Mwanamke Mgumba anayejielewa anahitajika awe na sifa hizi

Mwanamke Mgumba anayejielewa anahitajika awe na sifa hizi

Joshua P

Member
Joined
Jul 13, 2024
Posts
9
Reaction score
13
Habari wanaJF

Kichwa kimejieleza hapo juu ni jambo serious kwa huyu ndugu yetu kwani siku zote ukweli humweka mtu huru na amethubutu kuniweka wazi.

Ni mjomba wa miaka 36 lakini amejikuta anapitia changamoto nzito sana katika mahusiano yake kisa matatizo yake ya uzazi(ugumba).

Mimi sio mtalaam lakini ninavyomwona kwa jicho langu na kumsikia ninapoongea naye naona kabisa hayupo sawa jambo ambalo likanifanya nitafute muda mzuri wa kiongea naye kwa kina.

Baada ya kuonana naye Maongezi yetu yalikuwa hivi...

MIMI: kaka samahani huenda nikakukwaza kwa kuingilia maisha yako personal lakini mimi ni mdogo wako rafiki wa karibu sana napenda sana kuona kaka yangu upo sawa una amani na furaha lakini naukona haupo sawa kama hautojali naomba kujua kinachokusibu kaka yangu tafadhali...

YEYE: Mdogo wangu mimi nipo sawa kabisa mbona au unanionaje?
Hata hivyo wewe hupaswi kusema unaingilia maisha yangu binafsi wewe ni zaidi ya ndugu yangu na tumeishi vizuri kuzidi hata ndugu zangu wa damu nakushukuru kwa kujali ila kaka yako niko sawa.

MIMI: ni kweli kaka yumkini upo sawa kwa mwonekano wa nje na watu wakakuona hivyo lakini ndani ukawa na shida inayokutafuna kimya kimya na hakuna mtu asijue....mimi ni mwanaume mwenzako japo ni mdogo kwako lakini naona kuna jambo kwako halipo sawa ...najua ni maisha yako binafsi ndio nimetanguliza samahani kaka...una mpango gani kaka kuanzisha familia yako sababu naona umri unasogea sijawahi kukona na mwanamke hata kwa bahati mbaya toka kile kipindi umeachana na shemeji G..?

YEYE: sasa naanza kukuelewa mdogo wangu kumbe upo angle hii...kaka niliamua kuishi maisha yangu mara baada ya kuchana na shemeji yako G uliyekuwa unamwona sana. Ila kwa kuwa umeacha kazi zako na ratiba zako umenitafuta na kutaka kuongea na mimi wacha nikueleze kitu ambacho hukijui kuhusu mimi.

Mdogo wangu katika watu wote walionizunguka unaonekana wewe una jicho la huruma na kuona mbali zaidi...kaka yako sijabahatika kupata mwanamke atakayenipenda na kunikubali na hali yangu niliyo nayo kwani sina uwezo wa kumfanya mwanamke abebe ujauzito.

MIMI: samahani kaka sijakuelewa vizuri huna uwezo unamaanisha nini? Mnara hausomi au unasoma ila signals zinakata...?

YEYE: Mnara unasoma vizuri lakini siwezi kusababisha ujauzito utokee kwawanangu, na sina Bahati kwani wanawake wote niliohusiana nao wanataka kuzaa na kunyonyesha watoto wao hivyo nimekuwa napitia wakati mgumu sana hata shemeji yako G aliniacha kwa sababu hiyo alisema tumbo lake la uzazi linamletea maumivu asipozaa atateseka sana. Shemeji zako wengine waliniacha na dharau juu ndio maana nimeamua kuishi mwenyewe.

MIMI: pole sana kaka yangu lakini kama una simamisha vizuri japo mimi sio mtaalam wa afya lakini inaonekana tatizo lako sio kubwa tunaweza kupata ufumbuzi wa hilo jambo...je umeshawahi kwenda hospital kubwa na kuonana na wataalam bobezi wa hayo mambo walikuambiaje...?

YEYE: mdogo wangu nimezunguka sana hadi nje nimeenda kwa ajili ya hili lakini ndio hivyo haiwezekani hata kwenye maombi nilienda na naendelea kuenda mpaka leo hivyo nimejikubali na nimeamua niishi maisha yangu kwani kuna watu wengi wanakuwa wazima kabisa lakini wanapata magonjwa na kupelekea kukosa uwezo wa kuzaa au kusababisha mimba kwa mwanamke lakini bado wanaishi maisha yao ya furaha tu.

