Mkuu, William na Harry ni askari kamili na wamefuzu Sandhurst hivyo ukiwaona na suti ni kwamba hawako kikazi.
William ni rubani wa helikopta za uokozi na Harry yumo kwenye special forces na ni kamanda anaeendesha helikopta aina ya Apache sasa hivi ana cheo cha kanali.
Baba yao ni Navy kamanda yaani anaendesha yaani akiwa majini anaendesha meli, akiwa juu anaendesha ndege za kivita na helikopta na akiwa chini ardhini anaongoza vikosi vya ardhini.
Hawa watu wanafanya kazi ambazo kwao zaitwa "engagements" ambapo hujishughulisha na mifuko na kusaidia jamii kupitia mifuko hiyo.
Wanazunguka kila mahala na wana ofisi kabisa na wasaidizi.
Hivyo, ingawa wanakula kodi ya waingereza lakini na wao wanafanya kazi.