Mwanajeshi wa zamani na mkosoaji wa serikali ya Rwanda auawa chini Uganda

Ilikuwa bora ukoloni kuliko hawa kenge
 
Yaani unatoroka Rwanda unakimbilia Uganda,na unadhani upo mikono salama,hakujua kuwa kagame na Museveni ni akili moja na maswahiba WA kuzikana,ooh My God huyu mwanajeshi alijichanganya Sana RIP
 
Tawala za kiafrika ni za kizandiki.ni tawala zinazojali masilahi ya watawala na familia zao.njia pekee ni kuasi dhidi ya tawala hizo sababu haziamini tena katika demokrasia.
 
kwa hiyo alikuwa anamkosoa Kagame ana akaenda kujificha Uganda?...pole zake
 
Naye hana akili. UNAKIMBIA RWANDA UNAKIMBILIA UGANDA? HANA AKILI.
Kabisa mkuu, ni sawa na kumkimbia simba anaekufukuza ukakimbilia mtoni kwenye mamba na huku unajua huo mto una mamba. Jamaa ndezi sana ila siku za Kagame sio nyingi maana US na EU wameshamchoka wanamlia timing ni suala la muda tu.
 
Jamaa ni mzembe sana. Unamkosoa Kagame halafu unakimbilia Uganda! Bado haitoshi unasafiri umbali wa zaidi kilomita 45 kwenda kukagua ujenzi wa nyumba!!

Wenzake wanaojitambua wamekimbilia Afrika ya Kusini huku wakiishi maisha ya kificho.
Wapo walio uwawa afrika kusini. Huko ndio shida kufa rahisi.

Wahindi waliwaua wakosoaji huko Canada

Urusi ndio usiseme

Kasogi unafahamu yaliyomkuta.

China wanayao pia.

Wamarekqni ndio kabisa.
 
Kagame mwenyewe kama museveni ni mgonjwa. Kwani, ataishi milele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…