Mwanamke mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika: Chanzo na tiba yake

Mimi siyo daktari..... lakini nakumbuka wakati wa ujauzito wa kwanza nilipatwa na hiyo hali, ilinitesa sana. nakumbuka daktari wangu aliniambia hiyo hali itakuwepo mpaka angalau nimalize ile robo ya kwanza, na kweli ilikuwa hivyo. Nakumbuka siku moja nilimlazimisha dada mmoja muuzaji wa duka la madawa anichome sindano ya kuzuia kutapika maana niliona kama siku zangu ndo zimeisha...... mdada wa watu ilimbidi avunje masharti ya ofisi yake na kunichoma sindano.
Daktari wangu alinishauri kutumia dawa za kuzuia kutapika kila siku asubuhi kabisa nikiamka tu. kwa hiyo nilikuwa nafanya hivyo. Nikiamka tu dawa, then napumzika kidogo halafu napiga mswaki, napata breakfast. nilikuwa nikifanya hivyo kweli sitapiki siku nzima.
 

mkuu ni kawaida,mimi nilitapika sana mpaka nikawa nasikia kizunguzungu,yani ilibidi niende hospitaly nikapewa dawa za kuzuia kichefuchefu ila hazikusaidia nikaachana nazo,miezi mitatu ya mwanzo kutapika,kutema mte na adha zingine ni kawaida,ila zitzisha
 
Kunywa chai ya tangawizi the fist thing in the morning hata kabla hujapiga mswaki, and mind you tangawizi iwe mbichi na usiweke hata sukari, kuna watu wamwshauri dawa za kuzuia kutapika lakini wataalamu hawashauri sana mama mjamzito kutumia madawa. Cha muhimu ni kujaribu kutafuta natural ways za kuzuia tatizo kama hiyo ya kunywa tangawizi mbichi bila sukari the first thing in the morning.
 
mimi sio daktari ila kuna vidonge vinaitwa nosic ni vzur vnasaidia kuzuia kutapika...asubuh kabla ya kula chochote ameze ni 1 mara 2,ila hali ya kutapka ikiisha anashauriwa kuacha..
 
huwa inatokea lakini sio kwa kila mwanamke mara nyingi huwa kwa kipindu kifupi tu ila kama ni mfululizo ni vizur aonane na madaktari
 
Pole sana hii ni hali inayotokana na mabadiliko ya chachu mwilini (Hormones) ila wakati mwingine inawezekana kuna upungufu wa madini katika mwili ambao unakupa hali yakusikia kama kuna udongo so jitahidi kupata balance diet na ikibidi jitahidi kupata vyakula vyenye protein ikiweza kupata mayai ya kware (quail eggs) ukachemsha yanasaidia
 
Ipo dawa japo mi sikuitumia niliogopa. Hospitali watampa kama wanaona ni serious. Ila miezi 3-4 ya mwanzo ni kawaida. Mimi nilikuwa nachemsha maji naweka tangawizi bila majani ya chai then naweka glucose kama sukari vijiko viwili nakunywa. Hii ilinisaidia nisiishiwe nguvu. I used to drink this kama mara 3 kwa siku
 
Kichefuchefu hakina dawa hasa kwa mjamzito, ni hali ya kawaida kabisa, labda useme kutapika
 
Msaada mini DAWA ya kichefuchefu kwa mjamzito

pole kwa shida ulionao hili tatizo lako halina sababu maalum ila laweza kusababishwa na mabadiliko ya mwili hii ni hali ya kawaida kwa mwanamke anapokuwa mjamzito maana kuna kitu kipya kimeingia 1. hakikisha wewe unakuwa katika hali ya usafi wakati wote pamoja na usafi wa nyumba iwe na hewa ya kutosha .2 epuka vyakula vyenye mafuta mengi 3 epuka kunywa maji mengi wakati wa kula ikiwezekana acha kunywa maji wakati wa kula, subiri baada ya muda kidogo ndo unywe maji 4 pata muda wa kupumzika 5 punguza stress
 
Tangawizi inasaidia sana.....


Chemsha maji na tangawizi alafu weka sukar kdg au majani ukipenda.....

Unaweza weka tangawizi katika chakula chako pia inasaidia....
 
Nosic ni dawa nzuri sana kwa kichefuchefu cha ujauzito. Maana kuna kichefuchefu kingine kikikupata unataman hata kulia, kutapika hutapiki ila cha moto unakiona.
 
Nosic ni dawa nzuri sana kwa kichefuchefu cha ujauzito. Maana kuna kichefuchefu kingine kikikupata unataman hata kulia, kutapika hutapiki ila cha moto unakiona.

Ni kweli kuna kipindi nlitumia hii dawa ikanisaidia.
 
Nosic ni dawa nzuri sana kwa kichefuchefu cha ujauzito. Maana kuna kichefuchefu kingine kikikupata unataman hata kulia, kutapika hutapiki ila cha moto unakiona.

Kwa mimba ya muda wowote mana kuna DAWA haziruhusiwi kwa mimba ya muda flani
 
Habari wana JF,

Mpenzi wangu ana mimba ya miezi mitatu. Tatizo mara nyingi asubuhi huwa anatapika hata kama hajala chochote na jioni pia huwa anatapika akionja chakula tu. Hii kitu inaniumiza sana, maana siku nyingine analala bila kula. Mwenye ujuzi anifahamishe, nini tatizo?
 
Sio tatizo ni mchakato tuu, avumilie kitaisha hakuna tiba rasmi, zaidi ya kujifungua/ Ku abbort
 

akiamka atafune tangawizi mbichi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…