Umenena vema mkuu, lakini mambo yanayoendelea yanafanya mtu uquestion hizi dini sometimes, ingawa ukaribu na Mungu unakuwa umebaki palepale.
Ukiangalia matapeli unaweza kudhani Walokole ni matapeli. But ukweli ni kuwa waganga wa kienyeji, matapeli ya mjini na vitombi nao wanajiita walokole.
Ila kuna watumishi wa Mungu wamenyooka kama rula na wana lengo moja tu, kuhakikisha kondoo wao wanaenda mbinguni. Kama kuna mtu yuko confused nimwelekeze mahali salama. Wapo wengi tu, sema sio maarufu!
Cha msingini mtu kujua hata siku ile Yesu atawaambia sikuwajua ninyi. So kabla hujakaa chini ya mtu au kanisa hakikisha kwanza wanamheshimu Mungu. Kama hawamheshimu Mungu jua utakuwa kinyago chao!
Naamini umewahi soma haya maneno ya Yesu mwenyewe
“Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao.
Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.”
Mt 7:15-20
Na hii hapa
“Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”
Mt 7:21-23