Ukazaa naye au ulisepa? Na kama ulisepa ulifanikiwaje?
Namfahamu mwamba mmoja yeye katika pitapita za ujanani akamtia mimba mwanamke mmoja. Mwanamke alikuwa na uwezo wake na hakutaka hata kumsumbua jamaa. Bidada akasafiri kwenda mkoa mwingine na wakapotezana na jamaa.
Akazaa mtoto wa kiume huko. Huku jamaa akaanza maisha yake na akaowa. Bidada yeye ana uwezo kifedha na hataki kuzaa kila mtoto na baba yake. Akaamua kumtafuta mwamba na kumwambia pamoja na kwamba ameowa, yeye anachohitaji ni kuzaa naye tu. Hivyo bidada alipolea mtoto wake na kufka miaka mitano, akaanza kumtafuta mwamba. Wakazaa wa pili.. Mpaka sasa wana watatu na bidada wala hasumbui..