Mwanamke: Aina 10 za wanaume wa kuepuka kuwa na mahusiano nao hawa hapa…!

Mwanamke: Aina 10 za wanaume wa kuepuka kuwa na mahusiano nao hawa hapa…!

magombe junior nafikiri chance ya kubadilika kwa mtu huwa ni ndogo sana,na kubadilika kwenyewe ni mpaka mtu mwenyewe aamue lakini si kwa kushauriwa au kuombwa badilike na famili au mke wake,nimeiexpirience hii maishani mwangu na inaumiza sana.
Ndiyo maana nikasema hapo kama umempenda uvumilivu unahitajika mtu hubadilika taratibu,na kama hakuna uvumilivu basi tena utajikuta una msululu wa wapenzi uliotembea nao
 
Mkuu no 2 kuna watu utakuwa huwatendei haki, kuwa na kazi au kutokuwa na kazi siyo factor. Unaweza kuwa kwenye kazi ndani ya mahusiano kazi ikaisha utamshauri waachane atafute mwenye kazi??!!!! Halafu kipimo cha kujishughulisha ni kipi??!! No 8 pia kuna watu huwatendei haki, kwani ukitoka na manzi mara ya kwanza hela unatakiwa uhesabie usoni kwake??!! Pia kama anamchagulia ni kutokana na uwezo wake asije fedheka baadae kushindwa kulipa bill, vinginevyo kama wa kipato cha chini hawana nafasi katika mapenz.
 
10. Mwanaume mwenye kisirani na asiyeweza kumuuwa nyoka akafa :

sijaielewa vema hii hasa kipande cha mwisho, waweza kumuua nyoka halafu asife!
 
Mkuu siku hizi wanaangalia personality ya mtu na kuchanganua kama hapa kuna mgodi kabla haja kuuliza unafanya kazi gani.
 
Kuna watu hawana kazi ila hata kujishughulisha kuzitafuta hizo kazi hawataki au wanachagua kazi na kazi ikiisha ndani ya mahusiano si huyo mpenzi wako anakuwa anajua issue haiko kwako ipo kwake kama anakupenda atakuvumilia kulingana na ukubwa wa tatizo. Pia siku ya kwanza ndo siku ambayo mwanamke hutambua kuwa anamwanaume wa aina gani na ndo siku ambayo wanaume wengi hujitutumua ili wasionekane.
 
Mkuu siku hizi wanaangalia personality ya mtu na kuchanganua kama hapa kuna mgodi kabla haja kuuliza unafanya kazi gani.
Mkuu unaweza kusema mwanamke anataka wenye pesa lakini si kweli unaweza ukawa na pesa na mwanamke mzuri lakini akawa anachit anatoka na mtu asiye na pesa tena yawezekana yeye akawa anamsaidia hizo pesa umeshwahi kujiuliza ni kwanini? kuna mtu humu kalalamika mpenzi wake ameumwa amemgharamia kila kitu lakini bado akaambiwa hajui kujali
 
10. Mwanaume mwenye kisirani na asiyeweza kumuuwa nyoka akafa :

sijaielewa vema hii hasa kipande cha mwisho, waweza kumuua nyoka halafu asife!
Ili tuseme umemuua nyoka lazima tuthibitishe kuwa kafa haujaelewa nini hapo mkuu
 
Kwa bahati mbaya wanawake waliotulia huolewa na wanaume vicheche
Wanawake ni rahisi kuwaongopea na ukapata unachokihitaji ndo maana hata nyoka hakumfuata Adam pale bustanini
 
yaani awe nazo zote ila ilo la ubahili habaki huko huko maana mimi nina matumizi ya nguvu ataakiwa vipi yale mambo lazima atayatoa wallet lazima iunge urafiki na mimi
 
10. Mwanaume mwenye kisirani na asiyeweza kumuuwa nyoka akafa :
Mwanaume mwenye kisirani ni ngumu sana kuishi naye. Mwanaume mwenye kisirani na anayependa kuweka vitu rohoni na asiyeweza kusamehe ni janga. kuishi na mwanaume wa aina hii ni sawa na kuishi na explosive material ambayo yakipata joto tu hulipuka. Mwanaume umetoka naye mtoko wa kwanza na kwa bahati mbaya mhudumu wa mghahawa akasau kitu katika vitu mlivyoagiza akagomba kupita kiasi na kuwakusanya mameneja wote wa mghahawa akiwemo mpishi mkuu akilalamika.
Na kama hiyo haitoshi mtaondoka hapo mghahawani njia nzima kambeba kichwani mhudumu yule masikini aliyeghafilika mpaka mwisho wa safari yenu na huenda akalala naye kichwani. Mwanaume huyo hafai kama gome la mgomba lisilofaa kwa dawa ya miti shamba wala kuni, labda kwa kufungia ugoro. Huyo mpishe ajiendee zake hakufai.

NILIWAHI KUKUTANA NA HILI JANGA AISEEE.... ILA NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIEPUSHIA HILI.. YAAN AKIKOSEWA NA MTU YEYOTE ATAPAYUKA MNO MPAKA KILA MTU ATAJUA KUWA AMEUDHIWA
 
Mungu afanye msaada kwa akili yangu sitoweza...
 
Back
Top Bottom