Mwanamke anayejitambua hawezi kuwa Mke wa Pili au mchepuko

Mwanamke anayejitambua hawezi kuwa Mke wa Pili au mchepuko

Second option kivipi,wakati mke wa kwanza nilioa iringa 1999 wa pili dar 2005!?..kule iringa ningemuonaje huyu wa pili aliyekua dar Ili asiwe 'second option'!?
Kwani second option mpaka uione?
Unaweza Ukawa na wazo hili Leo lakinimiaka mitatu ijayo ukapata wzo jingine mbadala àmbalo haukuwa nalo kipindi ukifanya wazo la Kwanza.

Mke WA pili NI second option àmbaye husababishwa na mambo yafuatayo;
1. Tamaa na kutojizuia Kwa Sisi Wanaume.
2. Mke kuwa na madhaifu na kero Ambazo zinamkatisha tama Mwanaume

3. Uchaguzi mbaya au ushamba, ya ulimbukeni wa mapenzi.
Wakati Mtu anafanya uchaguzi WA Kwanza labda alikuwa na wenge, au Maskini au kapuku hivyo hakuchagua mwanamke WA Ndoto yake baàda ya kujanjaruka na kupata kipato akaona Mke WA Kwanza hakuwa Sahihi.

4.Mila potofu Kwa Kwamba Kuoa Wake wengi NI ufahari.
 
MWANAMKE ANAYEJITAMBUA HAWEZI KUWA MCHEPUKO AU MKE WA PILI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Binti yàngu, kwetu Watibeli ni mwiko Kwa Binti zetu kuolewa Mke wa Pili au Uke Wenza au Kuwa mchepuko.

Huko ni kutojitambua, kujidhalilisha na dalili ya umaskini na uvivu.

Wewe siô mzuri mpaka úwe Mke WA pili au úwe mchepuko?
Wewe siô mchapakazi na mwenye uwezo wa kujitegemea mpaka úwe Mke WA pili au mchepuko.

Mwanamke mwenye mzuri kwelikweli hawezi kuwa Mchepuko au Mke WA pili. Hakunaga huyo Mwanamke.

Mwanamke anayefanya Kazi na kujitegemea hawezi kuwa Mke WA pili au mchepuko.

Kama nilivyokufunza Binti yàngu, kuwa Sisi Watibeli kufanya Kazi ni Dini. Lazima ufanye Kazi uweze kujitegemea mwenyewe.
Ndoa pia ni Dini lakini haimaanishi úwe Mke wa Pili au mchepuko.

Ukijitegemea Huwezi kuwa Mke WA pili Daima dawamu.

Kitu kizuri huwa chaguo la Kwanza. Kitu kinachopendwa huwa chaguo la Kwanza Binti yàngu. Usikubali kuwa na kuitwa wa ziada au nyongeza. Wewe siô wanyonyeza. Wewe NI wathamani.

Úkiwa mvivu na mwenye kumtegemea Mwanaume, hutaki kufanya Kazi na kujitegemea unavunja utu wako na Kwa hakika Watu watakudharau ikiwemo kuwekwa mchepuko au Mke wa Pili.

Kuolewa Mke WA pili au mchepuko NI kukosa Soko, haiwezeniki Wanawake wenzako Kila Siku wanaolewa na kupata Wanaume waô wènyewe alafu wewe úwe mpàngo wa kando au Mke WA Pili.

Huo ni Mkosi
Huko ni kujichafulia Ñyota yako. Kuizim.

Kuitwa Mke mdogo Binti yàngu siô Sifa Njema. Wewe siô Bi. Mdogo. Nilikuzaa úwe Mke Mkubwa Kwa Mwanaume atakayekupa First priority. Sikukuzaa uitwe Bi. Mdogo au Nyumba ndogo.

Wewes siô Bi. Mdogo.
Nyumba yako Kamwe isiitwe Nyumba ndogo.
Kamwe Usiitwe Mpàngo wa kando au mchepuko. Wewe ni Njia kuu, Mke Mkubwa. Nyumba kûbwa.

Wewe ni Highway, michepuko itoke kwako hiyo siô kesi lakini siô wewe ati úwe mchepuko Kutoka Njia kuu. Huko ni kujidhalilisha. Binti za Tibeli Kamwe na haitokuja kutokea wakawa na sîfa hiyo.

Kwani unaharaka gàni?
Wanaume wa kukuoa wàpo anakimbilia kuwa Mke WA pili au mchepuko ili kushusha hadhi na Ñyota yako Maisha yako yôte Kisa nini?

Fanya Kazi wewe NI Mwanamke unayeweza kujitegemea.

Elewa, Mwanamke mzuri anayefanya Kazi akajitegemea hawezi kuwa Mke WA pili au mchepuko Kwa sababu Wanaume weñye Akili hujua thamani yake na watamuoa akiwa nafasi ya Kwanza.

Fanya Kazi, linda heshima yako na thamani yako kama Mwanamke.

Masuala ya kusema mbona Zamani Bibi zako walikuwa wanaolewa Wake Wenza au Michepuko hiyo ilikuwa Zamani Wakati Wanawake wakiwa watumwa.

Tenà hata hizô Zamani Binti za Tibeli na Wanawake wa Tibeli hawakuwahi kuolewa Mke wa Pili Wala kuwa michepuko.

Hiyo siô desturi ya Wanawake Bora wanaojitambua.
Hilo la Mke WA pili au mchepuko Acha Wengine wafanye lakini siô wewe Binti yàngu. .
Baadhi ya Mapokeo ya Dini àmbayo hayakufuata HAKI Bali yalifuata matamanio ya Wanadamu na matamanio ya waandishi wa Wakati huo usiyafuate.

Mimi Baba yako, na Mama yako ndivyo tulivyokuagiza hayo. Yasikilize maneno yàngu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Kumbe michepuko ni mahututi hawajitambui wako hoi 😂😂
 
Kwani second option mpaka uione?
Unaweza Ukawa na wazo hili Leo lakinimiaka mitatu ijayo ukapata wzo jingine mbadala àmbalo haukuwa nalo kipindi ukifanya wazo la Kwanza.

Mke WA pili NI second option àmbaye husababishwa na mambo yafuatayo;
1. Tamaa na kutojizuia Kwa Sisi Wanaume.
2. Mke kuwa na madhaifu na kero Ambazo zinamkatisha tama Mwanaume

3. Uchaguzi mbaya au ushamba, ya ulimbukeni wa mapenzi.
Wakati Mtu anafanya uchaguzi WA Kwanza labda alikuwa na wenge, au Maskini au kapuku hivyo hakuchagua mwanamke WA Ndoto yake baàda ya kujanjaruka na kupata kipato akaona Mke WA Kwanza hakuwa Sahihi.

4.Mila potofu Kwa Kwamba Kuoa Wake wengi NI ufahari.
Kea muktadha wa mke sharti wawepo wote sehemu moja wakati mmoja na umchague mmoja kisha mwingine afuatie,ndipo awa second option,kwa mpira vilevile ukimuanzisha Aziz ki ukamtoa na kumuingiza chama,hapo chama ni second option
 
Wewe Mkeo akitaka úwe Mume WA pili utakubali?
 
Back
Top Bottom