Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kwa majonzi makubwa nachukua nafasi hii kuwatangazia ya kwamba dada mama na ndugu yetu mwanaJamiiForums mwenzetu dada niah ametwaliwa kutoka maisha haya..! Amefariki juzi tarehe 2 Dodoma General hospital alikokuwa akipatiwa matibabu
Msiba uko nyumbani kwake Dodoma na ndugu yetu Mwifwa yuko huko hivyo atatujuza zaidi
Mara ya mwisho kabla ya kurejea nchini alikuwa Lebanon Beirut ambapo mumewe ni mwambata wa ubalozi kule.. Mumewe si raia wa Tanzania
Mazishi ni kesho mjini Bukoba ambako ndiko asili yake
Nilimfahamu mwaka 2017 hapa JF na baadae nje ya JF.. Alikuwa ni mama mwenye upendo mkuu ushauri mwanana asiye na majivuno na aliyekuwa anaisaidia bila kubagua
Hakuwa mshiriki sana kwa maana ya kuandika lakini alikuwa msomaji mzuri sana wa karibia kila kilichokuwa kikiandikwa hapa
Alikuwa dada na rafiki mwema kwangu. Nitamkumbuka daima
Kwa ruhusa maalum naweka picha yake ya msibani hapa.
Pumzika kwa amani dada yangu niah 😪