Mwanamfalme wa Uingereza Harry kufunga ndoa na muigizaji wa Marekani Meghan Markle

Mwanamfalme wa Uingereza Harry kufunga ndoa na muigizaji wa Marekani Meghan Markle

Oprah kazidi kuwa mbibi hajapendeza hataa!

Serena Williams kapendeza ila yeboyebo zake zimeshaanza kufumuka!

Clooney katoka chicha na baby wake!

Idriss katoka bomba ila bidada kamuangusha na huo mgauni!

Beckham and his wife look mwaaa!
Hahah!, kha Serena nae hakutaka hata kuzi refresh yeboyebo..[emoji1]

Beckhams, sana tu. They never disappoint.
 
Duuuh wazungu wana raha haya machombo ya kwaya na kusindikizia nyimbo kwetu hamna bali maspika makuubwa likishtuliwa ghafla moyo unaruka sarakasi za ajabu [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Princess Diana na Dodi Fayed walitumbukia rasmi katika mapenzi Jumanne ya Juni 3, 1997. Siku 38 baadaye, Ijumaa ya Julai 11, 1997, Princess Diana aliwasili kwenye nyumba ya shamba la Mzee Al Fayed yenye bustani kubwa eneo la San Tropez, kusini mwa Paris, Ufaransa, akiwa na watoto wake, William na Harry.

Wakati huo Dodi Fayed alikuwa chumbani kwake na mchumba wake, Kelly Fisher, mwanamitindo wa Mmarekani. Dodi hakuwakutanisha Kelly na Diana. Wakati Baadaye Diana akiwa katika boti, ndege binafsi ilitumwa kwa ajili ya Kelly. Diana na Kelly hawakujuana.

Kelly alikasirika sana alipogundua kuwa Dodi alimzubaisha ili apate nafasi ya kumtongoza Diana. Hatimaye Diana alirejea Uingereza na watoto wake. Ndipo siku 20 baadaye, Alhamisi ya Julai 31, Diana akarejea tena San Tropez, wakati huu akiwa bila watoto wake. Bado hakujua Dodi alikuwa na uhusiano na Kelly hadi aliposikia katika vyombo vya habari.

Siku hiyo, Julai 31, Kelly Fisher alikuwa Los Angeles, Marekani, akijiandaa kwa ajili ya harusi kati yake na Dodi Fayed iliyokuwa imepangwa kufanyika Jumamosi ya Agosti 9, 1997. Lakini siku mbili kabla ya hapo akavisikia vyombo vya habari duniani vikitangaza mapenzi kati ya Dodi na Diana. Huo ukawa mwisho wa Dodi na Kelly.

Jumba hilo la kifahari lilikuwa limefungwa vinasa sauti kufuatilia mazungumzo ya Diana. Kila alichozungumza Diana hakikuwa siri kwa wale waliomfuatilia.
Gharama ya kuolewa na watu wenye power
 
Back
Top Bottom