Mwanamke mpole na mtulivu sana

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
2,977
Reaction score
3,798
Niliwahi kufundisha chuo kikuu kimoja hapa Tanzania. Nilikuwa na mwanafunzi mmoja—mpole, mkimya, hana makuu, hanywi pombe, haendi out, ni mtulivu sijapata kuona.

Ni Mkristo, lakini huvaa ushungi kila siku, na darasani alikuwa wastani tu. Alimaliza na alipata kazi mji huohuo aliposomea. Baada ya miaka miwili, nilienda kumtembelea alipopanga. Nilimkuta na sifa zake zilezile.

Niliongea naye sana, na akaniambia kuwa mpaka sasa hajapata mchumba japo anatafuta sana mwenza na anasali kila siku. Nilishangaa, mdada mzuri kama huyo kukosa mume. Kweli, hata mimi roho inaniuma sana.
 
Upole si sababu ya Mtu kuwa Binadamu, kinyume chake ni sawa na Mtu aliyezaliwa na ukarimu ila kihulka ni Mkali au Mkorofi.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…