MIMI: sawa kaka najaribu kukuelewa lakini nataka kujua zaidi katika kuzunguka kote huko wataalam walikuambia kiini cha tatizo lako ni nini...? Je una ugonjwa uliopelekea hiyo hali kutokea.., sperms zako hazina ubora wa kusababisha mimba au ni tatizo la kuzaliwa nalo..., na walikupa ushauri gani kaka yangu...?

YEYE: Kumbe maswali kwako ni nature mimi nikajua ukubwani utaacha..anyways, sina ugonjwa wowote wa kuwa chanzo cha hili, nilizaliwa na hili tatizo mdogo wangu. Walinishauri ni adopt...bahati mbaya ni kuwa napata wanawake wanaotaka wabebe ujauzito kwa matumbo yao sio kuadopt watoto.

MIMI: pole sana kaka yangu lakini bado naamini unaweza kupata watoto kwani MUNGU yupo na hajawahi shindwa kwa lolote naomba kuwa na Imani maana Imani ni ushindi mkubwa usijilaumu wala kukata tamaa kaka yangu, to be honestly nilikuona umeshakata tamaa ya mahusiano kabisa na hali ndio imenifanya nitafute muda wa kuongea na wewe. na hapa nimepata picha vizuri inamaana akipatikana mwanamke ambaye atakupenda na kukubaliana na hali uliyo nayo upo tayari kwa mahusiano na utampenda pia ...?

YEYE: kwa sasa nimeamua kuishi mwenyewe mdogo wangu kusema akipatikana mwanamke ambaye atakubali hali yangu ni uongo sababu wengi wanakubali mwanzoni tu lakini mbeleni hubadilika na kuja na sababu nyingi hadi wengine wanaenda kubeba mimba nje ya ndoa tunajionea kwenye jamii, labda ikitokea nikapata mwanamke mgumba mwenzangu hapo tunaweza kuishi vizuri na kubebeana madhaifu yetu.

MIMI: duh kaka usiseme hivyo mimi naamini uliokutana nao na wakakukimbia kwa sababu ya hilo tatizo lako japo mimi sioni kama ni tatizo kubwa sana hawakuwa na upendo kwako na hawakuwa watu sahihi katika maisha yako wapo wanawake wazuri wenye roho nzuri heshima na upendo huwezi kukata tamaa hivyo na kuishi mwenyewe kaka yangu ujue sex pekee ni tiba ya akili na mambo mengi sasa kaka yangu mimi naomba tutafute shemeji naamini tutapata mwanamke mzuri mwelewa atakayekukubali jinsi ulivyo naamini wapo wengi.

YEYE: Tutafute mwanamke una maana gani mdogo wangu ? Ni kweli sex kwa mwanaume ni nzuri lakini kama inakuumiza na kukuhuzunisha haiwezi kuwa nzuri tena...kama nilivyokuambia nawish nipate mwanamke mwenye shida kama yangu hapo tumaini lipo naweza kuishi naye.

MIMI: sawa kaka nimekuelewa na Ahsante sana kwa kuniheshimu na kuniambia ukweli ambao nilikuwa siujui kabisa ni watu wachache sana wanaweza kusema hivyo ikizingatiwa umenizidi umri ungeweza hata kupuuzi na kuona shida msaada wowote kwenye hilo.

YEYE: Ni kweli kwani hata ndugu zangu hawajui na sipendi wajue kulinda heshima yangu hata wewe nimekuambia kwa sababu nakuheshimu alafu unajielewa sana but NAKUOMBA HII IWE SIRI YAKO USIJE UKAMWAMBIA MTU YEYOTE UTAKUWA UMENIDHALILISHA SANA.

MIMI: kaka nashukuru sana kwa kuniamini nitakutunzia siri kaka yangu kuwa na amani ila ninaombi kwako naomba unikubalie na ulipokee in positive way isione kama nimekudharau lahasha naomba unipe kazi mimi ya kumtafuta shemeji uliyewish unaweza kuwa naye katika mahusiano tafadhali.

YEYE: mdogo wangu unasemaje..?? yaani wewe unitafutie mwanamke mimi sasa hiyo ni dharau na tunaenda kudhalilisha Eboo! Uliona wapi mkubwa anatafutiwa mke na mdogo wake..?

