Nimekaa na huyu demu almost 3 years but I'm done.
- Ni mpole sana kwa kumwangalia tu hata anavozungumza
- Hajui make up wala mkorogo
- Anasali sana na nyimbo anazosikiliza ni za dini tu
- Hana mambo mengi sijui atoke aende disco sijui kwa marafiki. Ana ghetto lake lina kila kitu na anafanya kazi. Akitoka kazini anarudi kulala.
- Ni msiri sana hata kwa mambo ambayo angetakiwa ayafahamu mtu wake.
Yaaani ukibahatika kukutana nae, ndani ya week lazima utangaze ndoa.
Kilicho nichosha.
- Ni muongo muongo sana. Akikueleza kitu kichukue asilimia 50% zingine changanya na zako.
- Ni mbinafsi sana, chake ni chake lakini changu ni cha wote.
- Anapenda kufanya vitu kipekepeke yake. Atakushirikisha akipeleza pesa za kufanya hilo jambo, napo utaambiwa robo ya ukweli
- Simu yake ukishika utazimia, wanaume humo wamepangwa utafikiri danguro.
Inshort nataka nikushauri kuhusu kumwangalia MTU kwa nje na kumrefer kwa MTU mwingine, sio dili kabisa kwasababu mwisho wa siku tabia binafsi za mtu zinabaki kuwa too personal, hadi akae na muhusika wajuane ndio atangundua yaliyomo kama yamo au lah.