Mwanamke anayejitambua hawezi kuwa Mke wa Pili au mchepuko

Mwanamke anayejitambua hawezi kuwa Mke wa Pili au mchepuko

MWANAMKE ANAYEJITAMBUA HAWEZI KUWA MCHEPUKO AU MKE WA PILI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Binti yàngu, kwetu Watibeli ni mwiko Kwa Binti zetu kuolewa Mke wa Pili au Uke Wenza au Kuwa mchepuko. Huko ni kutojitambua, kujidhalilisha na dalili ya umaskini na uvivu.

Wewe sio mzuri mpaka úwe Mke WA pili au úwe mchepuko? Wewe sio mchapakazi na mwenye uwezo wa kujitegemea mpaka úwe Mke WA pili au mchepuko.

Mwanamke mwenye mzuri kwelikweli hawezi kuwa Mchepuko au Mke WA pili. Hakunaga huyo Mwanamke. Mwanamke anayefanya Kazi na kujitegemea hawezi kuwa Mke WA pili au mchepuko.

Kama nilivyokufunza Binti yàngu, kuwa Sisi Watibeli kufanya Kazi ni Dini. Lazima ufanye Kazi uweze kujitegemea mwenyewe. Ndoa pia ni Dini lakini haimaanishi úwe Mke wa Pili au mchepuko.

Ukijitegemea Huwezi kuwa Mke wa pili Daima dawamu.

Kitu kizuri huwa chaguo la Kwanza. Kitu kinachopendwa huwa chaguo la Kwanza Binti yàngu. Usikubali kuwa na kuitwa wa ziada au nyongeza. Wewe siô wanyonyeza. Wewe NI wathamani.

Úkiwa mvivu na mwenye kumtegemea Mwanaume, hutaki kufanya Kazi na kujitegemea unavunja utu wako na Kwa hakika Watu watakudharau ikiwemo kuwekwa mchepuko au Mke wa Pili.

Kuolewa Mke WA pili au mchepuko NI kukosa Soko, haiwezeniki Wanawake wenzako Kila Siku wanaolewa na kupata Wanaume waô wènyewe alafu wewe úwe mpàngo wa kando au Mke WA Pili.

Huo ni Mkosi huko ni kujichafulia nyota yako. Kuizim.

Kuitwa Mke mdogo Binti yàngu siô Sifa Njema. Wewe siô Bi. Mdogo. Nilikuzaa úwe Mke Mkubwa Kwa Mwanaume atakayekupa First priority. Sikukuzaa uitwe Bi. Mdogo au Nyumba ndogo.

Wewes sio Bi. Mdogo. Nyumba yako Kamwe isiitwe Nyumba ndogo. Kamwe Usiitwe Mpàngo wa kando au mchepuko. Wewe ni Njia kuu, Mke Mkubwa Nyumba kubwa.

Wewe ni Highway, michepuko itoke kwako hiyo siô kesi lakini siô wewe ati úwe mchepuko Kutoka Njia kuu. Huko ni kujidhalilisha. Binti za Tibeli Kamwe na haitokuja kutokea wakawa na sîfa hiyo.

Kwani unaharaka gàni? Wanaume wa kukuoa wàpo anakimbilia kuwa Mke WA pili au mchepuko ili kushusha hadhi na Ñyota yako Maisha yako yôte Kisa nini?

Fanya Kazi wewe NI Mwanamke unayeweza kujitegemea.

Elewa, Mwanamke mzuri anayefanya Kazi akajitegemea hawezi kuwa Mke WA pili au mchepuko Kwa sababu Wanaume weñye Akili hujua thamani yake na watamuoa akiwa nafasi ya Kwanza.

Fanya Kazi, linda heshima yako na thamani yako kama Mwanamke. Masuala ya kusema mbona Zamani Bibi zako walikuwa wanaolewa Wake Wenza au Michepuko hiyo ilikuwa Zamani Wakati Wanawake wakiwa watumwa.

Tena hata hizo Zamani Binti za Tibeli na Wanawake wa Tibeli hawakuwahi kuolewa Mke wa Pili Wala kuwa michepuko.

Hiyo siô desturi ya Wanawake Bora wanaojitambua. Hilo la Mke WA pili au mchepuko Acha Wengine wafanye lakini siô wewe Binti yàngu. .

Baadhi ya Mapokeo ya Dini àmbayo hayakufuata HAKI Bali yalifuata matamanio ya Wanadamu na matamanio ya waandishi wa Wakati huo usiyafuate.

Mimi Baba yako, na Mama yako ndivyo tulivyokuagiza hayo. Yasikilize maneno yàngu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Kwa kuwa wewe ni mwana FASIHI...ninaamini ujumbe wako unaenda mbele zaidi ya MKE.....Ninaamini unawatia moyo watanzania kupambana na ku-aim to be the best katika kila jambo unalolifanya...kama ni elimu, michezo,,,,,nk.

Ila kama ujumbe wako unalenga kuzungumzia MKE na wewe haujavuka miaka 70 .....basi nakusihi tema mate chini....maana umetukana kijiji. Swala la kuoa au kuolewa sio la akili za kibinadamu........Pia ndoa hazifanani...ndoa ya wazazi wako haiwezo fanana na ya kwako,,,,,,,Huo ni mtazamo wako wewe na wala sio wa WATIBELI........Mwache BUNTI yako awe huru. Pia kumbuka furaha ni subjective......kama wewe unafurahia kuwa na mke mmoja...wenzako wanafurahia kuwa na wake wengi
 
Nimesema ulaya hawaruhusu mitala na haipo kisheria, sijakataa kama hakuna wazungu wanapenda mitala. Tunarudi pale pale, kila binadamu ana mtazamo wake kuhusu jambo fulani. Mitazamo ya watu na iheshimiwe. Hatuwezi kuwa na mitazamo inayofanana hata siku moja.
Wakati mwingine hao Namba Moja huwa wanakuwa wake wazuri sana...ila tatizo linakuja kwa MUME.....Mume anakuwa na vituko kiasi MKE Mkubwa anaamua kuachana naye na kwenda kutafuta KIBEN-TEN......Na huyo KIBEN Ten anakuwa na Mke...So MKE mkubwa above 35 anaenda kuolewa na Kiben-ten cha miaka 23 ambacho kinakuwa na MKe wa Miaka 22.......Jamaa yangu mambo ya ndoa yaache kama yalivyo.....na usije shangaa mke wako analiwa na mume wa mtu....
 
Mitazamo potofu inayoleta vurugu na migogoro ndàni ya jamii haiwezi kuheshimiwa.

Mitazamo inayoumiza Wengine na kuharibu Maisha ya Wengine haiwezi kuheshimiwa
 
Kwa kuwa wewe ni mwana FASIHI...ninaamini ujumbe wako unaenda mbele zaidi ya MKE.....Ninaamini unawatia moyo watanzania kupambana na ku-aim to be the best katika kila jambo unalolifanya...kama ni elimu, michezo,,,,,nk.

Ila kama ujumbe wako unalenga kuzungumzia MKE na wewe haujavuka miaka 70 .....basi nakusihi tema mate chini....maana umetukana kijiji. Swala la kuoa au kuolewa sio la akili za kibinadamu........Pia ndoa hazifanani...ndoa ya wazazi wako haiwezo fanana na ya kwako,,,,,,,Huo ni mtazamo wako wewe na wala sio wa WATIBELI........Mwache BUNTI yako awe huru. Pia kumbuka furaha ni subjective......kama wewe unafurahia kuwa na mke mmoja...wenzako wanafurahia kuwa na wake wengi

Watibeli mitazamo yetu Inafanana Kwa sababu inazingatia HAKI, UPENDO, AKILI NA UKWELI.

Unaposema siô mtazamo wa Watibeli unamaanisha unawajua hao Watu?
 
Wakati mwingine hao Namba Moja huwa wanakuwa wake wazuri sana...ila tatizo linakuja kwa MUME.....Mume anakuwa na vituko kiasi MKE Mkubwa anaamua kuachana naye na kwenda kutafuta KIBEN-TEN......Na huyo KIBEN Ten anakuwa na Mke...So MKE mkubwa above 35 anaenda kuolewa na Kiben-ten cha miaka 23 ambacho kinakuwa na MKe wa Miaka 22.......Jamaa yangu mambo ya ndoa yaache kama yalivyo.....na usije shangaa mke wako analiwa na mume wa mtu....
Maisha yanaweza yaka suprise mtu akatoka kwenye misimao yake. Kwa hiyo huwa sishangai watu wakifanya maamuzi fulani. Watu wanabadilika .
 
Maisha yanaweza yaka suprise mtu akatoka kwenye misimao yake. Kwa hiyo huwa sishangai watu wakifanya maamuzi fulani. Watu wanabadilika .

