Mwanamke ambaye sio rafiki yako hawezi kuwa mkeo

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
MWANAMKE AMBAYE SIO RAFIKI YAKO HAWEZI KUWA MKEO

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Rafiki yako namba moja baada ya Mungu ni Mkeo/Mumeo. Kama hii kwako ni ngumu acha kuoa/kuolewa. Ndoa itakushinda Mapema Sana.

2. Na isipokushinda ukajikaza. Utaishi kwa Mateso na kugugumia. Ndoa ni urafiki wa karibu Sana baina ya Mwanaume na mwanamke. Ukaribu uliopitiliza kuliko kawaida.

3. Unapooa alafu mkeo akawa sio Rafiki yako. Au ukashindwa kumfanya awe Rafiki yako. My friend umefeli pakubwa Sana. Yaani kimsingi hapo maana ya msingi ya ndoa haipo.

4. Mkeo hawezi kukuficha jambo lolote like. Narudia lolote lile kama wewe ni Rafiki yake. Na kama umefanikiwa kumfanya kuwa Rafiki yako.

5. Moja ya Makosa ambayo Wanaume wengi wanayafanya na kupelekea Wanawake kuwaumiza, kuwachezea shere ni kujifanya kauzu, nunda, ubabe na kutomfanya mkewe Rafiki yake. Kiulinzi na kiusalama ndani ya himaya yako umefeli pakubwa.

6. Iko hivi, huwezi mdhibiti mtu ambaye Yuko mbali na wewe. Huwezi mtawala mwanamke ambaye sio Rafiki yako.

7. Kwenye utawala wa kijeshi na serikali, power ina operate zaidi palipo na ukaribu.
Ndio maana unaona hata mataifa kama Amerika yakitaka kukudhibiti au kukutawala yanakukaribia karibu kabisa au ndani yako kabisa. Kwani Fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

8. Mkeo ili umtawale lazima uwe naye karibu Kihisia, kiroho, kimwili na kiakili. Awe Rafiki yako.

9. Falsafa hizi za kitibeli hazijawahi kushindwa poppet pale kama ukizitumia kwa kufuata itifaki.

10. Unapokuwa karibu na mkeo automatically unakuwa karibu na familia yako. Unajua asilimia 99% ya kinachoendelea ndani ya himaya yako.

11. Unapokuwa Mbali na Mkeo. Kwamba sio Rafiki yako. Huna lolote ujualo ndani ya familia na himaya yako labda asilimia moja 1%. Tuu ambayo no majina yao, wanaafya au hawana n.k

12. Usipojua Himaya yako hujui future ya Familia yako. Kifupi huwezi kuweka malengo ya Himaya yako kama huijui vizuri. Malengo yako yatakuwa irrelevant

13. Urafiki ni kuwa karibu. Kwenye ukaribu kuna kujuana. Kumjua vizuri mkeo

14. Urafiki ni Uhuru. Kupitia urafiki MTU anakuwa huru kujiachia.
Kwenye Uhuru ndipo mtu utamjua tabia zake vilivyo.

15. TaikonMaster huwaga nawaambia Kila Siku. Wanawake ni viumbe wanaoeleweka kama vile binadamu wengine kwa sababu wanatumia mfumo wa saikolojia ya kawaida ya binadamu

16. Waliosema wanawake hawaeleweki ni kundi la watu ambao lilikuwa linawasoma na kuwachunguza wanawake wakiwa watumwa, wafungwa na wakiwa hawapo huru.

17. Mimi kama Mwanafalsafa. Huwezi mchunguza na kumjua mtu aliyefungwa, mtumwa, asiye huru na ukajua tabia zake halisi.

18. Mfungue, MPE Uhuru, mkomboe then utamjua mtu huyo ni mtu wa aina gani.

19. Ni Sawa na wale wanaosema Mtu akipata pesa anabadilika na kuwa jeuri nope! Habadiliki. MTU habadiliki. Ila ana adapt kulingana na mzingira ila uasilia wa mtu upo palepale.

