Malia Elizabeth, mama mwenye umri wa miaka 38 kutoka Florida, nchini Marekani, alikamatwa kwa tuhuma za kufanya vitendo vya kingono na mnyama, baada ya mume wake ambaye walikuwa wametengana kugundua video ya kamera za usalama ikimuonyesha akifanya kitendo hicho na mbwa wao wa familia aitwaye Ranger.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Charlotte, uchunguzi ulianza baada ya mume huyo kuchapisha tuhuma hizo pamoja na picha kutoka kwenye video kwenye mitandao ya kijamii. Awali, alikuwa ameweka kamera mbili za usalama ndani ya nyumba ili kubaini ni nani aliyekuwa akiiba fedha kwenye chupa ya sarafu.
Alipokuwa akikagua video kutoka kwenye kamera iliyokuwa chumbani, aligundua rekodi za mwaka 2024 zilizomuonyesha Malia akiwa na mbwa huyo wa familia. Mume huyo aliikabidhi laptop iliyokuwa na video hizo kwa wachunguzi.
Alipoulizwa na polisi, Malia alikiri kwamba ndiye aliyeonekana kwenye video na kwamba mbwa huyo alikuwa wake. Hata hivyo, alikanusha kufanya kitendo chochote cha kingono, akidai kwamba alikuwa akimbembeleza tu mbwa huyo. Wachunguzi walisema alionekana kuwa katika hali ya ulevi au kutokuwa sawa wakati wa mahojiano na alitoa maelezo yanayokinzana kuhusu video hiyo.
Malia alipelekwa katika Gereza la Kaunti ya Charlotte na kushtakiwa kwa kosa la second degree ambalo ni felony. Aliendelea kushikiliwa kwa dhamana ya dola 35,000 za Marekani, sawa na takribani shilingi milioni 38 za kitanzania.
Sheriff wa Kaunti ya Charlotte, Bill Prummell, alilaani vikali kitendo hicho, akieleza kuchukizwa na unyanyasaji huo dhidi ya mnyama. Pia alizungumzia picha yake rasmi ya polisi(mugshot )ambapo Malia alionekana akitabasamu sana licha ya kitendo hicho.