Demi
JF-Expert Member
- Nov 22, 2016
- 40,466
- 88,695
Ushauri wako naupotezea.Sawa sawa. Na wahindu nao mungu wanayemwamini ni nishati, na wachawi mungu wanayemwaini... na waabudu mashetani mungu wanayemwamini...
Ndugu yangu haijalishi hakimu ninayemwamini mimi huwa anaachia huru wabakaji, siku nikibaka basi nitakutana na hakimu wa ukweli na mvua 30 nitakula. Yule hakimu wa kichwani mwangu hatakuwa kwenye kiti.
So unachoamini ni useless kama sio uhalisia. Kila mtu ana version yake ya Mungu kichwani halafu tena sasa kuna Mungu mwenyewe.
Bahati mbaya huyo mungu wako hayupo. Mungu alimuumba babu yako wa kwanza Adam akiwa mkamilifu. Akaasi na kupoteza ukamilifu. Naye alipoulizwa alimrushia Mungu lawama kama wewe hivi.
Lakini wakati unasema uongo ulikuwa na hiyari ya kusema ukweli. Na bado unataka kumlaumu Mungu kwa uongo uliousema?
Nani anayezini asijue ni jambo baya? Na bado utamlaumu Mungu.
Anyway kama ambavyo mbele ya hakimu inaongea sheria ndivyo siku ile mbele za Mungu. Nakushauri tu kwa upendo fikiria tena majibu bora zaidi ya kumpa Muumba wako siku hiyo. Haya hayana mashiko. Na usisahau yeye atakuwa hakimu wewe utakuwa mshtakiwa. Hutakuwa na nguvu ya kuamua by that time.
Ni ushauri tu kama haufai unaweza kuupotezea!
Umeandika mambo yakufikirika tu na tayari umejiaminisha kuwa mawazo yako ni sahihi ila ya wengine ni pumba.
Kila mmoja abaki na mungu wake anaye mwamini. Mwisho wa siku kila mtu kivyake...