Aaahahahahha loooh umenikumbusha mbaliiii.....!!![emoji28][emoji28][emoji28]
Nakumbuka nilinusurika kubebwa, aliyeniokoa ni binamu yangu alikuja nyumbani kama katumwa na malaika.
Akasema Kasinde nna njaa naomba nipikie ugali na nswalu. Hapo karanga hadi nizisage kwenye jiwe unga hadi niutwange kwenye kinu. Na nilikiwa najiandaa kwenda kuchota maji.....
Utii wangu wa kumuandalia chakula binamu ndo uliniokoa kumbe vijana walijibanza wanibebe wanipeleke kwa jamaa halafu baada ya siku mbili walete zizi la ng’ombe nyumbani...
Hadi namaliza kumpikia binamu ilikuwa giza lishaingia sikwenda tena kuchota maji. Nilikuja kuambiwa baadae na rafiki zake kaka zangu ...![emoji1]