane na Veronica na jana yake Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea ilitoa haki ya mke kutunza mtoto.

Veronica akiwa na rafiki yake aitwaye Jamila Said walienda kwenye kambi hiyo alikokuwa akifanya kazi mshitakiwa ili kupeleka amri hiyo.

Wakiwa lango kuu, mshitakiwa alimuona mtalaka wake na kwenda alipokuwa akiwa ameshika bunduki na kumuuliza amefuata nini na akamjibu wameshahudumiwa.

Ghafla mshitakiwa alichukua bunduki aliyokuwa nayo na kumfyatulia risasi Veronica kisha akaanza kumkimbiza askari mwenzake aliyekuwepo eneo hilo na kumfyatulia risasi pia na wote wawili kufariki.

Jamila alifanikiwa kutoroka kupitia kibanda kilichokuwapo jirani na alipokuwa anakimbia alisikia milio mingine ya risasi kule alikokuwa ametoka baadaye alijulishwa rafiki yake ameuawa na mtalaka wake.

Mshitakiwa akiwa na bunduki alielekea ofisi kuu ya kambi akiendelea kufyatua risasi kabla askari wawili hawajamdhibiti.
Wakati tukio linatokea nilikuwa kule mkoani hadi nilishamsahau huyu jamaa.
 
Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI
. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.
Yes, naikumbuka hio kesi
 

Attachments

  • AK-47_type_II_noBG.png
    AK-47_type_II_noBG.png
    312.1 KB · Views: 8
Hakuna rais aliewahi kusaini hukumu ya kifo tangu sheria ilipotungwa hadi leo hajanyongwa hata mtu mmoja nnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnn
 
Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI
. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.....(Jamii forum)
 
Huku vijiweni tunaaminishana wajeda wanaruhusiwa kuua.Sasa imekuwaje tena!!
 
Kijana
Hakuna rais aliewahi kusaini hukumu ya kifo tangu sheria ilipotungwa hadi leo hajanyongwa hata mtu mmoja kwa saini ya rais, km yupo taja hio ke
Kijana acha kupotosha uma..Kipind cha utaifishaji wa mashamba kuna raia alimuua mkuu wa mkoa wa iringa Dr.kleruu.. raia alinyongwa na nyerere ndo mana imemuwia vgum kupata utakatifu kisa kaua..Dig more bro before u conclude
 
Ulaya na Marekani mbona hawazitumii AK 47, na SMG kwenye vita?
Marekani na baadhi ya nchi zilizoendelea, hutengeneza silaha zao, hivyo huzipa majina yao, ila ukizichunguza vizuri, uwezo wake hautofautiani sana.
Kama ilivyo kwa pisto, zinatofautiana majina tu.
 
Back
Top Bottom