Kuna msemo wa kizungu unasema " if you cant defeat them, Join them"
Serkali ya Awamu ya Tano imeshindwa kabisa hata kuelewa maana ya huu msemo na kufata principle zake.
Tunakumbuka awamu iliyopita iliweza kudhoofisha upizani kwa kuungana nao. Tuliona wabunge wa CCM na upinzani kuwa kama kitu kimoja. Lakini serkali ya leo inatumia nguvu nyingi kuwatenganisha huku ikisahau hii principle.
Kikwete hakuwa mjinga wala mdhaifu kuwaalika wapinzani ikulu na kupiga nao story.
Ukiwa kwenye nyumba ya vioo usijaribu mrushia mawe jirani yako. Utaumia. Hili ndilo linatokea kati ya RC Makonda na Gwajima.
Sasa gwajima anazidi kupata umaarufu wa ajabu. Mimi huwa siamini sana hawa maaskofu wa namna hii ila kwa hali inavyoendelea ni bora kumuamini gwajima kuliko serkal ya Magufuli.
Sasa kila Jmapili masikio ya watanzania huamia kwenye kanisa la Gwajima kutaka kusikia ametoa nini kipya hasa juu ya RC makonda.
Hata mimi apa ninaandika huu uzi huku nikivuta muda ili ifike saa nne nikajiunge kwenye ibada ya Gwajima mubashara kupitia channel yake ya youtube .
Kuhusu Lussu kupewa umaarufu na serkali ya magufuli hili lipo wazi kabisa na jana kupitia uchaguzi wa TLS tumepata prove.
Njama zote za kitoto na zisizokuwa na weledi zimeishia kumpa Lisu ishindi wa kishindo.
Sasa hivi Watanzania tumeanza kupata utamaduni wa kuhoji. Why this, why that, why him etc.
Sasa ni muda muafaka Serkal ibadili mbinu zake za kimafia maana Watanzania tutahoji kila ki2.