Mwanamke kutojua kupika inaweza kuwa sababu ya kupewa talaka?

Joanah

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
22,527
Reaction score
79,976
What's up wakuu
Mko bwax?
Basi sawa(in chief engineer's voice)

Kwenu wakuu mliofanikiwa kuoa ama kuolewa ama wenye experience na hizi issues

Hivi ni muhimu kiasi hiko kwa mwanamke kufahamu namna ya kupika chakula?Leo katika stories za hapa na pale na my babes tukajikuta katika hii mada ya upishi

Kuna best yangu(kanizidi kama miaka minne hivi) aliolewa mwaka jana na ana miezi mitano tu katika ndoa yake . .nimepata ubuyu kuwa sasa hivi yupo kwao na talaka juu eti kisa tu alikuwa hajui kupika

Binafsi sijawahi kuona umuhimu wa kujua kupika

Asa wakuu hivi suala la kutojua kupika tu linaweza kufanya mtu akapewa talaka?
Naombeni kufahamishwa maana nishaanza kuogopa huku
 
Kwa wabongo kujua kupika ni muhimu. Wengi huwa hawapendi kula chakula cha HG na hasa ukitilia maanani baadhi ya HG walibambwa wakiweka mkojo au vitu vingine visivyostahili kuwekwa kwenye msosi.
 
Hii ni Africa dada! Jukumu la mke ukiacha na kutoa unyumba inabidi ajue kumtunza mume... Aweze kumpikia, kumfulia na ata kumfanyia usafi etc. Na mwanamke hadi unafika umri wa kuolewa hujui kupika ni picha mbaya, inaonesha ulivyo mzembe. Yaani ata kama mimi mwanaume, nakurudisha kwenu aisee!!!
 
Hizo ndio shida mnatoka kwa wazazi wenu mlizoea house girl ndio mfanyakazi wa kila kitu!
Wewe mtoto wa mwenye nyumba kuamka saa nne hata kuchemsha chai hujui!

Aende huko wazazi wake wakamfundishe kupika ebooo!
Waje rafiki zangu mtu unaleta chakula hakijaiva kwanini!
 
Kwa huu wivu nlokuwa nao Wala sicomment,
nadhani na wanaume wengine watapita kimya kimya......
 
Kwa wabongo kujua kupika ni muhimu. Wengi huwa hawapendi kula chakula cha HG na hasa ukitilia maanani baadhi ya HG walibambwa wakiweka mkojo au vitu vingine visivyostahili kuwekwa kwenye msosi.
Nafikiri huyu best yangu hakuweka jitihada za kufahamu kabla ya ndoa
 
Reactions: BAK
Inaonekana ni suala muhimu sana . .tutaacha uzembe
 
Hahahah
Mkuu umeongea kwa hisia zote [emoji28]
 
Ulizia hilo neno "kupika" linamapana gani ktk ndoa. Na kama hujui kupika kweli usiote ndoa aseeee, itakuwa masaa tu upo kwenu na maandishi
 
Mwanamke ndani ya nyumba mbali na yote basi ufanikiwe kuwa nayo haya matatu makubwa.... Ulimi unaotoa maneno matam kwa mmeo, ujue kumpikia mumeo chakula kizur kuijenga afya yake, na tatu chakula cha chumbani(kitandani) nacho ujue kukipika na kupakua vema. Nimekumegea tu ayo kwa uzoefu wangu wa miaka kadhaa ndani ya ndoa.
 
[emoji122] [emoji122] [emoji122] Shikamoo dada mzuri!.....nimekupenda bure yaani![emoji106]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…