Mwanamke hata kujinunulia Vocha hawezi alafu analazimisha akushauri. Ujinga mtupu!

Mwanamke hata kujinunulia Vocha hawezi alafu analazimisha akushauri. Ujinga mtupu!

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
MWANAMKE HATA KUJINUNULIA VOCHA HAWEZI ALAFU ANALAZIMISHA AKUSHAURI. UJINGA MTUPU!

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Nyie dada zangu. Nilishawaambia mfanye kazi. Baadhi yenu bado vichwa ngumu. Hamtaki kujishughulisha.

Alafu ninyi ninyi ndio wakwanza kulalamika waume zenu hawawasikilizi, hawataki ushauri.

Aiseeh! Hata mimi sitakubali kupokea ushauri wa kiuchumi au pesa au uzalishaji mali kwa mtu ambaye hata vocha ya miatano tuu hawezi kujinunulia. Anasubiria kupiga vizinga wanaume. Na anaona ni kawaida kabisa.

Vijana, hakuna ushauri wa maana wowote, wakiuchumi utaupata kwa mtu ambaye ni ombaomba, anamtazamo wa kuhudumiwa. Kamwe!

Wanawake wengi hujiongelesha na kukushauri sio kwa sababu wana mawazo mazuri yenye tija. Au wanataka kweli ufanikiwe. Nope! Hiyo ni tricky tuu. Ni mind game wanakuchezea.

Lengo lao ni kujionyesha kwamba wanaakili na ni wife material 😄😆.
Na wanaume wengi wenye upeo mdogo sio rahisi kutambua jambo kama hilo. Hivyo hujikuta nyavuni.

Mtu hana hata biashara, hajui chochote kuhusu biashara. Ni ombaomba. Nauli hata ya elfu 5 ya kuja kukuona hana mpaka umtumie. Hivi huyo atakushauri jambo gani mzee?

Unajua wale wanaosema ndoa ni utapeli. Na ajira kwa wanawake wengi wapo sahihi kwa kiwango kikubwa.

Fikiria mtu ambaye alifeli Mathematics lakini anajifaragua na kutaka kukushauri kuhusu mambo ya geometry au algebra. Utamsikiliza?

Mwanamke muda wote anafuatilia udaku, umbea umbea, kutwa kukimbizana na nyimbo za kina Nandy na Diamond, kutwa kuangalia tamthilia za DSTV.
Kazi hana.
Kipato hana.
Lakini anang'ang'ania akushauri. Akushauri kitu gani wewe!

Binti yangu ukiona mumeo hafuati ushauri wako. Au hataki umshauri ujue ameshakuona upeo wako ni mdogo kwenye kile unachotaka kumshauri.

Baki kwenye laini yako. Fanya yale anayokuamini. Kama anakuamini kwenye malezi ya watoto. Jikite huko.
Kama anakuamini kwenye utunzaji wa nyumba, jikite huko.
Usiwe na kiherehere, hanisikilizi. Akusikilize una kipi chakusikilizwa kwenye hicho unachotaka kushauri?

Alafu wanawake wengi wao hupenda kujifanya wanakushauri ili ionekane walichangia.
Ukiwaambia wafanye wenyewe hawataki.

Anakupa wazo. Unamwambia hilo wazo halitekelezeki. Anakuambia ujaribu tuu. Na anakung'ang'aniza kabisa.
Sisi watibeli hatusikilizi.

Mwingine anakuambia nataka nianzishe biashara fulani. Unamwambia unamtaji? Anaanza kulialia, na kukulalamikia humsapoti.
Sasa mtu anasapoti biashara au wazo la biashara?

Wengine wanafikia hatua ya juu kabisa wanatishia wanaume, kwamba hunipendi, blah blah! Mara nitaondoka.
Kijana, usitishwe na maneno.
Hizo ni tricky, mingames kukuingiza katika mfumo wake.

Mwambie kama humpendi anafanya nini hapo? Aende huko anakopendwa.

Najaribu kusema nini? Usikubali mwanamke, mtoto au aliyechini yako yeyote kukuweka chini ya shinikizo. Kukulazimisha. Wewe ni kiongozi. Wewe ndiye kichwa cha nyumba.

Mkumbushe na muweke kwenye mipaka yake. Hataki aseme muagane kwa amani.

Chunguza familia nyingi hasa zilizodondoka. Au zisizo na mbele wala nyuma. Utakuta Mwanamke anamdomo na kujifanya anaakili kuliko mwanaume.

Mara zote utawasikia wakijifanya wanaakili na mawazo kuliko waume zao.
Na mtoto yeyote ambaye humwona mama anamawazo kuliko Baba yake Mara nyingi naye hujikuta amefeli.

Fuatilia familia zilizofanikiwa sana. Wasikilize wanawake wanavyoongea. Utasikia wakijivunia kumuamini mume wake. Kuamini katika akili ya mumewe.

Ni hatari kuishi na mwanamke ambaye haamini katika akili yako. Hakuamini.
Unamwambia hivi yeye anasema vile. Na analazimisha. Yaani ushauri wake anataka ndio uwe. Sisi Watibeli tunafukuza haraka sana.

Mfano, wewe kama Baba ushaona kipato chako hakitoshi kuwapeleka watoto shule fulani. Pia ushaona mbele kuwa hizi elimu ni biashara. Hakuna sababi ya kumpeleka mtoto shule ya gharama kubwa kwa kujitesa wakati mwisho wa siku mtoto atarudi mtaani.
Unampeleka mtoto shule ya kawaida. Mkeo anaanza kuleta fujo. Mtoto wangu ataenda shule hii.
Aiseeh! Labda kama wewe sio Baba. Sisi Watibeli hatutaki mabishano. Tunachokisema ndicho kinatakiwa kufanyika. Hauwezi jiuzulu kama Nchimbi. Sio lazima uwe mke wangu na wala sio lazima niwe mume wako. Hivyo yaani!

Baba na mtawala lazima ujue kusimamia unachokiamini. Pia kujua ushauri sio lazima na mwanamke ajue ushauri ni mpaka aombwe. Na kama atataka kushauri ni anatakiwa kuomba kutoa ushauri. Ni ruhusa yako kuamua kukubali ombi lake au kulikataa hata kusikia ushauri wenyewe unahusu nini. Hivyo ndivyo mwanaume unatakiwa kuwa.

Kama mwanamke hata match mfumo wako. Usimlazimishe, usimfundishe, usipoteze muda wako kuona mabadiliko.

Nimemaliza vijana. Msijesema hamkuambiwa.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom