Mwanajeshi ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mtalaka wake na Mwanajeshi

Kwanini asingehukumiwa kijeshi hukohuko kambini kwao?
R.I.P Vero na souja.
 
Pole sana kaka hakika hayaelezeki maumivu yake [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Sheria ya kunyongwa Tz imeanzishwa mwaka 1989!

Mkuu nikikwambia wewe ni muongo utasema nakudhihaki?

Je wafungwa walionyongwa katika utawala wa marais wa awamu ya kwanza na awamu ya pili, walinyongwa bila ya sheria hiyo kuwepo?

Pia kumbuka kuwa hukumu ya kunyongwa haibadilishwi na kuwa hukumu ya kifungo cha maisha hadi hukumu hiyo ibatilishwe kwa rufaa ama msamaha wa Rais.

Maisha ya kila siku ya jela kwa mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa ni ya dhiki kuu, maana hutengwa(condemn) bila ya kupata fursa ya kuonana ama kuchanganyika na wafungwa wengine.

Ndiyo maana mfungwa wa kunyongwa huomba heri anyongwe ama abatilishiwe adhabu na kupata kifungo cha maisha kuliko kukaa kwa kufungiwa na kutengwa maisha yake yote.

Hivyo isichukuliwe marais kutokuidhinisha adhabu hiyo ni poa kwa mfungwa, kuishi kwa kutengwa ndani ya gereza la kifungo ni adhabu kali sana kuliko kunyongwa kwenyewe.
 
Ulaya na Marekani mbona hawazitumii AK 47, na SMG kwenye vita?
Hiyo silaha ni aina moja, kuipa sifa ya vitu viwili tofauti ni kudhania kuwa wali siyo ubwabwa!

USA na UK, nchi zenye viwanda vya silaha za kila aina na ubora wa umadhubuti, viache kutumia vya kwao ikashadadie bidhaa ambazo teknolojia yake imeigwa kutoka kwao?

Wadhani huyo mrusi Klashnikov aliyegundua hiyo AK huo mwaka 1947,mataifa ya Marekani na ulaya hawakuwa na teknolojia tayari ya kutengeneza bunduki za rashasha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…