Mwanajeshi ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mtalaka wake na Mwanajeshi

Mwanajeshi ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mtalaka wake na Mwanajeshi

Kwanini asingehukumiwa kijeshi hukohuko kambini kwao?
R.I.P Vero na souja.
 
Pole sana kaka hakika hayaelezeki maumivu yake [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Haipo hadi rais asaini unyongwe

Kwa Tanzania ni kiini macho tu haitekelezwi hakuna rais anaekubari kutia saini ili mtu auwawe kwa kunyongwa, maana tangu itungwe hio sheria mwaka 1989 hadi leo hakuna kiumbe msumbufu alimaarufu km mhalifu alienyongwa

Kwa hio mtu akipewa adhabu ya kunyongwa magereza yana-assume km kapewa adhabu ya kifungo cha maisha

Ukija upande wa haki za binadamu na baadhi ya watu wa masuala ya kisheria husema ni kheri mtu km huyo afanye kazi akiwa kwenye usimamizi uko magereza kuliko kumuua ndio maana hua hawauwawi kwa kunyongwa ila wanafungwa maisha

Nchi zinazotekeleza hizo sheria kwa Africa nchi inayoongoza ni Misri ambapo mpaka watu 150 hunyongwa kwa mwaka kwa makosa tofauti

Nchini nyingine yenye kutekeleza kwa ukali ni kutoka bara la Asia ambayo ni China inasemekana kwa mwaka watu 1000 hunyongwa au hupigwa risasi China km adhabu ya kifo kwa makosa tofauti na kati ya hayo ni kosa la kubeba na kusafirisha Madawa ya Kulevya

Napita..
Sheria ya kunyongwa Tz imeanzishwa mwaka 1989!

Mkuu nikikwambia wewe ni muongo utasema nakudhihaki?

Je wafungwa walionyongwa katika utawala wa marais wa awamu ya kwanza na awamu ya pili, walinyongwa bila ya sheria hiyo kuwepo?

Pia kumbuka kuwa hukumu ya kunyongwa haibadilishwi na kuwa hukumu ya kifungo cha maisha hadi hukumu hiyo ibatilishwe kwa rufaa ama msamaha wa Rais.

Maisha ya kila siku ya jela kwa mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa ni ya dhiki kuu, maana hutengwa(condemn) bila ya kupata fursa ya kuonana ama kuchanganyika na wafungwa wengine.

Ndiyo maana mfungwa wa kunyongwa huomba heri anyongwe ama abatilishiwe adhabu na kupata kifungo cha maisha kuliko kukaa kwa kufungiwa na kutengwa maisha yake yote.

Hivyo isichukuliwe marais kutokuidhinisha adhabu hiyo ni poa kwa mfungwa, kuishi kwa kutengwa ndani ya gereza la kifungo ni adhabu kali sana kuliko kunyongwa kwenyewe.
 
Ulaya na Marekani mbona hawazitumii AK 47, na SMG kwenye vita?
Hiyo silaha ni aina moja, kuipa sifa ya vitu viwili tofauti ni kudhania kuwa wali siyo ubwabwa!

USA na UK, nchi zenye viwanda vya silaha za kila aina na ubora wa umadhubuti, viache kutumia vya kwao ikashadadie bidhaa ambazo teknolojia yake imeigwa kutoka kwao?

Wadhani huyo mrusi Klashnikov aliyegundua hiyo AK huo mwaka 1947,mataifa ya Marekani na ulaya hawakuwa na teknolojia tayari ya kutengeneza bunduki za rashasha?
 
Back
Top Bottom