Mwanajeshi mstaafu ateka mzee wa miaka 80 Ifakara

Mwanajeshi mstaafu ateka mzee wa miaka 80 Ifakara

Ifakara kwa muda sasa matukio ya ajabu ya utekaji na mauaji hayakauki.
 
Bibi Kalembwana mwanae si yupo Kiberege Mwisho wa Lami, Malinyi kuna mtaalam mwingine mpya.

Kwa mvua za karibuni hiyo bajaj imetembea Lupiro mpaka Malinyi kwa masaa mangapi
 
Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la EMMANUEL MKOMAWAGI ambaye alikuwa mwanajeshi Arusha Monduli akishirikiana na mwenyekiti wa kijiji cha Kaporo Ifakara anayeitwa SAIDINA FAYA kumteka mzee mstaafu anayekadiriwa kuwa na miaka 80(jina Kapuni!)ambaye anasumbuliwa na kisukari na presha.

Mzee huyo alichukùliwa kwa udhalilishaji mkubwa akiwa kwake mchana kweupe.

Alikodishiwa wahuni wakaja wakambeba mzobe mzobe wakamweka kwenye bajaji wakiwa wanampiga na kumkanyaga kanyaga (aliwekwa sehemu ya kukanyagia miguu kwenye Bajaji.

Watekaji hao walimsafirisha usiku mzima hadi wilaya nyingine hadi kijiji kinaitwa Ihowanja wilaya ya Malinyi akiwa amenyang'anywa simu pamoja na wallet yake

Tunashukuru Jeshi la Polisi Ifakara mjini kwa kushirikiana na wasamarian wema kumtrack mwanajeshi na kujua yuko huko vijijini kwa bibi mnyoa nywele kwa lengo la kwenda kumnyoa nywele(imani za kishirikina zilizopitwa na wakati)

Tunaomba vyombo vya sheria vimsaidie Mzee huyu kupata haki yake kwani Mwanajeshi anajitapa amestaafu amelipwa kiasi kizuri cha pesa anatamba atashinda hii kesi..

Huyu mzee mstaafu alipokonywa hela alizokua nazo, simu, pamoja na kadi zote za benki na kadi ya NHIF.

Naombeni msaada wa "kisheria" kuhusiana na hili suala la UTEKAJI NA UDHALILISHAJI Kwa huyu mzee .

Natanguliza shukrani

Cc;@Pascal Mayala
Petro E. Mselewa
Hii kesi naijua sana na huyo Mzee ni msukuma ana jina kama la marehemu Rais wa Tanzania!

Kisa cha hii kesi ni mgogoro wa ardhi!

Yule Mzee si alienda kushitaki kwa Mkuu wa Wilaya na mwanajeshi aliwekwa ndani?? Au kuna shida gani zaidi?? Karibu inbox
 
Kesi iko huko ila hadi leo hajui kinachoendelea .i mean hajaitwa na mjeshi anajitapa balaa mtaani kua atahonga
 
Bibi Kalembwana mwanae si yupo Kiberege Mwisho wa Lami, Malinyi kuna mtaalam mwingine mpya.

Kwa mvua za karibuni hiyo bajaj imetembea Lupiro mpaka Malinyi kwa masaa mangapi
Yule wa kiberege alikufa vitu vimerudi huko huko ihowanji kwa mwingine
 
Ndugu zangu wakazi wa wilaya ya Kilombero,Ulanga na Malinyi imani za kishirikina zimetanda kwenye akili zao.
Wanawaza uchawi + kupelekana kwa Kalembwana kunyoona nywele pamoja na mavyuzii ni ujinga sana ndio maana umasikini wa kipato hadi wa akili ni mkubwa sana kwa jamii ile.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Askofu wa Jimbo Kuu la Mahenge Agapiti Ndorobo enzi za huyo bibi mwenyewe waliisha chimbana mikwara kuhusu waumini kwenda kunyolewa nywele ikafika kipindi ukienda kunyolewa unatengwa na kanisa
Naskia kunyolewa ni hiari...sasa huyu alibebwa juu juu na kupigwa juu akiwa haelewi kitu...alidhalilishwa sana aise
 
Ndugu zangu wakazi wa wilaya ya Kilombero,Ulanga na Malinyi imani za kishirikina zimetanda kwenye akili zao.
Wanawaza uchawi + kupelekana kwa Kalembwana kunyoona nywele pamoja na mavyuzii ni ujinga sana ndio maana umasikini wa kipato hadi wa akili ni mkubwa sana kwa jamii ile.
Wanazipeleka wapi na Kwanini wanapelekana kunyolewA
 
Back
Top Bottom