Mwanamke jina Happyness Khalfan amekatwa mkono na mume wake kwa kukataa asisome sms kwenye simu yake baada ya kuchelewa kurudi nyumbani

Mwanamke jina Happyness Khalfan amekatwa mkono na mume wake kwa kukataa asisome sms kwenye simu yake baada ya kuchelewa kurudi nyumbani

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
#Repost @wasafifm
——
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Happyness Khalfan amekatwa mkono na mume wake Charles Peter kwa kosa la kukataa asisome ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu yake mara baada ya kuchelewa kurudi nyumbani.

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe Desemba 15, 2024 katika kata ya Mwendakulima halmashauri ya manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga SACP. Janeth Magomi ametoa ufafanuzi juu ya tukio hilo na kusema kuwa jeshi la polisi linaendela na ufuatiliaji wa kitendo hicho cha kikatili huku wivu wa mapenzi ukitajwa kuwa chanzo cha mwanamke huyo kufanyiwa kitendo hicho.

Akisimulia kwa njia ya simu mhanga wa tukio la kukatwa mkono Bi. Happyness Khalfan amesema kabla ya kufanyiwa kitendo hicho hakukuwa na ugomvi wowote kati yake na mumewe isipokuwa mara tu alipochelewa kurudi nyumbani ndipo alichukuwa panga na kumkata sehemu ya mkono wa kushoto.

Aidha kamanda Magomi ametoa rai kwa watu kutoa taarifa kwenye Jeshi la Polisi kupitia madawati ya jinsia pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na si kuyafumbia macho.

Cc: @officialkimoco
#WasafiDigital
 
Tumeshauriwa kuishi nao kwa akili...
Hawa alimwingiza Adam cha kike.
Samson naye Delila alimwingiza cha kike.
Ayub tu ndio alikomaa lakini alinusurika kuingizwa cha kike.
 
Kichwa cha habari ni ambiguous, nani alizuiwa kusoma sms ? Mume au mke
 
Tumeshauriwa kuishi nao kwa akili...
Hawa alimwingiza Adam cha kike.
Samson naye Delila alimwingiza cha kike.
Ayub tu ndio alikomaa lakini alinusurika kuingizwa cha kike.
Yusufu pia nilikomaa kutokula Mke wa Mfalme Potifa, usinidhulumu CV umwamba kwa vipochi manyoya...😏

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Ndio dawa yao...haiwezekani uhudumiwe alafu usitake kufuata masharti ya muhudumiaji.

Ukitaka uhuru wako usiolewe
 
Kataa Ndoa!
Ndoa ni kupokonywa uhuru wako binafsi 🤣
 
Back
Top Bottom