Maisha yanaweza kuku-suprise ndîo lakini hiyo haimaanishi kuwa unaweza kuvunja misimamo Fulani.

Mfano Kwa wewe unaweza kuwa shoga?
Hata Maisha yabadilike vipi naamini Huwezi kuwa hivyo, si ndîo?
 
As long as hawavunji sheria , wana haki ya kufanya wanvyoona vinafaa.

Nakubaliana na wéwe Kabisa

Ila Kwa Watibeli tunajua athari mbaya za Ndoa za milala na kuwa na michepuko ndîo maana Kwa Binti zetu Kamwe hawawezi kufikiri kitu kama hicho achilia mbali kukifanya.
 
Mwanamke anawezaje kuwa shoga?

Umesema Maisha yanaweza kuku-suprise Mpaka ukabadili maamuzi.
Ndîo nikakuuliza, wewe binafsi Kwa hoja hiyo, Maisha yanaweza kubadili maamuzi yako Siku Moja Ukawa Shoga?
Kama jibu ni hapana.

Elewa kuwa pia wàpo Wanawake ambao no matter what hawawezi kuolewa Mke WA pili Dunia ingalipo waô wakiwepo
 
Ndivyo mnavyojidanganya?

Mwanamke aliumbwa kwaajili ya Mwanaume. Umesema kweli lakini siô Mwanamke anayejitambua aumbwe akawe Nyumba ndogo au mke wa pili ilhali Wanaume Wengine wàpo. Huko ni kutojitambua
Kumbe ishu ni kuwa wa kwanza! Kwamba akiwa wa kwanza tu hakuna shida hata kama mwanaume akiendelea kuoa wanawake wengine!
 
Umesema Maisha yanaweza kuku-suprise Mpaka ukabadili maamuzi.
Ndîo nikakuuliza, wewe binafsi Kwa hoja hiyo, Maisha yanaweza kubadili maamuzi yako Siku Moja Ukawa Shoga?
Kama jibu ni hapana.

Elewa kuwa pia wàpo Wanawake ambao no matter what hawawezi kuolewa Mke WA pili Dunia ingalipo waô wakiwepo
Ni misimamo na mitazamo yao. Tatizo mnataka watu wawe na mitazamo sawa, hilo halitakaa liwezekane.
 
Ni misimamo na mitazamo yao. Tatizo mnataka watu wawe na mitazamo sawa, hilo halitakaa liwezekane.

Watibeli hatutaki mitazamo ya Watu íwe Sawa na yetu
Ila tunawatia Moyo wake weñye mitazamo Sawa na yetu kujiona wako Sahihi Kabisa.

NI Haki kîla Mtu kuwa na maonî na mtazamo wake
 
Watibeli hatutaki mitazamo ya Watu íwe Sawa na yetu
Ila tunawatia Moyo wake weñye mitazamo Sawa na yetu kujiona wako Sahihi Kabisa.

NI Haki kîla Mtu kuwa na maonî na mtazamo wake
Yes , wewe mtibeli baki na misimamo yako na wasio wabaki na yao.
 
Yes , wewe mtibeli baki na misimamo yako na wasio wabaki na yao.

Ndivyo ilivyo.
Weñye misimamo Yao sijawahi waingilia ndîo maana NI ngumu kunikuta kwèñye Uzi WA Mtu Mwingine akiwa na mtazamo au Msimamo Fulani nikimlazimisha awe na mtazamo kama wàngu.

Labda kama ni kujadili
 
Kwa Mwanamke anayejitambua hawezi kuolewa Mke wa pili hata iweje. Pia Mwanamke anayejitambua Kisha anajitegemea ndîo haiwezeniki Kabisa kuwa mke wa pili au mchepuko.

NI umaskini wa Wanawake ndîo unawafanya wakubali kishingo upande kuolewa wake wengi Huko kwèñye jamii za kifugaji.

Hizô Dini Wanawake Asilimia tisini na tisa hawakubali hicho kipengele. Alafu hicho kipengele kipô Kwa Matamanio ya Wanaume na waanzilishi wa hizô Dini.

Hata wazungu wàpo weye mtazamo wa kuoa Wake wengi.

Ninachopinga NI Mila Potofu
hakuna ulichonijibu mkuu. kuolewa mke wa pili sio laana wala kutokujitambua!
 
Back
Top Bottom