Mwanamke kusifiwa ni jambo la asili, iwe nyumbani, kazini au kwenye siasa, na watu wanapaswa kuelewa hilo

Mwanamke kusifiwa ni jambo la asili, iwe nyumbani, kazini au kwenye siasa, na watu wanapaswa kuelewa hilo

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Nikiwa shuleni kwa muda mref sana sikuweza kupata rafiki wa kike katika shule yetu ya mchanganyiko. Rafiki zangu wote walikuwa na girl friends. Siku moja rafiki yangu mmoja akaniambia, ukitaka msichana akupende msifie, hata kama unachomsifia sio kweli. Sasa nenda kajaribu hilo uone kama hutapata girl friend.

Basi nilipomwona msichana ninayependezwa nae, ambae huko nyuma nilimfuata na akanikataa, nikaanza kumsifia. Siku ya kwanza nikasema sketi zake zinampendeza sana. Siku nyingine nikasema alivyosuka nywele kilioni amependeza mno na ule mtindo unampendeza kuliko wasichana wengine! Siku nyingine nikasema anatembea kwa mvuto sana kama mwana mitindo!

Sasa baada ya hapo, ikawa hata akiniona kwa mbali ananifuata ili angalau asikie nikimpa sifa, na mimi nikawa hodari wa kumsifia, mara anavyocheka, macho yake, nk! Haikuchukua muda huyo msichana akawa ndio girl friend wangu!

Fast forward, nimekua mtu mzima. Rafiki yangu kzini akanipa siri kuwa mke wake huwa mara nyingi anamnyima haki yake ya ndoa! Nikamuuliza, huwa unamsifia? Akasema hapana. Nikasema hata kama tendo la ndoa ni haki yako, usipomsifia atakunyima tu. Basi kila mkienda kulala, tafuta kitu cha kumsifia usiku huo. Chakula alivyopika siku hiyo hta kama aliunguza, anavyonukia vizuri akitoka kuoga, alivyo bado na umbo kama vile mlivyotoka kuoana nk! Jamaa akaniambia I say, yaani siku hizi kupewa haki yangu ya ndoa wala siombi tena!

Fast forward tena, tunafika kwa Bashiru. Anasema kwamba Watanzania, hususa wakulima, hawapaswi kusifia mtu ili wapate haki yao, kwa sababu ni haki yao kupewa hiyo huduma.

Sasa nauliza hivi, hivi Bashiru, ameoa kweli? Bashiru, umeoa babaangu?

Basi waambie hao wakulima, wakitaka huduma bora, waendelee kumwaga sifa kwa wingi tuu, hata pale zisipostahili! Kuna wanasiasa wajanja walishagundua hilo siku nyingi!
 
Back
Top Bottom