Mwanamke ambaye sio rafiki yako hawezi kuwa mkeo

Mwanamke ambaye sio rafiki yako hawezi kuwa mkeo

Urafiki mkubwa haimaanishi usiwe na mipaka. Haimaanishi ukabidhi ID yako yote.

Hapo ndipo Matumizi ya Akili yalipo.
Urafiki unakua kulingana na wakati pia. So kadiri MTU unavyoushi naye ndivyo mnavyozidi kusogeleana.

Kuna kanuni na formula za urafiki. Sio MTU umekutana naye Leo au mna miezi mitatu au mwaka unajiachia nope!


Hii ni kanuni nzuri na iko relevant

Lakini inategemea mpaka umeuwekea wapi, na unaufungua wakati gani ili mshare mambo yenu

Nakuelewa.
Na ni vizuri umetahadharisha hili maana wengine wanaweza kujiachia moja kwa moja bila tahadhari


Uhuru lazima uwe proportional na uwezo wa Akili.
Uhuru wenye maadili.

Inategemea na mahusiano yenu yalivyo lakini na upeo wa akili wa wahusika.

Uhuru unapouachia unauachia polepole kulingana na uelewa na ukuaji wa akili qa mhusika.

Mfano, watoto wako unawabana wakiwa wadogo kwa sababu hawana uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi.
Lakini kadiri wanavyokua huku ukiwafundisha ndivyo unavyoongea Uhuru wao kidogo kidogo mpaka pale ambapo wakikua kabisa na unawaacha wakijiamulia kwa Uhuru mambo yao.

Ndivyo hivyohivyo kwenye Mahusiano
Copy
 
Mkuu wewe tupia vitu lakini elewa kwenye haya maisha Kila jambo lina Formula zake.
Kutojua formula Fulani katika Jambo Fulani haimaanishi Jambo Hilo halina formula

Epuka kauli za wenye upeo Mdogo kama Maisha hayana formula 😂😂

Yaani wanahisi mambo yanajiendea tuu. Yaani kufikiri hivyo tuu ni dalili kichwa haifanyi KAZI vizuri.

Kama huioni formula ya maisha. Basi elewa aliyebuni hayo maisha anajua formula zake
Kwani mkuu haya umeyajuaje wakati hapa duniani sisi wote ni wageni mkuu???
 
MWANAMKE AMBAYE SIO RAFIKI YAKO HAWEZI KUWA MKEO

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Rafiki yako namba moja baada ya Mungu ni Mkeo/Mumeo. Kama hii kwako ni ngumu acha kuoa/kuolewa. Ndoa itakushinda Mapema Sana.

2. Na isipokushinda ukajikaza. Utaishi kwa Mateso na kugugumia. Ndoa ni urafiki wa karibu Sana baina ya Mwanaume na mwanamke. Ukaribu uliopitiliza kuliko kawaida.

3. Unapooa alafu mkeo akawa sio Rafiki yako. Au ukashindwa kumfanya awe Rafiki yako. My friend umefeli pakubwa Sana. Yaani kimsingi hapo maana ya msingi ya ndoa haipo.

4. Mkeo hawezi kukuficha jambo lolote like. Narudia lolote lile kama wewe ni Rafiki yake. Na kama umefanikiwa kumfanya kuwa Rafiki yako.

5. Moja ya Makosa ambayo Wanaume wengi wanayafanya na kupelekea Wanawake kuwaumiza, kuwachezea shere ni kujifanya kauzu, nunda, ubabe na kutomfanya mkewe Rafiki yake. Kiulinzi na kiusalama ndani ya himaya yako umefeli pakubwa.

6. Iko hivi, huwezi mdhibiti mtu ambaye Yuko mbali na wewe. Huwezi mtawala mwanamke ambaye sio Rafiki yako.

7. Kwenye utawala wa kijeshi na serikali, power ina operate zaidi palipo na ukaribu.
Ndio maana unaona hata mataifa kama Amerika yakitaka kukudhibiti au kukutawala yanakukaribia karibu kabisa au ndani yako kabisa. Kwani Fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

8. Mkeo ili umtawale lazima uwe naye karibu Kihisia, kiroho, kimwili na kiakili. Awe Rafiki yako.

9. Falsafa hizi za kitibeli hazijawahi kushindwa poppet pale kama ukizitumia kwa kufuata itifaki.

10. Unapokuwa karibu na mkeo automatically unakuwa karibu na familia yako. Unajua asilimia 99% ya kinachoendelea ndani ya himaya yako.

11. Unapokuwa Mbali na Mkeo. Kwamba sio Rafiki yako. Huna lolote ujualo ndani ya familia na himaya yako labda asilimia moja 1%. Tuu ambayo no majina yao, wanaafya au hawana n.k

12. Usipojua Himaya yako hujui future ya Familia yako. Kifupi huwezi kuweka malengo ya Himaya yako kama huijui vizuri. Malengo yako yatakuwa irrelevant

13. Urafiki ni kuwa karibu. Kwenye ukaribu kuna kujuana. Kumjua vizuri mkeo

14. Urafiki ni Uhuru. Kupitia urafiki MTU anakuwa huru kujiachia.
Kwenye Uhuru ndipo mtu utamjua tabia zake vilivyo.

15. TaikonMaster huwaga nawaambia Kila Siku. Wanawake ni viumbe wanaoeleweka kama vile binadamu wengine kwa sababu wanatumia mfumo wa saikolojia ya kawaida ya binadamu

16. Waliosema wanawake hawaeleweki ni kundi la watu ambao lilikuwa linawasoma na kuwachunguza wanawake wakiwa watumwa, wafungwa na wakiwa hawapo huru.

17. Mimi kama Mwanafalsafa. Huwezi mchunguza na kumjua mtu aliyefungwa, mtumwa, asiye huru na ukajua tabia zake halisi.

18. Mfungue, MPE Uhuru, mkomboe then utamjua mtu huyo ni mtu wa aina gani.

19. Ni Sawa na wale wanaosema Mtu akipata pesa anabadilika na kuwa jeuri nope! Habadiliki. MTU habadiliki. Ila ana adapt kulingana na mzingira ila uasilia wa mtu upo palepale.

20. MTU kupata pesa inamfanya awe huru, na anakuwa sio mfungwa tena. So anaonyesha ule uhalisia wake sasa. Kama ni mpole au mkali. Kama anahuruma au mkatili. N.k.
Concepts hizo najaribu kuziingiza humu nikojaribu kushona Ile hoja ya urafiki na Uhuru na kumjua mtu.

21. Mwanamke anapokuwa Rafiki yako akakuamini kwa kiwango cha juu Sana. Haoni shida kukuonyesha madhaifu yake waziwazi. Kukueleza shida zake waziwazi.

22. Ikiwa mkeo sio Rafiki yako basi elewa siri zako zipo nje ya familia yako.
Kuna mtu ambaye ni Rafiki wa mkeo kuliko wewe anazosiri zako. Anakuchora.

23. Rafiki wa mkeo hapaswi kuwa Mama/ babaake, Mchungaji au sheikhe wake, mganga wake, shostiake, Mdogo wake au yeyote Bali wewe hapo.

24. Kumbuka Mwanamke anamashimo Saba yanayoonekana.
Shimo la nane halionekani.

25. Shimo la Saba lazima ulijaze vizuri na uweze kulitumia vizuri ili mashimo mawili kule juu(masikio) yakusikie. Shimo la Saba ni Papuchi.
Hili anapiga yeyote. Sio ajabu hukumkuta bikra.

26. Shimo la nane lisiloonekana lipo moyoni. Hilo ndio la urafiki uliopitiliza. Ukiweza kulijaza hilo. Hayo mashimo Saba yaliyobakia utayamudu.

27. Bahati Mbaya shimo la nane wengi hawalijui, hawajawahi kulisikia au kuambiwa habari zake.

28. Utasikia mwanamke wangu kiburi, hasikii, anasikiliza mashoga zake, au anamsikiliza zaidi mamaake.

29. Nishaeleza vyakutosha.

Mwenye swali aweza kuuliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Ex kaolewa ananiita Mimi rafiki..

Hiyo imekaaje mtibeli
 
Back
Top Bottom