20. MTU kupata pesa inamfanya awe huru, na anakuwa sio mfungwa tena. So anaonyesha ule uhalisia wake sasa. Kama ni mpole au mkali. Kama anahuruma au mkatili. N.k.
Concepts hizo najaribu kuziingiza humu nikojaribu kushona Ile hoja ya urafiki na Uhuru na kumjua mtu.

21. Mwanamke anapokuwa Rafiki yako akakuamini kwa kiwango cha juu Sana. Haoni shida kukuonyesha madhaifu yake waziwazi. Kukueleza shida zake waziwazi.

22. Ikiwa mkeo sio Rafiki yako basi elewa siri zako zipo nje ya familia yako.
Kuna mtu ambaye ni Rafiki wa mkeo kuliko wewe anazosiri zako. Anakuchora.

23. Rafiki wa mkeo hapaswi kuwa Mama/ babaake, Mchungaji au sheikhe wake, mganga wake, shostiake, Mdogo wake au yeyote Bali wewe hapo.

24. Kumbuka Mwanamke anamashimo Saba yanayoonekana.
Shimo la nane halionekani.

25. Shimo la Saba lazima ulijaze vizuri na uweze kulitumia vizuri ili mashimo mawili kule juu(masikio) yakusikie. Shimo la Saba ni Papuchi.
Hili anapiga yeyote. Sio ajabu hukumkuta bikra.

26. Shimo la nane lisiloonekana lipo moyoni. Hilo ndio la urafiki uliopitiliza. Ukiweza kulijaza hilo. Hayo mashimo Saba yaliyobakia utayamudu.

27. Bahati Mbaya shimo la nane wengi hawalijui, hawajawahi kulisikia au kuambiwa habari zake.

28. Utasikia mwanamke wangu kiburi, hasikii, anasikiliza mashoga zake, au anamsikiliza zaidi mamaake.

29. Nishaeleza vyakutosha.

Mwenye swali aweza kuuliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mapenzi hayanaga muongozo bwashee, bora uwafundishe madogo jinsi ya kula ugali kwa picha ya samaki , kubana matumizi , ukocha wa mapenzi unachemka kinouma, karibu bia na nguruwe hapa🍺🍺

Wanaosema kitu Fulani hakina muongozo ujue wamefeli.
Hakuna kitu chochote kisicho na Muongozo. Weka akilini hiyo.

Sema wewe au Mimi kitu hiki sijui muongozo wake ila sio kitu Fulani hakina muongozo/formula
 
Mpare acha nilewe tu ogopa watu wanaolala uchi , mimi nimemaliza

Mkuu wewe tupia vitu lakini elewa kwenye haya maisha Kila jambo lina Formula zake.
Kutojua formula Fulani katika Jambo Fulani haimaanishi Jambo Hilo halina formula

Epuka kauli za wenye upeo Mdogo kama Maisha hayana formula 😂😂

Yaani wanahisi mambo yanajiendea tuu. Yaani kufikiri hivyo tuu ni dalili kichwa haifanyi KAZI vizuri.

Kama huioni formula ya maisha. Basi elewa aliyebuni hayo maisha anajua formula zake
 
Nilishamaliza bwashee, ni maoni yangu tu mlevi mimi🤣
 
Ujinga ambao upo JF na mitandao mingi ni generalization

Kwa experience ndogo ya ndoa ambayo ni less than ten years unaamini unajua Kila kitu .

Ni MUHIMU baadhi ya mambo mkawa mnatumia I , me and myself

Kwakuwa kuishi na MTU yeyote awe KE , au ME is very complicated hakuna muongozo wala kanuni

Zaidi zaidi ukubali kuvumilia maumivu , madhaifu na senseless dramas za MTU wako

Madogo wengi wa JF ambao wapo below 60 Wana less life experience ila Sasa
 
Mapenzi hayanaga muongozo bwashee, bora uwafundishe madogo jinsi ya kula ugali kwa picha ya samaki , kubana matumizi , ukocha wa mapenzi unachemka kinouma, karibu bia na nguruwe hapa🍺🍺
Pia, jinsi ya kula ugali mkubwa kwa ugali mdogo. yaani 'kuufanya ugali mkubwa kama ugali, na ule mdogo kuufanya mboga tamu sana'.

Ni hayo tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…