Mwanamke adai kupigwa ngumi na mchungaji wakati wa maombi

Mwanamke adai kupigwa ngumi na mchungaji wakati wa maombi

Wanawake ndio wahanga wa waganga na pia kwa hawa mitume na manabii wa uongo
 
Ujinga wa waafrika,
Mnaacha kufanya kazi mnaenda kusomewa biblia na mjanja mmoja na pesa mnachunishwa, upuzi kabisa.

Dini ni silaha kubwa ya umaskini.
Ingekuwa hivyo zilipoanziwa ulaya na uarabuni wangekuwa masikini wa kutupwa
 
Mwanamke mmoja ameshindwa kuzuia hasira zake baada ya kudai kupigwa ngumi ya usoni na mchungaji wakati akimuombea.

Katika video iliyopostiwa kwenye Mtandao wa TikTok, mwanamke huyo anaonekana akiongea kwa hasira kwamba mchungaji alikuwa akimuombea na kumpiga ngumi kwa uchungu usoni kama njia ya kumsukuma kuanguka chini ili kudhihirisha kwamba ameingiwa na Roho Mtakatifu. chanzo. Global Publishers.

View attachment 2355194
Naumia sana matukin haya kiuni.
 
Nilinyanyuka akarudia tena uli nirudi chini. Sifanyi tena huo ujinga wa kwenda sehemu kama hizo😅
Kweli usiende wanaweza ku take advantage ukiwa chini wamalize kabisa
 
Ndo maana sijawahi waamini wachungaji Sijui manabii...sikuzote naamini Imani yangu juu ya Yesu kristo
 
Wakati mwingine matatizo mnajitafutia wenyewe....
Bora ya huyo, wengine wana liwa vizuri tu kwa jina la bwana
 
Sasa wajameni kama Pepo halitaki kutoka!!….. Mtumishi yeye Afanye nini sasa?? pale lilipigwa pepo siyo mtu!! km angepigwa mtu angevuja damu!
 
AAHAHAHAHAH ndo mkomege!! mnatuacha sisi hapa!! ohooo!! naenda kwa gwajima unoana sasa???!! ukipinda kiuno tu watakwambia jinni hilo limetokea kiunoni!
Kiukweli mimi sijawahi kwenda kwa ridhaa yangu mara zote inakuwa kama nimelazimishwa nafanya kumridhisha mtu. Ila now slendi hata iweje maana hata hao watumishi sijawahi kuwaamini
 
Hapana mimi sio mlokole kabisa lakini nimezungukwa na walokole wengi , siku nikajikuta huko kwa mtumishi
Huyo ni mtumishi kivipi na anakata watu mingumi kama Mandonga? Huyo ni mtu mishe!
 
Kama viongozi wa dini hawamuogopi Mungu, na wanachezea jina lake kwa maslahi yao, ingawa wanadai wana ushuhuda wa miujiza yake, waumini wafanyaje?
Siwalaumu watu wasiyo na imani na dini kabisa.
Kuwepo matapeli sio excuse kabisa. Biblia imeweka wazi siku zetu hizi manabii wa uongo watakuwa wengi na watadanganya wengi. Tena ikasema kwa matunda yao tutawatambua.

Kwa hiyo kwa anayesoma Biblia anajua hizi ni nyakati za hatari na kuwepo hawa watumishe ni uthibitisho wa Neno la Mungu.

Kuwepo pesa feki ina maana kuna OG. So badala ya kukataa pesa zote jifunze kujua feki na OG
 
Back
Top Bottom