Mwanamke mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika: Chanzo na tiba yake

Mwanamke mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika: Chanzo na tiba yake

Mkuu hiyo hali ni kawaida kwa baadhi ya wanawake hasa kwenye first trimester ( kipindi cha miezi 3 ya kwanza ya mimba ) itakwisha au kwa wengine inaendelea kwa kipindi chote cha ujauzito ila anaweza kutumia vidonge vya Nosic kutwa mara 2 kwa siku 5 au vidonge vya Vomidoxin.
Ok nimekupata mkuu.
 
Pole sana , hiyo ni hali y akawaida, usitoe mimba ni dhambi, nenda hospitali ya Serikali iliyokaribu na wewe jieleze kwa Dr utasaidiwa tu,

Mimi nilikuwa na tatizo kama hilo miezi mitatu iliyopita, sasa niko fiti , Kunadawa inaitwa NOSIC na nyingine ni Domperidon ( sina hakika na spelling) zitakusaidia sana, bei ni Tshs 2,000/=

nenda kamuone Dr usinywe dawa bila kuonana na Dr, kwa kipindi hicho ni hatari kujinywea dawa bila ushauri wa Dr, Pole sana natumaini ukienda kwa Dr utatulia na kazini utaenda vizuri tu. Mungu akusaidie pole sana
 
Wadau salamu!
Naishi Morogoro.Shemeji yenu ni mjamzito wa miezi 2 kuelekea wa 3 sasa anatapika sana tumejaribu kutumia dawa z kuzuia kutapika akini hazisaidii, tumejaribu na sindano lakn haisaidii. Tkieda kw Daktari anasema ni hali ya kawaida itaisha. Naombeni ushauri kama kuna namna/dawa ya kusaidia kuzuia kutapika. Kuna daktari mmoja alsema hiyohali ikizid watalazimika kumanyia Abortion kumnusuru mama. Wataalam naomben ushauri.
 
Kawaida kaka naomba Kama Hana presha awe anatumia tangawizi yan atafune au aisage then achemshe Kama chai alaf anywe kila cku afanye hvyo asbh na jioni. Mim nilitapika sana kiasi kwamba nilibakia mbavu tu bt nilivyoelekezwa hiyo tiba humu jf na mzizimkavu Hali hiyo ikaisha kabisa na sasa nakula vzr tu na hamu ya kula ipo.
Nb: asitumie majani ya chai wala kahawa kabisa pia asile vyakula vilivyochacha au kupikwa kwa muda mrefu then ahakikishe anajilazimisha kunywa maji mengi sana na vitu vya kuongeza damu Kama matunda na mboga za majani. Asante!
 
Hiyo hali ya kawaida tu kama alivyosema daktari, itaisha tu baada ya muda. Hongereni sana mkuu.

Hiyo nadhani itakuwa mimba yake ya kwanza. Huwa zinakuwa na mambo sana, unaweza kudata. Usiwe na khofu mkuu tulieni tu.
 
Madocta naombeni msaada ninaujauzito wa miezi miwili sili chakula chochote nikinywa maji natapika nakunywa maziwa tu! Mate yanajaa mdomoni natema ovyo! Naombeni msaada nitumie dawa gani jamani nimekonda sana
 
Unahitaji kufanyiwa vipimo ili kuonyesha kama ujauzito uko sawa.

Hali ya kichefuchefu na kutapika ni kawaida kwa wajawazito lakini hali hiyo uzidi kwa wale wenye mapacha au matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma.

Njia zinazotimiwa kupunguza kichefuchefu na kutapika ni pamoja na kutumia tangawizi, kula kiasi kidogo kidogo lakini mara nyingi kwa siku na hali ikizidi zipo sindano na vidonge.

Kwa kawaida hali ya kutapika hupungua na kuisha kabisa kadri ujauzito unavyokua.

Pole kwa changamoto na kila la heri katika matunzo ya ujauzito na kujifungua.
 
Ndg wanajamvi nimerudi tena nikihitaji ushauri na tiba kwa ajili ya mama watoto wangu.
Kawaida ni tendo la kumshukuru Mungu pale unapofahamu kuwa mama watoto wako ni mjamzito, hasa pale mnapokuwa mmejiandaa ktk hilo.
Lakini pamoja na furaha hiyo ya kusubiria kiumbe kipya kwangu imeonekana kama nimemletea balaa mke wangu, kwani amekuwa mtu wa kutapika kila siku name kila anachokula hukitapika sasa hataki chakula aina yeyote.
Sasa wataalam na wadau wote naomba kujua kama kuna dawa ya kuzuia au kutibu hali hiyo kwani inamfanya hata mwili kukosa nguvu.
Nimejaribu kuuliza majirani name marafiki wengi majibu yao ni kuwa hiyo hali eti haina dawa. Sasa nimeamua kuleta kwenu wadau kwa msaada zaidi. Nawasilisha.
 
Ajitahidi kula. Lazima kuna kitu kinapita. mi ilikuwa maziwa na matunda. hamna dawa ilonisaidia.
 
Ngoja waje madaktari;
Japo ni hali ya kawaida, hasa kwa miaka hii kila ujauzito una matatizo yake;
Atateseka hivyo ila kufa hawezi kufa; Ni uhakikishe tu hapungukiwi maji mwilini.
 
Wanawake tumetofautiana...kuna wanaotapika kipindi chote cha ujauzito wengine ujauzito ukiwa mchanga au akihisi harufu ya kitu chochote ie chakula,manukato etc na wengine ni kichefuchefu tu wala hatapiki..

Ajitahidi kula hasa vimininika na matunda kwa wingi,msosi ajilazimishe tu coz hata akitapika hakitok chote
Hongereni,poleni kwa challenges na malezi mema
 
Well this is my first pregy na nipo zaidi ya nusu ya safari yangu na sijawah kutapika ila nina uchaguzi tu wa vyakula

Tumetofautiana ila usiogope ni hali ya mpito
 
Back
Top Bottom