MIMI: NO kaka sijakudharu na wala siwezi kufanya hivyo ndio maana nimeomba ulipokee in a positive way nia yangu ni njema na sitaki udhalilike katika hilo, kama ulivyosema wapo wanawake wengi sana ambao ni wagumba nao wameteswa sana na kunyanyasika kwa ugumba wao hivyo nimewaza mbali sana hiyo kazi naweza kuifanya naomba uniamini kaka yangu naamini tutapata na utafurahi.

YEYE: unachoongea sikielewi unataka kunitafutia wapi wewe unao hao wanawake au ? Si ndio mwanzo wa kuanza kutafuta wanawake social media huo udhalilishaji mimi sitaki kuusikia hapa mdogo tafadhali.

MIMI: hapana kaka niamini mdogo wako ni kweli sina wanawake wenye hiyo shida hata hivyo hata wangekuwepo nisingeweza kumbeba tu na kumleta kwako maana mahusiano ni suala la hisia pia sio kubebana tu kwa sababu wote mna shida inayofanana.
Lakini pia Mwanamke mwema anatoka kwa BWANA ila BWANA yupo kila mahali unaweza pata mwanamke mahali popote iwe kwenye gari, msibani, harusini, kwenye ndege, kwenye meli, kanisani, msikitini, mtaani hata kwenye mitando ya kijamii maana mitandao ya kijamii haitembelewi na wahuni tu ..kuna watu na akili zao wanajoelewa na kujiheshimu wapo huko...hivyo naomba hiyo kazi niache mimi wewe niambie tu unataka awe na sifa zipi ntakufanyia kazi kwa uaminifu mkubwa kaka yangu.

YEYE: Mdogo wangu suala la wewe kunitafutia mwanamke halijakaa sawa nakuheshimu sana na nakuamini sana ila kwenye hilo ni ngumu ...anyways nipe muda nitafakari kwanza nikakujibu.

MIMI: sawa kaka yangu mimi nimekulewa lakini wazo la kusema kukutafutia ni nimekudharau tafadhali naomba ulifute mimi siwezi kukudharau wewe hata kwa bahati mbaya kaka yangu, wewe tafakari kisha utaniambia...pia nashukuru sana kuwa muwazi kwangu na kunipa muda wa kuongea na wewe haswa yaliyoka ndani ya moyo wako.

YEYE: poa poa mdogo wangu shukrani pia kwa muda wako, sasa nadhani nikukimbie kidogo leo Yanga anacheza wacha nikamwangalie muda umefika.

MIMI: sawa bro kila la kheri.

BAADA YA MIEZI 3

YEYE: Mdogo wangu nimetafakari hakuna shina waweza kufanya kama ulivyonishauri.

SIFA ZA MWANAMKE

1. Mgumba
2. 26-33 yrs
3. Mkristo
4. Mwembamba wastani
5. Rangi yeyote bt asiwe amejichubua/anajichubua.
6. Asiwe mchaga.
7. Awe Tayari kupima afya.
8. Mpole, mtii na mwenye heshima.

MIMI: sawa kaka yangu ahsante kwa kuniamini wacha nikufanyie kazi.

SIF ZA MWANAUME

1. Mpole, starabu, mgumba, mkarimu sana ila ni utopolo wa kutupwa🤣
2. Rangi yake si mweupe sana sio mweusi sana
3. Anajielewa sana always anawaza mafanikio.
4. Urefu wa kati sio mrefu sana wala sio mfupi.
5. Ni mwembamba wa kati.


Walengwa PM iko wazi karibuni sana sifa zingine mtajionea wenyewe😃 mimi yangu ni hayo. Ahsanteni kwa muda wenu wa kusoma hili gazeti refu na linachosha.
 
Hii nafasi ingemfaa dada yangu mmoja hivi sema tatizo, sijui kama yupo tayari kuishi na mwanaume
 
SIFA ZA MWANAMKE

1. Mgumba
2. 26-33 yrs
3. Mkristo
4. Mwembamba wastani
5. Rangi yeyote bt asiwe amejichubua/anajichubua.
6. Asiwe mchaga.
7. Awe Tayari kupima afya.
8. Mpole, mtii na mwenye heshima.
Mbona ukabila tena jomba? Kwani Wachagga wana ubaya gani?
 
Back
Top Bottom