Mwanamke atakayenitongoza ndiye atakayenivumilia

Na nimepata maono kuwa mke wangu atakuja kwa stlye ya kunitongoza yeye yaani atakuja mwanamke huyo Ana sifa zote Tena anaweza akawa Ni bikra kabisa huyo ndo tutakwenda naye pamoja

Hili la Bikira kwa sasa achana nalo mkuu,, zingatia tu binti atakayekutongoza
 
Kuna kabinti flani hivii, kanatabia nzuriiii halafu kako nachuro.

Ngoja nikaelekeze ulivyo na ulipo kakutongoze.

Sina hakika kama ni kabikra ila ni kalutheri.

Wape hai hapo makao makuu [emoji4].
Nilengeshee mimi nikatongoze mwenyewe huyu yeye anasubiria atongozwe
 
Unataka kuangalia kama yaliyomo yamo?
 
Kama ulikuwa mchezeaji wanawake utakuwa ushapishana nae mkeo huko. Kuwa mpole utapata asie wako.
 
Niambie binti wa Tabora kwa wajanja😅
 
Nimekaa na huyu demu almost 3 years but I'm done.

  • Ni mpole sana kwa kumwangalia tu hata anavozungumza
  • Hajui make up wala mkorogo
  • Anasali sana na nyimbo anazosikiliza ni za dini tu
  • Hana mambo mengi sijui atoke aende disco sijui kwa marafiki. Ana ghetto lake lina kila kitu na anafanya kazi. Akitoka kazini anarudi kulala.
  • Ni msiri sana hata kwa mambo ambayo angetakiwa ayafahamu mtu wake.

Yaaani ukibahatika kukutana nae, ndani ya week lazima utangaze ndoa.

Kilicho nichosha.
  • Ni muongo muongo sana. Akikueleza kitu kichukue asilimia 50% zingine changanya na zako.
  • Ni mbinafsi sana, chake ni chake lakini changu ni cha wote.
  • Anapenda kufanya vitu kipekepeke yake. Atakushirikisha akipeleza pesa za kufanya hilo jambo, napo utaambiwa robo ya ukweli
  • Simu yake ukishika utazimia, wanaume humo wamepangwa utafikiri danguro.

Inshort nataka nikushauri kuhusu kumwangalia MTU kwa nje na kumrefer kwa MTU mwingine, sio dili kabisa kwasababu mwisho wa siku tabia binafsi za mtu zinabaki kuwa too personal, hadi akae na muhusika wajuane ndio atangundua yaliyomo kama yamo au lah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…